Tafuta

Ripoti ya ya kitaifa ya Caritas nchini Peru inathibitisha kusaidia familia zenye matatizo 198,000 kwa mwaka 2018.Hii ni shukrani kutokana na msaada wa taasisi tofauti,masharika yasiyo ya kiserikali na wafadhili Ripoti ya ya kitaifa ya Caritas nchini Peru inathibitisha kusaidia familia zenye matatizo 198,000 kwa mwaka 2018.Hii ni shukrani kutokana na msaada wa taasisi tofauti,masharika yasiyo ya kiserikali na wafadhili 

PERU:Zaidi ya familia 198,000 wamepokea msaada wa Caritas mwaka 2018!

Ripoti ya Kijamii ya Caritas nchini Peru ambayo inafafanua shughuli za mipango na taratibu katoliki kwa mwaka 2018 inathibtisha,Kanisa Katoliki nchini Peru imesaidia zaidi ya familia 189,000 nchini humo.Familia hizi zimehusisha katika mipango tofauti ya Caritas kwa kupanuliwa kwa mwaka.Mipango tofauti ni 45 ambayo baadhi yao imeweza kutekelezwa kwa ushirikiano na taasisi nyingine 35,mashirika yasiyo ya kiserikali na wafadhili.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kanisa Katoliki nchini Peru imesaidia zaidi ya familia 189,000 katika nchi kwa mwaka 2018 kufuatia na Ripoti ya Kijamii ya Caritas nchini Peru ambayo inafafanua shughuli za mipango na taratibu katoliki kwa mwaka 2018. Mkurugenzi wa Caritas kitaifa nchini Peru Carla Auza anaendelezea jinsi gani familia hizi zimepokea msaada na kwamba, “ familia hizi zimehusisha katika mipango tofauti ya Caritas ambayo imepanuliwa kwa mwaka 2018. Mipango hii tofauti ni 45, ambayo baadhi yao imeweza kutekelezwa kwa ushirikiano na taasisi nyingine 35, mashirika yasiyo ya kiserikali na wafadhili.

Kwa njia ya mipango, imewezesha familia 36,000 wenye kuhitaji

Bi Carla Auza akiendelea na ufafanuzi wa mipango ya Caritas kitafia amesema, kwa njia ya mipango hiyo imewezesha kufikia familia 36,000 zenye kuhitaji msaada; aidha kuna program za misaada ya kijamii ambayo imewezesha kuwasaidia zaidi ya familia 164,000 na watu ambao walikuwa na dharura. Wengi wao  ni wazalendo ambao wamepokea hata matibabu au zana mbalimbali au vifaa vya lazima vya  afya kama vile viti vya walemavu na wazee, magongo ya kutembelea kwa walemavu na mengine.

Taasisi tofauti,mashirika yasiyo ya kiserikali na wafadhili

Ripoti ya Caritas kitaifa pia imesema, inahamasisha hata mipango mingine yenye tabia ya mafunzo au sekta ya afya au kwa ajili ya lishe, katika hali ya kipeo cha mazingira. Kwa mfano kwa mwaka 2018 wametoa msaada wa dharura kwa familia 2,500 wakati wa kipindi cha baridi kali iliyoikumba  milima ya Peru (Ande za Peru). Jumuiya ndogo inayoishi katika milima hiyo ilipokea msaada ili kukukuza uzalishaji wa kilimo na mazao na wanyama waweze kuishi au kuongeza uchumi wao katika eneo lao.

22 August 2019, 14:44