Tafuta

Vatican News
Patriaki Daniel wa Kanisa la Kiorthodox nchini Romania amemshukuru Papa Francisko kwa mshikamano wa upendo katika ujenzi wa Kanisa kuu la Wokovu wa Watu wote! Patriaki Daniel wa Kanisa la Kiorthodox nchini Romania amemshukuru Papa Francisko kwa mshikamano wa upendo katika ujenzi wa Kanisa kuu la Wokovu wa Watu wote!  (AFP or licensors)

Hija ya Kitume Romania: Hotuba ya Patriaki Daniel: Mshikamano!

Kanisa kuu ni kwa ajili ya Wokovu wa watu wote. Hii ni bustani ya Bikira Maria, Mama wa Mungu, mlinzi na msimamizi wa Romania. Ni katika Kanisa hili, familia ya Mungu inakutana ili kuadhimisha Sherehe ya Kupaa Bwana Mbinguni pamoja na kuwakumbuka mashujaa wa Romania. Hili ni Kanisa lilowekwa wakfu kwa ulinzi na tunza ya Mtume Andrea, aliyejisadaka kutangaza Injili ya Kristo!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Patriaki Daniel wa Kanisa la Kiorthodox la Romania, Ijumaa, tarehe 31 Mei 2019 amemwelezea Baba Mtakatifu Francisko kwamba, hili ni Kanisa kuu kwa ajili ya Wokovu wa watu wote. Hii ni bustani ya Bikira Maria, Mama wa Mungu, mlinzi na msimamizi wa Romania. Ni katika Kanisa hili, familia ya Mungu nchini Romania inakutana ili kuadhimisha Sherehe ya Kupaa Bwana Mbinguni pamoja na kuwakumbuka mashujaa wa Romania. Hili ni Kanisa lilowekwa wakfu kwa ulinzi na tunza ya Mtume Andrea, aliyejisadaka kutangaza na kushuhudia Habari Njema nchini Romania kadiri ya Mapokeo.

Kanisa hili ni nyumba ya watu wa Mungu nchini Romania, ushuhuda wa Fumbo la Ufufuko, uhuru wa kidini pamoja na uhuru wa kuabudu baada ya Romania kuwa chini ya mfumo wa Kikomunisti kwa takribani miaka 50. Kunako mwaka 1999 na Mwaka 2002 Mtakatifu Yohane Paulo II amechangia kiasi cha dola za kimarekani 200, 000 kwa ajili ya ujenzi wa Kanisa kuu. Kiasi cha dola za kimarekani 500, 000 zimetumika kununulia kengele ya Kanisani ambayo kadiri ya Mapokeo ya Kanisa ni sauti ya Mungu inayowaalika watu kusali, kushirikiana na kushikamana kama ndugu wamoja. Kanisa la Kiorthodox linawapongeza viongozi wa Kanisa Katoliki nchini Italia kwa kutoa nafasi kwa waamini wa Kanisa la Kiorthodox kuweza kusali. Kuna nyumba za Ibada 426 na kati yake nyumba 306 ziko nchini Italia.

Patriaki: Sala
31 May 2019, 19:12