Tafuta

Vatican News
Pamoja na umasikini Kisiwani Madagascar, bado Kanisa linajitahidi kwa ngazi ya kijamii Pamoja na umasikini Kisiwani Madagascar, bado Kanisa linajitahidi kwa ngazi ya kijamii 

MADAGASCAR:bado kuna changamoto ya afya na magonjwa kama Ukoma!

Uwepo wa mashirika ya kitume kisiwani Magascar na Kanisa ni moja ya msaada mkubwa wa kijamii,kwa mujibu wa Sr.Maria Jardiolyn katika mahojiano na mwakilishi wetu wa Vatican News kisiwani Madagascar katika fursa ya hija ya kitume ya Baba Mtakatifu Francisko.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican News

Baba Mtakatifu anafanya hija ya kitume kuanzia tarehe 6-8 Septemba 2019 katika nchi ambayo ni dhaifu kwa upande wa Afya. Na hii ni kutokana na kwamba Madagascar haijafunikwa yote yote kuhusu ugonjwa wa ukoma na idadi kubwa ya magonjwa yatokanayo na wadudu na kusababisha hali halisi mbaya kwa upande wa afya.  Hata hivyo uwepo wa mashirika ya kitume katika mantiki ya Afya ni kubwa sana ambayo kwa taratibu katika karne hizi imekuwa rasilimali msingi kwenye huduma ya fya kwenye hospitali za umma au zinazoendeshwa na mashirika ya kitawa mahali ambapo wagonjwa wanapata huduma inayostahili. Moja ya whudumu wa afya katika vituo vya afya vya serikali na Kanisa ni wanashirika wanaojihusisha na hospitali liitwali Shirika la Watawa wa Uhuruma.  Na mmoja wa wawakilishi wa Vatican News, Antonella Palermo, katika fursa ya Ziara ya Baba Mtakatifu Francisko huko Madagascar, wameweza kukutana na kuhojana na Sr. Maria Jardiolyn, mwenye asili ya kifilippini ambaye amesisitizia juu ya umakini wao kwa ajili ya watu ambao hawana nyenzo muhimu hasa kiuwezo wa kuweza kupata matibabu bora katika hospitali za umma.

Sr. Maria Jardiolyn anasema, katika mji wa Antannarivo, watawa wao wanatoa huduma moja ya hospitali kubwa zaidi. Ni hospitali ya serikali, lakini kwa bahati mbaya huduma za Afya kisiwani Madagascar kwa ujumla, inatisha hasa hasa kwa upande watu masikini. Nafasi yao kama watawa ni ile ya kuweza kurahisisha huduma, na kutibu wagonjwa. Na zaidi wao wanaendeesha pia hospitali za Shirika, hata hospitali nyingine ya jimbo. Ni miaka sasa kumi hivi ambapo wanafika hata madaktari bingwa kuweza kuhudumia na wao wanatangaza kwa njia ya radio uwezekano wa madakatiri hao kufika ili watu waweze kufika kwa ajili ya kutibiwa. Baadhi ya sehemu huko Madagascar anathibitisha, ni lazima kuwafundisha watu kwamba wanapoumwa, lazima waende hospitalini. Na wengi wanapokuja, wanakuwa tayari wako hali mbaya sana, kwa maana hawaamini kwamba, hospitali inaweza kuwasaidia kupona. Kutokana na hiyo zaidi ya kuwatibu Sr Maria anasema, kazi yao ni kutafuta kufanya kazi kama utume wa kuwaalika hata watoto, au wanawake wajawazito, ambao mara nyingi wanafika wakati hakuna tena jambo lolote la kufanya zaidi ya kifo. Kwa bahati mbaya watu hao bado wanakwenda kukimbilia katika mtu mkubwa kwa sababu wanaamini bado katika miti hiyo mikubwa uwezekano wa kupona.

