Tafuta

Vatican News
Askofu mkuu Ioan Robu wa Jimbo Kuu la Bucharest anawataka waamini kuimarisha imani inayokita mizizi yake katika mapendo yanayopyaisha cheche za matumaini! Askofu mkuu Ioan Robu wa Jimbo Kuu la Bucharest anawataka waamini kuimarisha imani inayokita mizizi yake katika mapendo yanayopyaisha cheche za matumaini!  (Vatican Media)

Hija ya Kitume Romania: Imani, Mapendo na Matumaini

Familia ya Mungu Jimbo kuu la Romania inamwomba Baba Mtakatifu Francisko awabariki waamini, apende kuibariki Romania na kwa njia ya uwepo wake, asaidie kuimarisha imani inayokita mizizi yake katika mapendo yanayopyaishwa kwa cheche za matumaini, ili wote waweze kutembea katika njia ya historia, kwa kutafuta mafao ya wengi, udugu, amani na maridhiano kati ya watu!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Askofu mkuu Ioan Robu wa Jimbo kuu la Bucharest nchini Romania katika salam zake kwa Baba Mtakatifu Francisko, Ijumaa, tarehe 31 Mei 2019 baada ya Ibada ya Misa Takatifu, Siku kuu ya Bikira Maria kumtembelea binamu yake Elizabeti, amemshukuru na kumpongeza na kwamba, wamesikiliza kwa makini mahubiri yake! Wamesali kwa moyo wao wote na kwamba, amekuwa ni chemchemi ya furaha kwa waamini na watu wote wenye mapenzi mema nchini Romania! Familia ya Mungu Jimbo kuu la Bucharest inasema, itaendelea kumkumbuka na kumwombea Baba Mtakatifu Francisko katika maisha na utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro!

Kwa upande wake, Baba Mtakatifu aendelee pia kuwakumbuka na kuliombea Kanisa mahalia pamoja na nchi ya Romania katika ujumla wake. Familia ya Mungu Jimbo kuu la Bucharest inamwomba Baba Mtakatifu Francisko awabariki waamini, apende kuibariki Romania na kwa njia ya uwepo wake, asaidie kuimarisha imani inayokita mizizi yake katika mapendo yanayopyaishwa kwa cheche za matumaini, ili wote waweze kutembea katika njia ya historia, kwa kutafuta mafao ya wengi, udugu, amani na maridhiano kati ya watu!

Askofu Mkuu Robu
01 June 2019, 11:47