Tafuta

Tarehe 10 Novemba 2019 inatarajiwa kufanyika Ibada ya Misa Takatifu Kitaifa katika kituo cha Msimbazi jijini Dar Es Salaam Tanzania kwa ajili ya kufunga Mwezi Maalum wa Kimisionari Oktoba 2019 Tarehe 10 Novemba 2019 inatarajiwa kufanyika Ibada ya Misa Takatifu Kitaifa katika kituo cha Msimbazi jijini Dar Es Salaam Tanzania kwa ajili ya kufunga Mwezi Maalum wa Kimisionari Oktoba 2019 

Misa kitaifa ya kufunga Mwezi Maalum wa Kimisionari itafanyika 10 Nov,huko Dar Es Salaam!

Misa takatifu Kitaifa ya kufunga Mwezi Maalumu wa Kimisionari Oktoba 2019,itafanyika Msimbazi,Dar- es- Saalam Tanzania.Askofu Mkuu Nyaisonga ataongoza Misa kwa ushiriki wa Askofu mkuu Giampietro Dal Toso,Katibu Mwambata,Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu na Rais wa Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa;maaskofu,mapadre,watawa na walei.Na wakati huo huo tarehe 9-15 Novemba utafanyika mkutano wa NDESA.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 10 Novemba 2019 itafanyika madhimisho ya kitaifa  jijini Dar es Salaam- Tazania  kwa ajili ya kufunga Mwezi Maalumu wa Kimisionari Oktoba 2019 ambao umeoongozwa na kauli mbiu: “Mmebatizwa na kutumwa: Kanisa la Kristo katika utume ulimwenguni. Maadhimisho ya Misa Takatifu yatafanyika katika uwanja wa kito cha  Msimbazi na kuongozwa na Rais wa Baraza la Maaskofu katoliki, Askofu Mkuu Gervase Nyaisonga, wa Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya Tanzania.

Mkutano wa Mashirika ya kimisionari ya kipapa kwa nchi za lugha ya kingereza (Ndesa)

Hata hivyo kufuatia na tukio hilo taarifa zinabainisha kuwa wakati wa maadhimisho Kanisa katoliki Tanzania litamkaribisha Askofu mkuu Giampietro Dal Toso, Katibu Mwambata wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu na Rais wa Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa na wakarugenzi wote kitaifa wa Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa pia kutoka katika nchi za Afrika zinazozungumza kingereza  (NDESA) ambao pia wanatarajia kuanza mkutano wao wa Kanda kuanzia tarehe 9 hadi 15 Novemba 2019.  Mkutano huo kwa kawaida hufanyika kila baada ya miaka miwili, na mkutano wao  wa nara ya mwisho ulifanyika huko Harare Zimbabwe kunako 2017.

Zaidi ya waamini 2000 watashiriki maadhimisho ya kufunga na tuzo la washindi litatolewa

Taarifa kuhusu maadhimisho ya Kufunga Mwezi Maalum wa Kimisionari yanatarajiwa kuudhuriwa na zaidi ya waamini 2,000 wakiwemo Maaskofu, waratibu wa majimbo yote  katoliki ya Tanzania pamoja na wakarugenzi wote wa kitaifa wa Mashirika ya Kimisionari ya Kipapa PMS. Kadhalika watakuwapo wawakilishi kila  majimbo yote katoliki nchini Tanzania: mapadre, watawa/makatekista na waamini walei. Chama cha Utoto Mtakatifu cha Jimbo Kuu la Dar Es Salam watawakilisha watoto wote wa Majimbo yote katoliki ya Tanzania.  Baada ya Maadhimisho ya Misa Takatifu kwa ajili ya kufunga Mwezi Maalum wa Kimisionari, Oktoba 2019, Askofu Mkuu Dal Toso atawatunukia tuzo Majimbo yaliyoshiriki shindano ambalo limewekwa kwa ajili fursa ya Mwezi Maalum wa Kimisionari 2019.

MWEZI MAALUM
04 November 2019, 15:17