Tafuta

Nchini Afrika Kusini inasifika kwa utoaji mkubwa wa madini ya makaa ya mawe lakini ambayo yamesababisha vifo vingi kutokana na magonjwa ya mapafu Nchini Afrika Kusini inasifika kwa utoaji mkubwa wa madini ya makaa ya mawe lakini ambayo yamesababisha vifo vingi kutokana na magonjwa ya mapafu 

AFRICA KUSINI:Tume ya haki na amani kutoa sauti kwa niaba ya wachimba makaa ya mawe!

Tume ya Haki na Amani ya Afrika ya Kisini ya (Sacbc)imeandaa maonyesho ili kusaidia wachimba madini ambao walitoa madai yao katika kampuni ya madini “Sasol Coal” ya Makaa ya Mawe kutokana na kupata magonjwa makubwa ya mapafu na magonjwa mengine yatokanayo na kuvuta pumzi ya makaa ya mawe, kwa miaka mingi katika migodi ya kijamii.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tume ya Haki na Amani ya Baraza la Maaskofu wa Afrika ya Kusini SACBC), wakati wa kuwakilisha maonesho juu ya hali halisi ya machimbo ya makaa nchini Afrika Kusini wamesema “mara nyingi tunajidai kuwa na taifa lenye kuwa na umeme wa soko zuri, lenye msingi wa makaa, lakini bado haioneshi gharama ya kibadamu”.Tume ya Haki na Amani imeandaa maonyesho ili kusaidia wachimba madini ambao walitoa madai yao katika kampuni ya madini “Sasol Coal” ya Makaa ya Mawe kutokana na kupata magonjwa makubwa ya mapafu na magonjwa mengine yanayotokana na  kuvuta pumzi ya makaa ya mawe, kwa miaka mingi katika migodi ya kijamii. Na hii ni kweli kwamba nchini Afrika Kusini inasifika kwa utoaji mkubwa wa madini ya makaa ya mawe barani Afrika na kwingineko duniani.

Kupambania haki

Mpango wa Tume ya “haki na amani” unataka kuonekasha wazi na kutoa sauti kwa niaba ya  “maelfu ya wachimbaji wa zamani ambao wameugua magonjwa baada ya kufanya kazi kwa miaka mingi ili kuondokana na uchambaji wa makaa ambayo kwa kiasi kikubwa cha uzalishaji wa umeme nchini Afrika Kusini kinategemea”. Kwa njia  hiyo maonyesho hayo yanajaribu kutoa sauti ya  wachimbaji wagonjwa na kutoa mwanga juu ya mapambano yao kwa ajili ya haki.

Wajibu wa makampuni ya madini

Katika maandishi ya Tume ya Haki na Amani katika tovuti ya Sacb ambayo wanawaalika“kurekebisha uharibifu unaosababishwa na sekta ya kiwanda cha  makaa ya mawe ya Afrika Kusini. Makampuni ya madini lazima yachukua wajibu wake  hasa kwa kulipa fidia kwa wachimbaji wa zamani wanaosumbuliwa na ugonjwa wa mapafu meusi, au makaa ya mawe ya “pneumoconiosis”.

Hatua zilizofanyika

Ikumbukwe kwamba Maaskofu wa Afrika Kusini, kwa njia ya Tume ya Haki na Amani, kwa muda mrefu wameunga mkono hatua za matendo iliyoanzishwa na mamia elfu ya wachimbaji ambao wameambukizwa na ugonjwa huo na kwa familia ya wafanyakazi, ambao wamekufa kutokana na ugonjwa wa mapafu “pneumoconiosis”. Kwa mujibu wa “Utandawazi na Afya”, Globalization and Health”, kwamba tangu kuanza kwa mchakato wa kuomba fidia kwa ajili ya uharibifu wa wachimbaji, mwishoni mwa 2017, wachimbaji 111,166 wameweza kupokea fidia, ambayo watu  55, 864 wanashindwa  kupumua  na hivyo kuwa wagonjwawa kudumu na wengine 52,473 kwa kifua kikuu.  Hata hivyo, madai mengine ya watu 107,714 hayajalipwa. Maombi mengine mengi asilimia (28.4%) yanatoka Msumbiji, Lesotho, Swaziland, Botswana na nchi nyingine za Kusini mwa Afrika.

05 June 2019, 13:11