Tafuta

Vatican News
Familia ya Mungu nchini Morocco inamshukuru na kumpongeza Papa Francisko kwa kuitembelea! Familia ya Mungu nchini Morocco inamshukuru na kumpongeza Papa Francisko kwa kuitembelea!  (Vatican Media)

Hija ya Papa Francisko Morocco 2019: Jamani, Morocco kumenoga!

Baba Mtakatifu, amekuwa ni chemchemi ya faraja na matumaini ya kusonga mbele kwa ari na moyo mkuu katika ujenzi wa udugu wa binadamu unaofumbatwa katika mshikamano, kielelezo cha Injili ya Msamaria mwema, utambulisho wa Kanisa la Morocco! Amekazia mchakato wa majadiliano ya kidini na waamini wa dini ya Kiislam, katika ukweli na unyenyekevu!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Askofu Mkuu Cristabal López Romero wa Jimbo kuu la Rabat, Morocco, mwenyeji wa hija ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Morocco kuanzia tarehe 30-31 Machi 2019 iliyokuwa inaongozwa na kauli mbiu “Papa Francisko mhudumu wa matumaini Morocco 2019” amemshukuru na kumpongeza Baba Mtakatifu Francisko kwa kuwatembelea na kuhimiza ushuhuda na ujenzi wa Ufalme wa Mungu nchini Morocco.

Baba Mtakatifu, amekuwa ni chemchemi ya faraja na matumaini ya kusonga mbele kwa ari na moyo mkuu katika ujenzi wa udugu wa binadamu unaofumbatwa katika mshikamano, kielelezo cha Injili ya Msamaria mwema, utambulisho wa Kanisa la Morocco! Amekazia mchakato wa majadiliano ya kidini na waamini wa dini ya Kiislam, katika ukweli na unyenyekevu! Morocco inaendelea kuwa ni daraja kati ya Bara la Afrika na Ulaya; Kati ya watu wa Mashariki na Magharibi; tayari kushiriki katika ujenzi wa utamaduni wa watu kukutana na kusaidiana. Hii ni chachu ya matumaini kwa leo na kesho iliyo bora zaidi!

Hija ya Baba Mtakatifu Francisko nchini Morocco inajikita katika mchakato wa kujenga na kudumisha amani na udugu wa kibinadamu unaofumbatwa katika majadiliano ya kidini pamoja na ushuhuda wa uekumene wa upendo, tema ambazo zinapewa msukumo wa pekee na Baba Mtakatifu Francisko katika kipindi cha mwaka 2019.

Askofu Mkuu Lopez
31 March 2019, 17:59