Tafuta

Vatican News
Maendeleo fungamani ya watu,njia ya amani  na njia ya wakati endelevu Maendeleo fungamani ya watu,njia ya amani na njia ya wakati endelevu 

Pwani ya Pembe:Serikali yahamasisha haki na amani kijamii!

Katika mtazamio wa kuadhimisha miaka 50 tangu mkataba wa mahusiano ya kidiplomasia kati ya Vatican na nchi ya Pwani ya Pembe na Ubalozi wa Vatican nchini humo kwa ushirikiano na Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya watu,wameandaa Semina ya siku mbili ya 13 na 14 Novemba jijini Abidjan nchini humo.Semina hiyo imeongozwa na mada:maendeleo fungamani ya watu,njia ya amani na njia ya wakati endelevu.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Ni mapendekezo 10 yalitolewa katika semina iliyoongozwa na mada ya “maendeleo fungamani ya watu, njia ya amani na njia ya wakati endelevu. Semina hiyo ilifanyika siku mbili ya tarehe 13 na 14 Novemba jijini Abidjan nchini Pwani ya Pembe (Ivory Coast). Semina hii imeandaliwa na ubalozi wa kitume wa Vatican nchini Pwani ya Pembe kwa kushirikiana na Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo fungamani ya watu, katika mtazamio wa mwaka 2020 wakati watakapoadimisha Jubilei ya miaka 50 tangu kuwapo mkataba wa mahusiano ya kidiplomasia kati ya Vatican na nchi ya Pwani ya Pembe.

Kwa mujibu wa taarifa za habari kutoka Shirika la habari za kimisionari, Fides, washiriki wa semina hiyo walikuwa hawali ya yote ni wawakilishi wa serikali ya Pwani ya Pembe, viongozi wa kidini na wadau wa jamii ya umma ambao wameshiriki hata kuandaa mapendekezo 10 wakati wa kazi yao na ambayo imeoneshwa na Dk. Guouéra kutoka katika ofisi ya Baraza la Kipapa la Maendeleo fungamani ya watu.

Mapendekezo hayo ni kama ifuatavyo:

1) Washiriki wanaalika Serikali na vyuo vikuu kuzingatia maelekezo na  kuchukua hatua kwa ajili ya hali halisi ya mendeleo fungamani;

2) Serikali inaombwa kuongeza nguvu za kisheria ambazo zinahamasisha haki kijamii;

3) Serikali lazima izingatie matokeo ya watu wanaofaidikia na mipango ya maendeleo hata wakati wa ujenzi wa miundo mbinu;

4) Serikali, vyama na wadau wa kijamii wanapaswa kujikita kwa dhati katika kutoa kipaumbel cha nchi;

5)Vyama vya kisiasa lazima wahamasishe maisha ya kidemokrasia ya kijamii katika imani yao ;

6) Viongozi wa kidini na waamini wanaalikwa kuishi ukuu wa kijamii katika imani yao;

7) Wadau wa kiuchumi wanaalikwa kufanya kazi kwa uwajibikaji huku wakihamasisha usawa wa haki kwa wafanyakazi;

8) Familia, walimu, na vyombo ya habari vinapaswa kuhamasisha utamaduni wa kuheshimu na ukaribu hata katika kizazi tofauti;

9)  Serikali na vyamana vinatakiwa  kuwa wadau wa kijamii na kujitahidi kwa ari kwa ajili ya amani na ili kuzuia kuzuka kwa mivutano; na hatimaye

10) Serikali na wadau wa kiuchumi, wanaalikwa kuwatia moyo wazalishaji wa chakula ambao wanawezeaka kutoa vyakula bora kulingana na utofauti wa abinuai.

19 November 2019, 15:21