Katika kusisitizia juu ya waganga wa kinyeji, Sr. Maria anathibitishwa kwamba bado kuna kuamini sana ushirikina na waganga wa kienyeji, kwa maana hiyo wanafanya kazi hata kwa hakika ya kuhamasisha. Na kwa kuwa watu hawaji hospitalini, wakati mwingine, watawa wanakwenda katika misitu wanakokaa watu wenyewe. Wanajaribu kuwahamasishsa watoke katika misitu hiyo ili waweze kukaa katika vijiji kwa pamoja, lakini anangeza kwamba hiyo ni jukumu pia la serikali linalopaswa kutoa msukumo na kufanya kampeni za kukuza na hasa kwenda katika maeneo yaliyo mbali kwa watu hao. Katika vituo na katika miji kuna umaskini, lakini zaidi hata sehemu za pembezoni, kuna unyonyaji, ambalo ni moja ya sababu kuu, na mara nyingi ya kuwafanya watu wasije katika hospitali.  Kwa upande wao, wanatia moyo daima, na wakati mwingine wanakwenda kukutana nao katika njia. Hatimaye Sr. Maria akielezea hali halisi ya watu wa madagascar na matarajio ya kumpokea Baba Mtakatifu Francisko, kwa hakika ni shauku kubwa na maandalizi ambayo yamefanywa kwa ngazi ya kidini, lakini pia hata wale wasio na dini. Ni matarajio ya Sr. Maria kuwa ziara ya Baba Mtakatifu ni ile ya kukuza na kuongeza matumaini kwa watu wote.

Maratajio ya Askofu Askofu Rosario Vella Msalesiano wa Jimbo la Moramanga kuhusu ziara hii ya Papa: Aidha ziara ya Baba Mtakatifu Francisko kisiwa kikubwa cha Madagascar ni shauku kubwa ya watu hasa wakatoliki wanaowakilisha asilimia 35% lakini pia kuna madhehebu mengine ya imani za kidini. Katika mahojiano mengine na Askofu Rosario Vella Msalesiano wa Jimbo la Moramanga Kaskazini mwa kisiwa anaelezea matumaini yake kuhusu ziara hii ya Papa. Kila sehemu ni furaha kubwa na shauku. Watu wengi wanajiandaa kukutana na tukio hili la neema kwa sababu katika tabia za Madagascar, baraka inayotoka kwa yule anayewasiliana kwa namna ya pekee na Bwana, Mungu na Muumba na hata labda anamtambua  kwa mtindo mwingine, ni jambo la pekee. Kwa maana hiyo watu wanasubiri muda huo! Katika kusubiri ujio huo wameanzisha mambo mengi wa mfano, katika jimbo lake japokuwa na umasikini na umbali uliopo, watu elfu tatu watakwenda Antananarivo kuudhuria mkesha na Misa Takatifu ya Baba Mtakatifu Francisko Jumapili tarehe 8 Septemba 2019 katika uwanja mkubwa wa jimbo Soamandrakizay.

Kadhalika Askofu akifafanua juu ya matumaini yake na kile ambacho wanasubiri kwa Baba Mtakatifu Francisko ni kwamba wanafikiri kuwa ziara ya Papa italeta amani, ambayo si kusema kutokuwa na migogoro, lakini zaidi matarajio ya haki na amani ya ndani, amani kwa wale ambao wanaishi nao karibu, amani ili kuanza kwa upya ule uhusiano na Mungu. Kadhalika anaeleza matumaini, kwa sababu katika kipindi hiki ambacho wanaishi hali ngumu, hasa umasikini unaozidi kuongezeka zaidi. Uwiano mkubwa uliopo kati ya matajiri na masikini, kwa sababu wapo matajiri ambao kwa hakika wanawanyonya na kuwatesa kidogo watu na hivyo umasikini ni mpana sana katika kisiwa cha madagascar. Hali nyingine ambayo anasema   kwa bahati mbaya inazidi kuongezeka ni kuhusu husu ufisadi ambao anasema ni saratani ya kweli kwa ngazi zote. Hali hii anathiibtisha kwa bahati mbaya hata yule anayetaka kuwa haki awezi kupata kutokana na wengine kulipwa.

06 September 2019, 15:51