Tafuta

Vatican News
Mkutano wa mwaka umeongozwa na Msimamizi wa Kitume katika Upatriaki wa Kilatino wa Yerusalemu Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa Mkutano wa mwaka umeongozwa na Msimamizi wa Kitume katika Upatriaki wa Kilatino wa Yerusalemu Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa   (ANSA)

Ujumbe wa mwisho wa maaskofu kanda ya kiarabu

Ulinzi wa watoto,shughuli za kichungaji kwa vijana,familia na hali halisi ya Kanisa mahalia,jitihada za kutoa daraja la mapadre na mashamasi hata wasiwawasi kwa ajili ya kuwakaribisha walio wadhaifu ndiyo zimekuwa mada msingi katika Mkutano wa Maaskofu wa kanda ya Kiarabu kuanzia tarehe 18-21 Februari 2019 nchini Misri

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Utoto na ulinzi wa watoto,shughuli za kichungaji kwa vijana, familia na hali halisi ya Kanisa mahalia, jitihada za kutoa daraja la mapadre na mashamasi hata wasiwawasi kwa ajili ya kuwakaribisha walio wadhaifu (waliochwa au yatima na wahamiji), ndizo zimekuwa mada msingi katika mkutano wa Mwaka wa Baraza la Maaskofu wa Kilatino katika Kanda ya Kiarabu uliofanyika kutanzia tarehe 18-21 Februari 2019 katika Seminari ya Kikoptiki Katoliki ya Maadi huko Cairo nchini Misri.

Mkutano Mkuu umeongozwa na Msimamizi wa Kitume nchi Takatifu

Mkutano wa mwaka umeongozwa na Msimamizi wa Kitume katika Upatriaki wa Kilatino wa Yerusalemu Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa. Kwa mujibu wa Upatriaki wa Yerusalemu, uliongozwa na mada ya utoto na ulinzi wa watoto katika mada ya kina kutafakari kwa mwanga wa mkutano ambao umemalizika hivi karibuni mjini Vatican  wa tarehe 21-24 Februari 2019 uliokuwa unahusu ulinzi wa  wa watoto. Kwa namna hiyo umekuwa ni mwendelezo wao wa kutafuta njia  kwa pamoja ya  kuweza kukabiliana na kesi ya manyanyaso juu ya watoto. Kwa pendekezo hili Baraza la Maaskofu wa Kilatino katika Kanda ya Kiarabu. Katika mchakato wa kazi yao, maaskofu walimealikwa kuongozwa kwa dhana ya maparokia yao na Kanisa, misingi ambayo unaguswa na  umma na kuhusisha taasisi zote!

Kuna haja ya kuwaandaa walimu wenye karama ya kuhamasisha kwa shauku vijana

Aidha shughuli nzima ya kazi Upatriaki inatoa taarifa kuwa wameweza kuvumbua matatizo ya pamoja katika majimbo yao wanayowakilishwa na kutafuta suluhisho ambalo linawezakana kuwashirikisha. Mjadala wao  pia ulijikita katika suala la vijana na katika kukabiliana na upungufu wa miito. Ufunguo wa mada hiyo umetazamwa kufuatia kwa Siku ya vijana huko Panama na mhutasari wa Sinodi ya Maaskofu kuhusu vijana, imani na mang’amuzi ya miito, uliofanyika mwezi Oktoba 2018, mjini Roma. Kwa mtazamo huo wamegundua ulazima wa kujilita kwa kina katika mafundisho ya walimu ambao ni wenye karama ya kuweza kuwasaidia vijana. Ni lazima kutambua na kugundua mbinu ya kuwaandaa viongozi wenye karamana ili kuweza kuhamaisha kwa shauku vijana.

