Tafuta

Vatican News
Sr. Daniela ambaye ni katibu Mkuu wa Shirikisho la Baraza la Watawa wa Amerika ya Kusini(Clar)ameshiriki kama msikilizaji kwenye Sinodi ya Maaskofu kuhusu Amazonia tarehe 6-27 Oktoba 2019 Sr. Daniela ambaye ni katibu Mkuu wa Shirikisho la Baraza la Watawa wa Amerika ya Kusini(Clar)ameshiriki kama msikilizaji kwenye Sinodi ya Maaskofu kuhusu Amazonia tarehe 6-27 Oktoba 2019 

Amerika Kusini:watawa wanabeba uchungu na matumaini ya watu wanaoteseka!

Shirikisho la Baraza la Watawa wa Amerika ya Kusini (CLAR) wameandika ujumbe wao wa wakionesha utashi wa kubeba uchungu na matumaini ya watu wanaoteseka katika nchi kadhaa barani mwao,huku wakitoa mwaliko wa kutafakari,wa mshikamano na sala kwa ajili ya kile kinachotokea katika nchi hizi.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Shirikisho la Baraza la Watawa wa Amerika ya Kusini(CLAR)wameandika barua yao ikisema kuwa: “kutoka Assisi pamoja na Mtakatifu wa Amani, tunaweka mbele ya Mungu wa maisha, matumaini na uchungu wa ndugu wa watu wengi wa bara  ketu pendwa la Amerika ya Kusini na visiwa vya Carribien ambao wanakabiliwa na athari za kukandamizwa na vurugu kuzidi kiasi katika wiki za hivi karibuni dhidi ya mapambano ya haki na usawa wa haki kijamii”.  Kwa mujibu wa Shirika la Habari za Kimisionari Fides, wamepokea ujumbe wa Shirikisho la Baraza la Watawa wa Amerika ya Kusini (CLAR) huku wakitoa mwaliko wa kutafakari, wa mshikamano  na sala kwa ajili ya kile kinachotokea katika nchi hizi. Watawa hawa katika waraka wao, wanaeleza hali nyingi na tofauti katika Bara la Amerika ya Kusini, mahali ambamo watu wanaishi kwa mivutano au ghasia zinazosababisha mapigano ya waandamanaji na nguvu za vikosi vya mamlaka.

Vurugu nchini Chile, Bolivia, Equador, Haiti, Nikaragua

Wakiorodhesha matukio hayo kwa mtazamo wa nchi za Amerika ya Kusini zilizopo kwenye mgogoro kwa mfano nchini Chile wanaonesha kuwa, watu wamesema sasa inatosha kupandisha gharama za maisha na sintofahamu za wanasiasa, lakini ni mahali ambapo ghasia za kutumia nguvu zinaendelea bila kikomo na kuharibu hata ile imani dogo ambayo ilikuwa inatunza utulivu wa watu. Na kwa upende wa nchi ya Bolivia, watu bado wanaonekana kutetea demokrasia iliyozuiwa na mashaka makubwa katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni. Na  Haiti  Kanisa linaomba utulivu na amani mbele ya ghasia zilizosababishwa na ufisadi wa kukithiri kwa ngazi nyingi na ambazo zimesababisha majanga makubwa ya umasikini kwa watu wadhaifu wanaoteseka. Tukienda katika nchi ya Nicaragua, nayo  bado wanaonesha jinsi gani mfumo wa serikali inavyozuia ule uhuru wa kujieleza,  hadi kufikia  hata uhuru wa kidini, na hivyo demokrasia  inakuwa suala nyeti ka  ni mhusika mkuu halisi ya kutatua. Na kwa upande wa nchi ya Equador, pia  zoezi la mchakato wa  upatanisho la Maaskofu limeweza angalau kusitisha vurugu za maandamano hayo na ili kufanya majadiliano na vikundi vya kijamii.

Watu wana kiu ya amani na haki kijamii

Mbele ya mantukio hayo Shirikisho la Baraza la Watawa wa Amerika ya Kusini (CLAR), wanaandika kuwa: “watu wetu wanayo kiu ya amani na haki na tunataka kukishuhudia. Na kwa maana hiyo karibu na Mtakatifu ndugu wa Assisi, tunaomba kwa ajili ya amani, kwa maana ni zawadi ya Mungu na kila mmoja wetu lazima aipokee na kuijenga kila siku kwa msaada wake”. Kadhalika wanaongeza kuandika kuwa, “kama watu wa maisha ya kitawa, hatutachoka kutafuta na kuhamasisha michakato ya hatua ya mshikamano na hali, tukitazama  kutoa huduma mbali zaidi na matakwa binafsi. Hata katikati ya mateso mengi, tunaendelea kuwa wachukuzi wa ‘divai mpya’ inayopasua viliba vyetu na kuwafikia wote. Kilio cha masikini cha kutaka amani, kisibaki bila jibu na vijana kuwa na matumaini mema”. Katika hitimisho la barua hiyo imetiwa sahihi na Sr. Gloria Liliana Franco Echeverri, ODN Rais wa CLAR na  Katibu wake mkuu Sr. Daniela A. Cannavina, HCMR.

Sr. Daniela A. Cannavina ni mmoja wa wasikilizaji wa Sinodi ya Maaskofu

Hata hivyo Sr. Daniela A. Canannavina, ni mmoja wa washiriki wa kusikiliza kwenye Sinodi ya Maaskofu kuhusu Amazonia na ambaye tarehe 18 Oktoba wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya mwendelezo wa Sinodi kwa waandishi wa habari, alisisitiza juu ya wito wa kufikiria Amazonia  hasa katika kufanya mazoezi ya dhati ya kushinda hofu; alizungumzia juu ya wanawake kupewa nafasi ya kutoa mchango wao katika Sinodi na pia kugusia juu ya   maisha ya kitawa ambayo alieleza njia mwafaka wa kueledelea kuhamasisha maisha yanayo jikita katika msingi wa  Injili. https://www.vaticannews.va/sw/vatican-city/news/2019-10/sinodi-ya-maaskofu-amazonia-2019-fisichella-ripoti.html

26 October 2019, 13:20