Tafuta

Vatican News
Wakristo wengine wanne nchini Burkina Faso wameuwawa Jumapili 26 Mei wakiwa wanasali Kanisani Wakristo wengine wanne nchini Burkina Faso wameuwawa Jumapili 26 Mei wakiwa wanasali Kanisani  (SESAME PICTURES)

Burkina Faso:Mashambulizi dhidi ya Kanisa Katoliki na watu kufariki!

Jumapili 26 Mei 2019 wakati wa maadhimisho ya MisaTakatifu watu wanne wameuwawa na magaidi huko Toulfe nchini Burkina Faso kufuatia na mashambulizi ya kigaidi katika Kanisa Katoliki.Katika Tweet ya Papa anakumbusha kuwa hata leo hii wakristo wengi wameuwawa na kuteswa kwa ajili upendo wa Kristo.Hawa wanatoa maisha katika ukimya kwa sababu kifodini hakitangazwi na vyombo vya habari

Na Sr. Angela Rwezaula

Watu wanne wameuwawa katika mashambulizi mapya katika Kanisa katoliki wakati wa misa Jumapili 26 Mei 2019 huko Toulfe nchini Burkina Faso, katika kijiji kimoja km 20 kutoka Titao, mji mkuu wa Wilaya Loroum kusini. “Jumuiya ya kikristo mahalia imeshambuliwa kwa mara nyingine tena na magaidi  wakati wameunganisha kwa ajili ya kusali, kwa  mujibu wa taarifa kutoka kwa Askofu Kietenga wa Ouahigouya.

Baba Mtakatifu anasema vurugu dhidi ya wakristo hazitangazwi na vyombo vya  habari

Mara baada ya mashambulizi mapya dhidi ya Kanisa Katoliki, Baba Mtakatifu katika Tweet yake anakumbusha kuwa hata leo hii wakristo wengi wameuwawa na kuteswa kwa ajili upendo wa Kristo. Hawa wanatoa maisha katika ukimya kwa sababu kifo dini hakitolewi habari. Lakini lei hii wapo wakristo wafiadini zaidi ya karne iliyopita.

Na kwa mujibu wa ushuhuda  wa tukio hilo kwa njia ya gazeti la kimisionari Fides, watu 8 wakiwa na silaha walifika katika kijiji asubuhi ya saa 3.00 wakiwa na pikipiki 4. Waliingia Kanisani mahali ambapo waamini walikuwa wameunganika siku ya Jumapili wakisali na kufyatua risasi. Watu wanne walifariki hapo hapo, wakati mtu  mwingine alifariki baadaye akiwa na majeraha mengi mwilini na baadhi wamejeruhiwa.

Ni shambulio la nne kwa jumuiya ya kikristo katika siku za hivi karibuni

Mwishoni mwa mwezi Aprili watu wenye silaha walimuua mchungaji wa kiprotestanti na waamini wengine watano katika Kanisa jingine nchini Burkina faso Kaskazini. Padre mkatoliki na waamini watano wa Parokia  moja waliuwawa katika mji wa  Dablo tarehe 12 Mei na wakatoliki wengine wanne waliuwawa katika mashambulizi ya  kigaidi siku mbili baadaye katika mji wa Ouahigouya Kaskazini. Hata hivyo serikali inashutumu vikali makundi ya kigaidi yasiyo kuwa na jina ambayo yanaendelea kupigisha magoti  Ukanda mzima wa Sahel .

Na zaidi kuna vikundi vya itikadi kali vilivyo na makao yake huko Mali wakitumia sehemu za kaskazini na katikati ya nchi kufanya mashambulizi karibu na Burkina Faso na Ger. Mashambulizi ya kigaidi nchini Burkina Fazo yameanza tangu Aprili 2015 wakati makundi ya kijihadi yalipomteka nyara askari mlinda usalama katika machimbo ya madini ya Manganese huko Tambao, kaskazini ya Nchi. Na tangu wakati huo, mashambulizi ya makundi hayo yanazidi kuongezeka. Kwa mujibu wa kituo cha utafiti wa mkakati wa Afrika, mashambulizi haya yamezidi kutoka 3 kwa mwaka 2015 kufikia 12 mwaka 21016, 29 mwaka 2017 na 137 mwaka 2018

Makundi ya kijihadi yanafanya kazi yake katika kanda za Sahel

Hata hivyo taarifa zinathibtisha kuwa Kanda yenye kusuasua na usalama ni Sahel ambayo Kaskazini inapakana na Mali na Niger mahali ambapo kuna mashambulizi na kuteka nyara kwa upande wa makundi ya kijihadi.  Hata hivyo kwa upande wa Mashariki ya nchi pia umezidi kuwa na hali mbaya wakati wa kiangazi mwaka 2018. Nchini Burkina Faso ni  nchi ambazo zinaunganisha umoja na nchi nyingine nne na kufanya  G5 za ukanda wa sahel, kwa maana hiyo ni nchi ya Mali, Mauritania, Niger e Ciad, kama  Kikundi kimoja kinachopambana na ugaidi wa kijihadi katika Ukanda huo.

Ukimya wa dunia dhidi ya matukio ya mateso ya wakristo

Baba Mtakatifu Francisko tangu mwanzo wa kutangazwa kuwa Papa amekuwa makini zaidi juu ya jumuiya ya kimataifa kuhusiana na  matukio ya vurugu dhidi ya wakristo na  kwa mujibu wa maneno yake amesema mara nyingi vurugu hizi hazitangazwi na vyombo vya habari na mara nyingi ni kimya kigumu kwa upande wa wenye  nguvu ambao wangeweza hata kusimamisha (Misa katika Kanisa la Mtakatifu Marta 7 Septemba 2015)

Wafiadini waliofichika ambao hatujuhi hata majina yao

Kanisa leo hii ni Kanisa la wafiadini, anasema Baba Mtakatifu na kwamba ni  wafiadini waliofichika wa kila siku ambao hatujuhi hata na majina yao na ambao wanateseka katika vituo vya jela au wanaosingiziwa na wanateswa kwa ajili ya kutetea na kubaki na imani na Yesu. Wao wanateseka, wao wanatoa maisha na sisi tunapokea baraka ya Mungu kwa ajili ya ushuhuda wao” (Misa katika Kanisa la Mtakatifu Marta  21 Aprili 2015).

28 May 2019, 14:10