Tafuta

Kardinali  Jean-Claude Hollerich anasema zaidi ya hasira ni kilio cha kutisha cha watu waliokufa katika njia za uhamiaji Kardinali Jean-Claude Hollerich anasema zaidi ya hasira ni kilio cha kutisha cha watu waliokufa katika njia za uhamiaji 

Sala ya Mabaraza ya Maaskofu kwa ajili ya Bara la Ulaya

Katika maombi ya wawalikishi wa maaskofu wa mabaraza ya Maaskofu wa Umoja wa Ulaya yaliyo fanyika tarehe 23 Oktoba huko Bruxelles wakati wa kufungua Mkutanao wao,wanaombea wahamiaji na wakimbizi hasa siku ambayo imepatikana maiti39 mjini London wakiwa kwenye konteina.Wanaombea wanasiasa na viongozi wapya katika Tume ya Bunge iliwawe busara ya kutoa maamuzi katika roho ya huduma na kuhamaisisha ustawi wa wote.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika Kanisa la Notre Dame du Sablon,huko  Bruxelles,tareh 23 Oktoba, maasofu wawakilishi wa Mabaraza ya Maaskofu wa Umoja wa Ulaya , wameadhimisha Misa Takatifu kwa ajili ya kuliombea bara la Ulaya wakati wa ufunguzi wa Mkutano.Katika maombi yao wamekumbuka kusali kwa ajili ya wakimbizi na wahamiaji, siku ambayo mjini Londoni wamekuta miili ya watu  39 wakiwa katika Konteina, kwa ajili ya wanasiasa ili katika kipindi hiki  cha hatua ya kuelekea katika Bunge na viongozi wapya wa Tume waweze kuchukua maamuzi yao kwa busara, roho ya huduma na kuhamasisha ustawi wa wote, huku wakiwa na umakini kwa watu walio masikini zaidi na wanaoishi katika bara hili.

Maombi kwa ajili  ya Ulaya na zaidi masikini wanaoishi humo

Aidha katika maombi wanasali kwa ajili ya amani katika Nchi zenye waathirika wa vita na kutumia nguvu. Kwa ajili ya wakimbizi na kwa ajili ya wale ambao wanajikita kuwasaidia. Kwa ajili ya wahusika wa  sera za kisiasa na ili waweze kutambua kuchukua maamuzi yao yenye busara katika roho ya kuhamasisha wema wa pamoja, huku wakizingatia na kuwa makini kwa wale wote waathirika kwa namna moja wale wasio kuwa na sauti katika jamii. Maaskofu hao wawakilisho wa Mabaraza yote ya Maaskofu ya Umoja wa Ulaya, kwa hakika katika kukutana kwao kwenye Kanisa hilo la Notre Dame du Sablon huko Bruxelles, ilikuwa ni siku ambayo kwa hakika imekuwa nzito. Naye katibu Mkuu wa Baraza la Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Ulaya (Comece), Padre Manuel Barrios Prieto akizungumzia kuhusu hilo amesema kwa dhati katika siku hizi Ulaya inakabiliana na hatua mpya ya Bunge na Tume mpya yake. Katika mada za Mkutano wao, Maaskofu watakabiliana kuona ni jinsi gani ya kutoa mchango kama Kanisa barani Ulaya kwenye mchakato nsuna wa shughuli za  Ulaya ili kukuza hali ya majadiliano, usikivu, usindikizwaji leo hii katika ardhi hii ya kuweza kuwa sauti ya kinabii.  Hata hivyo Baraza hili limetingishwa sana na habari za upatikanaji wa miili 39 isiyokuwa na maisha ndani ya Konteina. Janga hili limetokea katika eneo la kiwanda cha Essex kusini mashariki mwa Uingereza. Na miongoni mwa waathirika hao kuna hata kijana. Lori hilo lilikuwa linatokea nchini Burgaria, na labda janga hili pia linahusishwa na uhamiaji haramu.

Ni kashfa kwamba leo hii bado  Ulaya watu wanaweza kufa kwa namna hii

Zaidi ya hasira, ni kilio cha kutisha anachosema Kardinali Jean-Claude Hollerich, Askofu Mkuu wa Lussemburg na Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Umoja wa Ulaya. “Kama wakristo hatuwezi kunyamaza. Ninajiuliza, namna gani ya kuzungumzia utambulisho wa kikristo iwapo watu wanaendelea kufa namna hii na katika majanga hayatugusi zaidi? Wazo la Kardinali Hollerich limewandea haraka wahusika wa kisiasa.  Na kwa maana hiyo anasema , wafu wanasema na  zaidi wanapaza sauti  zao kwamba kuna dharura ya kufanya katika sera za kisiasa kuhusu wahamiaji na wakimbizi.  Hii haitoshi,  tunapaswa hata kusaidia Nchi mahalia mahali wanapotoka hao wakimbizi na wahamiaji. Kutengeneza mpango ulio mkubwa zaidi kwa ngazi ya kuweza kutoa msaada. Kardinali akiwa  ni mmoja wa wa washiriki  jijini Roma katika  fursa ya Sinodi inayoendelea kuhusu Amazonia, amebainisha kuwa "mabadiliko ya tabianchi bado yataendelea kusababisha hali kuwa ngumu na wakati huo huo wahamiaji bado wataendelea kuongezeka".

Jitihada za kuunda mawazo chanya na ushawishi wa maendeleo ya sheria

Kuna uhusiano wa moja kwa moja kati kusali na  jitihada za kuunda mawazo chanya na kushawishi wa maendeleo ya sheria, anasema Askofu Mariano Crociata, wa jimbo katoliki  la Latina nchini Italia na ambaye ni Makamu rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Umoja wa Ulaya. Yeye anasema Kanisa la Ulaya haliwezi  kugeuza uso wake sehemu nyingine, bila kugutushwa na uchungu wa miili ya watu waliokufa katika njia za uhamiaji haramu. Askofu anabainisha kwamba,  hakuna mtu hadi sasa barani Ulaya na katika nchi binafsi ameweze kuchukua uamuzi wa dharura hii mikononi mwake na wakati huo ni kusukumizana mmoja na mwingine na wakati mataja na matatizo makubwa yanaendelea kutukia hasa katika vituo vya mapokezi. Kwa hakika ni kipindi kigumu na cha dharura zaidi kuliko awali cha matukio haya ya uhamiaji katika nchi mahalia na ambapo inahitajika mbinu mkakati wa kutoa vibali vya kuingia katika nchi yoyote ile kihalali.

24 October 2019, 17:00