Tafuta

Vatican News
Akamasoa mji wa urafiki umekuwa ni chemchemi ya matumaini ya watu waliokuwa wanaogelea katika dimbwi la umaskini wa ukutupwa! Akamasoa mji wa urafiki umekuwa ni chemchemi ya matumaini ya watu waliokuwa wanaogelea katika dimbwi la umaskini wa ukutupwa! 

Hija ya Papa Francisko nchini Madagascar: Akamasoa Mji wa Urafiki: Ukombozi wa maskini

Umaskini uliokuwa umekithiri sasa umekomeshwa, imani imepamba moto, heshima ikitamalaki na watu wakifanya kazi kama kawaida. Kwa unyenyekevu wote maskini sasa wameinuka na kusambaa katika mitaa wakitangaza uhuru na haki kwa wote. Ni ushuhuda ulionukuruwa na kuanza katika viunga vya Akamasoa ambapo umaskini ulikuwa umekithiri kiasi cha kutisha!

Na Padre Angelo Shikombe, - Vatican.

Ziara ya Baba Mtakatifu Francisko imetiririsha furaha zisizo na kifani katika Domenika, na maadhimisho ya Sherehe za kuzaliwa Bikira Maria yaliyofanyika  tarehe 8 Septemba 2019 huko nchini Madagascar. Wakati huo Injili ikipamba moto na kuangazia maelfu ya familia maskini na watoto waliosetwa na kutupwa pembezoni mwa jamii. Mahali ambapo palihesabika kuwa pametengwa na jamii, penye machafuko na vifo vya watu wengi, kutokana na ziara ya Baba Mtakatifu pamegeuzwa kuwa mahali penye matumaini, upendo na furaha. Taarifa zaidi zinabainisha Padre Pedro OPEKA akisema, Baada ya miaka 30 ya kutegemea uweza wa Mungu, Mwenyezi Mungu amechimba kisima cha matumaini mapya kwa jamii ya watu wa madagascar.

Mwenyezi Mungu kwa tukio la hija ya kitume ya Baba Mtakatifu, amerudisha tena heshima ya watoto, na vijana wanaokwenda shule na wazazi wanaowajibika kuandaa maisha ya watoto wao. Umaskini uliokuwa umekithiri sasa umekomeshwa, imani imepamba moto, heshima ikitamalaki na watu wakifanya kazi kama kawaida.  Kwa unyenyekevu wote maskini sasa wameinuka na kusambaa katika mitaa wakitangaza uhuru  na haki kwa wote. Ni ushuhuda ulionukuruwa na kuanza katika viunga  vya Akamasoa  ambapo umaskini ulikuwa umekithiri kwa kushindwa kujaliana na hasa kuzorota kwa viongozi wa kisiasa waliosahau Msalaba wao ulioko mabegani mwao juu ya wanacnhi waliowachagua na matokeo yake wakaendelea kujibovusha katika starehe. Jumuiya hii inaundwa na vikundi kutoka mataifa mbalimbali wanaofika kushiriki Ekaristi Takatifu kila Dominika.

Aidha, Padre Pedro OPEKA, ameendelea kusema, tumaini alilowaachia Baba Mtakatifu, ni pamoja na  kupabadili mahali ambapo palikuwa na vurugu na ghasia za kila aina na kupafanya mahali pa ujirani mwema na  mahali pa kushirikishana upendo wa Mungu. Hivyo wanamadagascar wanamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa ujio wa Papa katika Nchi yao. Hivyo wanamadagascar wanaendelea kuomba neema na baraka za Mwenyezi Mungu ili vijana walioipokea Injili wasikengeuke tena na kurudia maisha ya zamani. Wanaomba haki idumu mioyoni mwa wote na hasa kwa waliowanyonge na kwenye jamii ya watoto, akina mama na watu waliotengwa na jamii ili wapewe ulinzi na misaada wanayohitaji. Wanamadagascar wamemshukuru sana Baba Mtakatifu kwa ziara yake ya kitume  na moyo wake wa kibaba wa kuwapenda maskini. Hii inaleta furaha ya kweli ya Injili ya Kristo aliyohubiriwa tangu enzi za Mitume na inayomkomboa mwanadamu kutoka utumwa wa dhambi.  Hivyo, hisisa za furaha ya watoto na vijana inaeleza mbegu ya amani aliyoipanda Baba Mtakatifu nchini Madagascar.

 

 

09 September 2019, 16:38