Tafuta

Vatican News
Parokia ya Mtakatifu Maria Consolata huko Casal Bertone Roma ndipo Papa ataadhimisha Misa ya Sikukuu ya Mwili na Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Jumapili 23 Juni 2019 Parokia ya Mtakatifu Maria Consolata huko Casal Bertone Roma ndipo Papa ataadhimisha Misa ya Sikukuu ya Mwili na Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Jumapili 23 Juni 2019 

Sikukuu ya Mwili na Damu ya Yesu:Papa katika mtaa wa Casal Bertone

Baba Mtakatifu Francisko anatarajia kuadhimisha misa Takatifu ya Sikukuu ya Mwili na Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Jumapili 23 Juni 2019 katika Uwanja wa Parokia ya Mkatifu Maria Consolata saa 12.00 jioni masaa ya Ulaya.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Jumapili 23 Juni 2019 Baba Mtakatifu Francisko anatarajia kuadhimisha misa Takatifu ya Sikukuu ya Mwili na Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo katika Uwanja wa Parokia ya Mkatifu Maria Consolata saa 12 .00 jioni masaa ya Ulaya. Baada ya misa Takatifu yatafuata maandamano ya Ekaristi ya Mwili wa Yesu katika barabara za mitaa hiyo kwa kuongozwa na Kardinali Angelo De Donatis Makamu wa Papa wa Jimbo Roma.  Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Mawasiliano ya jimbo Kuu, inasema waamini kwa pamoja wataandamana  na Ekaristi ya mwili wa Yesu katika njia za mitaa ya Casal Bertone, Portonaccio na  Latino Silvio, na kuhitimishwa katika uwanja wa mpira karibu na nyumba ya Serena, jengo linalo wakaribisha watu wasio kuwa na makazi na ambamo wanahudumiwa na wamisionari wa Upendo  wa Mama Teresa wa Calcutta. Ni mwendo wa Kilometa moja na mita miambili.

Nyimbo zitaimbwa na kwaya mbili za parokia

Misa itaongozwa na kwaya mbili zilizoungana za Parokia ya Maria Consolata; hata huduma za kiliturujia zitaongozwa na wahudumu wa Parokia. Hata hivyo katika liturujia ya Jumapili tarehe 23 wanatahusishwa maparokia mengine saba ambayo yako katika tarafa ya XIV mjini Roma, kama vile parokia ya: Mtakatifu Barnaba, Mtakatifu Elena, Mtakatifu  Giulia Billiart, Mtakatifu  Yosefu Cafasso, Mtakatifu  Leone I, Mtakatifu Luca Evangelista, Watakatifu  Marcellino na  Pietro wa duas Lauros. Naombi ya waamini yatasomwa na wahudumu wa kutoa kumunio  katika jumuiya zao zote nane na watatoa Komunia katika maeneo yote yaliyo andaliwa kwenye uwanja huo karibu na Kanisa la Maria Consolata. Kutakuwa na nafasi kwa ajili ya watoto ambao mwaka huu wamepokea komunio ya kwanza na wazazi wao. Aidha katika uwanja watakaa zaidi ya watu 500 wanaolala katika nyumba ya Serena, vile vile sehemu nyingine kwa ajili ya wazee, wagonjwa na wahudumu wa vijana na watoto wakati wa shughuli za kiangazi.

Ikumbukwe mwaka jana alikuwa eneo la Ostia Roma

Ikumbukwe mwaka jana Baba Mtakatifu aliadhimisha Sikukuu ya mwili na damu ya Yesu katika eneo la Ostia. Kwa mwaka huu pia amechagua eneo la pembeni mwa mji ni katika kuonesha jinsi gani ya ushiriki wa Misa hiyo kama muungano na Mungu kati yetu kwa mujibu wa Padre Giuseppe Midili, Mkurugenzi  wa ofisi ya Liturujia kijimbo. Katika maadhimisho yao yatakuwa ndiyo ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 75 tangu kutabarukiwa Parokia. Na Papa Francisko atakuwa nne kutembelea Parokia hii ya Consolata. Kwa mara ya kwanza alikuwa ni Papa Paulo VI, Papa Yohane Paulo II, Papa Benedikto XVI na ambaye kama kardinali ilikuwa ni Parokia yake. Ni maandalizi makubwa sana wanayo msumbiri watoto, wazazi na waamini wote kwa ujumla. Na ili kufanikisha sikukuu na ziara hiyo, tarehe 20 Juni 2019 wameandaa siku nzima ya kuabudu Ekaristi ambapo Kanisa litabaki limefunguliwa kuanzia saa 1,30 asubuhi hadi saa 6 usiku wa manene!

18 June 2019, 15:46