Kuna umuhimu wa kuwasindikiza familia za ndoa na vijana wenye nia ya kutaka kufunga ndoa

Kati ya uwezekano wa kuanzisha masuala ya uhamasisha ni pamoja na muunganiko wa wa kuhamasisha shughuli ya kichungaji kwa vijana katika maandalizi ya Siku ya Vijana ijayo 2020. Kadhalika mada nyingi kuu ni ile ya familia ambapo maaskofu wanaonoa kuangua kwa familia nyingi kiimani hasa migawanyiko , talaka na  jeruhiwa, aidha na  matatizo mbalimbali ya hali na zaidi ukosefu wa kuzaa watoto. Maaskofu wamesisitizaia ulazima wa umakini katika  kuingilia kati ili kuwasadia kuwa na utambuzi kwa upya. Ni msingi kwa vijana wote wenye kutamani  kuanza familia ili weweze kufundishwa na kuongozwa na Kanisa. Kati ya suluhisho linalotarajiwa kukabiliwa ni kuwaandaa wenye kutaka kufunga ndoa, kuwasindikiza vijana ambao wameshaoa katika hatua zao za kwanza baada ya kufunga ndoa.

Kukabiliana na matukio ya ukosefu wa imani

Wakitazama imani kwa waamini, maaskofu wanakabiliana na matukio ya ukosefu wa imani kwa watu na kwa namna ya pekee mtazamo wa watu wenye tabia ya kujijengea sura ya Mungu  kadri ya kipimo binafsi wakiacha mafundisho ya Kanisa. Tabia kama hiyo maaskofu wanasema ni hatari kubwa inayopelekea kujibagua na kumpelekea mwaamini awez na tasaufi binafi ya kujitosheleza mwenyewe! Kutokana na hiyo maaskfou wanatoa pendekezo kwa mapadre, kuwaandaa vema waamini na kutazama kwa makini mahubiri na katekesi zao wanazotoa, kwa namna ya kubadili mtindo kama ni mgumu basi uwe rahisi na mabadiliko hayo ni kwa ajili ya kuweza kusisitizia juu ya fumbo la Kristo,ukuu wake kwa kubadilika katika njia ya neema. Mada nyingine ya mkutano imehusu uekemene, ambapo Maaskofu wamebainisha juu ya furaha ya kutiwa moyo  katika kutafuta namna ya kutafsiri Biblia kwa matumizi ya kiliturujia ya pamoja katika Makanisa. Mkutano huo  kwa upande huo wamependekeza kuunda Tume kwa ajili ya liturujia na kutuma kiungo hiki maalum mijini Vatican kwa sababu ya kuomba ridhaa ya  Misale ya waumini na Liturujia ya  Masifu na tafsiri nyingine za kanuni ya kutoa ushemasi, upadre na uaskofu.

Hati ya udugu wa kibanadamu iliyotiwa saini huko Abu Dhabi

Na zaidi katika mada hiyo ya uekumene, kwa namna ya pekee katika mkutano umekuwa na utajiri mkubwa wa muungano wa kidugu wakiwa na Mkuu wa Kiorthox Tawadros II, Patriaki wa Kanisa la Kiorthodox na Patriaki Ibarahim Isac Sidrak wa Kanisa la Kikoptiki Katoliki. Na mwisho Baraza la Maasfofu wa Kanda ya Kiarabu wamelezea kupendezwa kwao kwa ziara ya kihistoria ya Baba Mtakatifu Francisko huko Abu dhabi. Maaskofu kwa namna ya pekeee wametafakari kwa muda mrefu kutazama Hati inayohusu Udugu kibinadamu kwa ajili ya amani duniani, ambapo waliweza kuona kutiwa sahini  huko Abu Dhabi na kwamba wanaona dharura kubwa ya kueneza  ujumbe huo maana ya kile kilichomo ndani yake na hatimaye kuweza kuboresha elimu kwa waamini, wanandoa na walei. Katika Mkutano huo wa mwaka alipata kushiriki kati yao, Askofu Mkuu Bruno Musarò Balozi wa Vatican nchini Misri na ambaye wamemshukuru kwa uwepo wake  kwa kipindi chote cha mkutano wao.

04 March 2019, 15:26