Tafuta

Vatican News
Jimbo kuu la Westeminster, Uingereza limesikitishwa na uamuzi wa Mahakama kumlazimisha mwanamke mjauzito kutoa mimba kutokana na ulemavu alionao mtoto wake! Jimbo kuu la Westeminster, Uingereza limesikitishwa na uamuzi wa Mahakama kumlazimisha mwanamke mjauzito kutoa mimba kutokana na ulemavu alionao mtoto wake!  (Vatican Media)

Mama mjamzito mwenye mtoto mlemavu alazimishwa kutoa mimba kisheria!

Askofu msaidizi John Sherrington wa Jimbo kuu la Westminster nchini Uingereza, amesikitishwa na hukumu iliyotolewa hivi karibuni na Mahakama nchini humo, kwa kumwamuru Mama mwenye umri wa miaka 20 kutoa mimba ya mtoto wake ambaye anaonekana kuwa na ulemavu. Mama huyu alitamani kumzaa, kumtunza na kumlea mtoto wake hata kama alikuwa na ulemavu!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko anasema, maisha ni zawadi kubwa kutoka kwa Mungu. Kama waamini wanahamasishwa: kuilinda na kuidumisha, tangu pale mtoto anapotungwa mimba tumboni mwa mama yake, hadi mauti yanapomfika kadiri ya mpango wa Mungu, hata pale watu wanapokumbana na magonjwa na mahangaiko mbali mbali ya maisha. Hakuna mwenye haki ya “kunyofolea mbali zawadi ya maisha ya binadamu”.Askofu msaidizi John Sherrington wa Jimbo kuu la Westminster nchini Uingereza, amesikitishwa na hukumu iliyotolewa hivi karibuni na Mahakama nchini humo, kwa kumwamuru Mama mwenye umri wa miaka 20 kutoa mimba ya mtoto wake ambaye anaonekana kuwa na ulemavu.

Mama huyu alitamani kumzaa, kumtunza na kumlea mtoto wake hata kama alikuwa na ulemavu, kwani kwake, ilikuwa ni zawadi kubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, lakini Mahakama imemwamuru atoe mimba. Askofu msaidizi John Sherrington anasema, huu ni uvunjwaji wa haki msingi za binadamu na haki ya mtoto kuzaliwa katika familia ambayo iko tayari kulinda, kuendeleza na kudumisha Injili ya familia. Hali hii inaonesha upinzani mkubwa kati ya haki msingi za mtu binafsi na nguvu ya Sheria za nchi. Uamuzi huu wa Mahakama anasema Askofu Msaidizi Sherrington unasikitisha sana na Kanisa litaendelea kumkumbuka na kumwombea katika kipindi hiki anacholazimishwa kufanya maamuzi machungu katika maisha!

Injili ya uhai

 

25 June 2019, 10:28