Tafuta

Vatican News
Ni miaka 800 tangu Mtakatifu Francis wa Assisi alipokutana na Sultani wa Misri AL-Kamil kunako mwaka 1219 Ni miaka 800 tangu Mtakatifu Francis wa Assisi alipokutana na Sultani wa Misri AL-Kamil kunako mwaka 1219 

Ni miaka 800 tangu ufanyike mkutano wa Mt.Francis na Sultani wa Misri!

Mji Mtakatifu wa Yerusalemu unajiandaa kufanya kumbukumbu ya miaka 800 tangu Mtakatifu Francis wa Assisi alipokutana na Sultani.Ili kuweza kuishi kwa namna ya pekee siku hiyo wamefungua milango wazi kukaribisha mkutano unaohusu tukio la hija ya amani ya Mtakatifu Francis wa Assisi katika Mji Mtakatifu kunako mwaka 1219.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Mji wa Yerusalem unajiandaa kuadhimisha tukio muhimu. Hii ina maana ya kuelezea tukio hili kama moja ya ishara ya amani katika historia ya majadiliano kati ya Wakristo na waislam. Ni miaka 800 iliyopita tangu  Mtakatifu Francis wa Assisi na Sultani wa Misri Malek al-Kamel, walipokutana ikiwa ni katika mchakato wa Vita vya tano, kunako Juni 1219. Mtakatifu Francis wa Assisi baada ya majaribu yake ya kutaka upatanisho na kushindwa kwa  amani, yeye pamoja na ndugu wadogo walipanda mtumbwi wakiwa na wafanya biashara na kuifikia bandari ya Mtakatifu Yohane wa Acri Kaskazini mwa nchi ya Palestina (kwa sasa inaitwa  Israeli ya Acri) akiwa  na nia ya kukutana na Sultani wa Misri.

Mkutano huo labda ulifanyika  kati ya mwezi Agosti na Septemba, katika bandari ya Damietta, kwenye bonde la Nile, karibu kilomita 200 kaskazini mwa Cairo, ambapo mpwa wa Saladin, kwa mujibu wa ushauri wa wakuu wake, aliwakaribisha kwa heshima kubwa, akawapa hata zawadi ambazo zilikataliwa kwa heshima ya kiapo cha umaskini. Katika kukumbuka tukio hilo Yerusalemu kuanzia 30 Septemba hadi  alhamisi 3 imefunguliwa milango kwa ajili ya kufanya kumbukumbu ya miaka 800 tangu  hija ya amani ya Mtakatifu Francis wa Asisi katika nchi Takatifu (1219-2019). Tukio hili limeandaliwa na Ndugu wadogo wafransiskani wa usimamizi wa Nchi Takatifu.

Naye Padre Francisko Pattoni msimamizi wa nchi Takatifu akizungumza na Vatican ameelezea kuwa ni kumbukumbu ya miaka 800 kamili ambapo Mtakatifu Francisko wa Assisi alikwenda hija na kushuhuda amani kubaki  huko  hadi mwaka 1220 aliporudi Italia. Aidha Padre Pattone amekumbuka kuwa Mtakatifu Francis wa Asisi alifnaya uzoefu wa kuona vita na kupitisha mipaka ya vita hadi  kushinda mantiki ya migogoro ya kizalendo na kufuata maelekezo matakatifu ambayo yalimpelekea kuamini kuwezekano wa kukutana kidugu na kila kiumbe. Huo ni ujumbe ambao unafaa hata leo hii, kwa sababu majadiliano maana yake ni kwenda kukutana na mwongine bila hukumu, kwa amani ndani ya moyo, kwa utambuzu wa kukutana hawali ya yote na mtu mbali na imani yake. Mwenye ndoto Mtakatifu Francis wa Assisi, anasema Padre Pattoni,kuwa  alionesha maana kubwa ya matendo ya dhati ya kwenda kukutana na Sultani na ndiyo matokeo hayo ya kuadhimisha miaka 800 iliyopita ambayo kama wafransiskani bado wapo katika nchi Takatifu wakiwa na ari ya kuendelea katika nyayo zake alizozipitia.

Hata hivyo ikimbukwe kwamba, Kardinali Leonardo Sandri, Rais wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya Mashariki anatarajia kuhutubia katika mkutano wa tarehe 3 Oktoba hasa kuzungumzia mada juu ya  Mkutano kati ya Mtakatifu Francis wa Asisi  na Sultani:katika mafundisho na ishara za Baba Mtakatifu Francisko, kwenye  Msikiti wa Al-Aqsa. Katika siku hiyo pia inatarajiwa mkutano muhimu kwenye msikiti huo na Mufti Mkuu wa Yerusalemu. Aidha Kardinali  Sandri ndiye atakayeongoza Misa kuu katika hafla ya sikukuu ya Mtakatifu Francis wa Assisi  Ijumaa tarehe 4 Oktoba 2019 katika Kanisa la Mtakatifu Salvatore nchi Takatifu.

01 October 2019, 14:29