Tafuta

Padre Francesco Patton,msimamizi ya Nchi Takatifu na viongozi wengine mapatriaki Padre Francesco Patton,msimamizi ya Nchi Takatifu na viongozi wengine mapatriaki 

Misri:Katika mkutano wa Damietta unaonesha kuwa amani haipatikani katika udhaifu

Padre Francesco Patton,msimamizi ya Nchi Takatifu athibitisha kuwa mkutano wa Damietta mahali ambapo Mtakatifu Francis wa Assisi alikutana na Sultani unakumbusha ni kwa jinsi gani udhaifu wa amani hauwezi kushinda adui

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tarehe 2 Machi 2019 Msimamizi wa Nchi Takatifu Padre Francesko Patton ametoa hotuba yake akiwa mjini Cairo katika Chuo Kikuu cha Kiislam cha Al - Azhar kwenye mkutano uliondaliwa pamoja na Shirika la Wafransiskani huko Misri na Shirika la Kimataifa wenye shahada kutoka Chuo Kikuu cha Al-Azhar. Ni Mkutano ulio ongozwa na mada ya mazungumzo ya Amani na uhakika kati ya Mabalozi wa Al-Azhar na Shirika la Kifransiskani.

Mkutano huo umeandaliwa katika fursa ya kuadhimisha miaka 800 tangu Mtakatifu Francis wa Assisi alipokutana na Sultani Al-Kamil Al-Malek, huko Damietta. Hayo ni maadhimisho yaliyo anza tarehe 1-3 Machi 2019. Katika kipindi cha vita kati ya wakristo na waislam Mtakatifu Francis wa Assisi na Sultani walipata fursa ya kuwa na uwezo wa kuzungumza na waamini kwa kuheshimiana kati yao, kusikilizana na kupokeana, amethibitisha Padre Patton.

Baada ya miaka 800, mkutano huo unajikita katika thamani yake na kuwa na mapendekezo mapya ya kwenda kinyume na dunia, kwa kuheshimu utamaduni wa kuvumiliana na kupinga vizingiti. Katika nyakati kama hizi Padre Patton ameongeza kusema  kuwa wengine wanapendekeza ghasia kwa wazalendo na kukimbilia katika matumizi ya nguvu na fujo,wakati huo  mkutano wa Damietta, unakumbusha ni kwa jinsi gani ipo nafasi hasi ya kutumia vurugu na nguvu, kwa jinsi gani ni kujidanyanya kuwa na ushindi kwa njia kutumia nguvu, aidha ni kwa jinsi gani udhaifu wa amani hauwezi kumshinda adui.

Badala yake, Mkutano wa Damietta kati ya viongozi  wawili  ilikuwa ni kuonesha kwamba ni kwa njia ya kukutana na kuzungumza, inawezekana kuzaa matunda ya muda mrefu. Aidha Msmamizi wa Nchi Takatifu ameshukuru kwa upya Al – Tayyib kwa ajili ya kutia sahini huko  Abu dhab na Baba Mtakatifu Francisko na kwamba juhudi za ndugu wadogo wa Mtakatifu Francisko wa Asisi katika  Nchi Takatifu watazidi kueneza ujumbe huo.

Kwa kuhitimisha, Padre Patton amesema  leo hii katika shule za Nchi Takatifu, kama zilivyo hata v shule nyingine za ndugu wadogo wa Fransiskani katika Familia Takatifu Misri, ni mfano wa dhati kuhusu udugu, mazungumzo na katika juhudi ya pamoja ya kujenga utamaduni na kuelimisha amani ambayo ndiyo ahadi msingi wa kila tendo la Amani. Maombi kwa ajili ya amani ndiyo iwe kiini katika sala zao ili kuweza kupata zawadi  kutoka kwa Bwana; na ili mbegu ya amani iliyopo ndani ya mioyo yao iweze kuchanua maua  ambayo atimaye yalete matunda kwa njia ya maneno na matendo yao (SIR).

04 March 2019, 15:08