Tafuta

Ni lazima kuthubutu amani.Ni lazima kufanya uzoefu katika mwanga wa historiailiyopita ambayo inathibitisha kwamba hakuna amani bila Mediterranea,kwani inaunganisha Ni lazima kuthubutu amani.Ni lazima kufanya uzoefu katika mwanga wa historiailiyopita ambayo inathibitisha kwamba hakuna amani bila Mediterranea,kwani inaunganisha  

Mkutano wa Baraza la Maaskofu Italia 2020 kwa ajili ya amani katika Mediterranea!

Kuanzia tarehe 19-23 Februari 2020 huko Bari nchini Italia utafanyika Mkutano kwa ajili ya kuzungumzoa juu ya amani katika eneo la Mediterranea na ambapo Kamati ya Kisayansi ya maandalizi ikiongozwa na Kardinali Gualtriero Bassettti Rais wa Baraza la Maaskofu Italia CEI wamekutana kwa mara ya kwanza mjini Roma tarehe 21 Machi 2019

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Bahari ya Mediterranea ni kama mpaka wa amani mahali pa kuweka maagano na kujikita kwa dhati  katika jitahada za kuwa wajenzi wa maelewano na mapatano. Ndiyo lengo la mkutano wa tafakari na tasaufi ya amani kuhusu Meditetranea, unaotarajiwa kufanyika huko Bari nchini Italia kuanzia tarehe 19-23 Februari 2020, ambapo Kamati ya Kisayansi ya maandalizi ikiongozwa na Kardinali Gualtriero Bassettti Rais wa Baraza la Maaskofu Italia CEI wamekutana kwa mara ya kwanza mjini Roma tarehe 21 Machi 2019.

Kardinali Bassetti katika hotuba yake kwenye mkutano huo amesisitiza kwamba, wanapaswa kuthubutu amani. Wanapaswa kufanya uzoefu katika mwanga wa historia yao  iliyopita ambayo inathibitisha kwamba, hakuna amani bila Mediterranea, kwa maana, iwapo Mediterranea haiunganishi inaweza kugawanya dunia na wanaoteseka zaidi kutokana na mgawanyiko huo, Kardinali Bassetti anathibitisha kuwa, Baba Mtakatifu Francisko angesema kwamba, daima ni maskini! Akiendeleza na maelezo yake anasema, inatosha tu kutazama habari za kila siku kwenye luninga, ili kujua ni kitu gani kinaendelea katika dunia hii. Uwajibikaji mkubwa kwa ajili ya amani duniani, unahitajika kwa kasi lakini hiyo ni kwa wakristo wote na wote wenye mapenzi mema!

Kardinali Bassetti akinukuu maneno ya liyokuwa akisema padre mmoja Enesto Balducci anasema: kama tunaacha eti wakati endelevu uje peke yake kwa jinsi ambavyo umekwisha na hatujitambui wajibu wetu na wa mababa zetu, basi hakutakuwa na matarajio ya wakati endelevu. Wakati endelevu unapaswa ujengwe sasa hivi. Iwapo tunaamua kwenda kukutana na mwingine kwa mikono iliyo jaa urithi tofauti na kushikana kati ya maagano ambayo yanadumisha umoja asili, ndipo kweli tutakuwa na utambuzi wa maana ya vikwazo ambavyo leo hii vinafunga mipaka yetu. Katika kukabiliana na Mkutano ujao huko Bari 2020, wanahitaji kuondokana na vizingiti nafsi amesisitiza.

Naye Askofu Antonino Raspanti Makamu rais wa Baraza la Maaskofu Italia (Cei) kwa ajili ya Italia ya Kusini anathibitisha kwamba Mediterranea siyo suala tu la kuona kama eneo la kijografia au muundo wakisiasa na  kijiografia, bali ni nafasi ya kihistoria, iliyo na mahusiano mengi na ambayo yanapishana  kati yake na kukubaliwa katika mkutano hata malumbano. Ni kutoka katika ugumu na ukubwa wa eneo la Meditterranea, hadi kufanikiwa kwake, ongezeko lake  ndipo inawezekana kutambua  na kujiwekea wito ambao si wa sintofahamu, bali ambao umeunganishwa kwa pamoja kwa njia ya wito wa kiinjili. Kutokana na hili, tunasukumwa  zaidi na zaidi kukaribisha wito katika ishara ya matumaini na kuamini uwezekano wa kujitoa na kuchangia. Kwa mujibu wa Askofu Ruspanti:kulinda hali halisi na ukweli ni kitu kimoja cha kupokelewa katika Injili ambayo inashinda vikwazo dhidi ya ukosefu wa usawa, ulaghai na kukosa huruma. Mazungumzo, lazima yaanzie kwa kusikiliza Injili ya pamoja ya Yesu Kristo, mahali ambapo leo hii bado inasikika wito wa  uongofu ili kupokea Ufalme ambao umetambuliwa, anahitimisha Askofu Ruspante.

22 March 2019, 15:44