Tafuta

Vatican News
Askofu Mkuu Pizzaballa Msimamizi wa Kitume nchi Takatifu anawashauri waamini katika kipindi hiki kigumu kwa Kanisa na ulimwengu kuinua mtamzamo wao kwa Bwana Askofu Mkuu Pizzaballa Msimamizi wa Kitume nchi Takatifu anawashauri waamini katika kipindi hiki kigumu kwa Kanisa na ulimwengu kuinua mtamzamo wao kwa Bwana  

Yerusalemu:Ujumbe wa Kwaresima wa Askofu Mkuu Pizzaballa

Katika fursa ya kuanza kipindi cha Kwaresima, Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa ametoa ujumbe wake kwa waamini katika nchi Takatifu akisisitizia juu ya kutoa sadaka kuliko kukusanya kwa ajili ya manufaa binafsi

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Kupata fursa ya kusikiliz za Neno la Mungu; kusali katika Parokia, kusikiliza Mungu kabla ya kusikiliza matakwa binafsi, kuadhimisha kwa imani na kuishi kwa pamoja katika sakramenti ya ya upatanisho; kufunga  katika maisha yao hasa si katika kujikatala kile kinacho vimbisha tumbo, badala yake kutafuta kile ambacho kinaujaza moyo kwa dhati; kurudia katika Ekaristi ya upendo ambayo kweli unashibisha njaa ya maisha na furaha; kutambua kutoa kuliko kukusanya zaidi kwa ajili ya matakwa binafsi. Haya na mengine ndiyo maelekezo yaliyotolewa katika ujumbe katika  hija ya Kwaresima kwa waamini wa Upatriaki wa Kilatini katika mji Mtakatifu Yerusalemu na Msimamizi wa Kitume Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa.

Kupyaisha imani kwa Bwana

Katika ujumbe wake wa Kwaresima 2019 ambao umesambazwa katika Upatriaki wa nchi Takatifu Yerusalemu, Askofu Mkuu Pizzaballa anawashauri waamini katika kipindi hiki kigumu kwa Kanisa na ulimwengu kuinua mtamzamo wao kwa Bwana na kupyaisha imani yao kwa uwepo wake na katika matendo yake. Na anasema kwamba iwapo Kanisa halikusita kujieleza kuwa Kwaresima na Pasaka kama sakramenti ni kwa sababu ya kutaka kukumbusha kuwa, Yesu sasa yupo hapa mwenyewe, katika nguvu ya Roho na katika utii wa imani yetu, yeye ni karibu nasi na kutembea nasi katika njia ya kuelekea jangwani, hadi tutakapofikia katika bustani ya Pasaka, mbele Yake na makaburi yetu, hadi kufikia kuondokana na kila aina ya huzuni na uchungu wa kifo.

Changamoto za jangwa la maisha

Akitazama juu ya changamoto maisha,Askofu Mkuu Pizzaballa anathibitisha kuwa zawadi na jitihada za Kwaresima ni changamoto za jangwa katika kukabiliana na ukavu wa maisha yetu na shughuli zetu, hata za kichungaji, namara nyingine, bila kutafuta njia za mikato ya miujiza, ahadi , kukata tamaa na iliyo mbaya zaidi, dhambi, lakini pia kushirikishana imani na matumaini ya Yesu kwa upendo wa Baba na uzuri wa Mbingu. Katika kipindi hiki katika Kanisa lao na katika jumuiya zao, zilizojaribiwa hivyo, wakati mwingine zinafafana na zile za jangwa ya kwaresima  ambapo wanaweza kuadhimisha katika roho na ukweli wa sakremento ya kwaresima, iwapo watu daima watapata nafasi ya kusikiliza kutoka katika Neno la Mungu, iwapo wataacha  ubinafsi na kujiependelea, kuondokana na kukata tamaa, iwapo watamkaribisha maskini na mwenye kuhitaji na ndipo sasa katika maisha yao watakuwa wamekombolewa na kila ina ya uhakika wa uongo kwa kukaribisha zawadi na kushirikishana; na wanaweza kweli kutengeneza njia ya Pasaka yenye rutuba ambayo ni maisha yanayozaliwa kwa sababu ya kujitoa binafsi.(SIR)

08 March 2019, 15:02