Cerca

Vatican News
Licha ya wahamiaji,Askofu mkuu wa Johannesburg anasema,lazima kujumuisha mantiki pia ya watu wanaoishi katika mtaa wa mabanda,kwani hao pia hawana makazi Licha ya wahamiaji,Askofu mkuu wa Johannesburg anasema,lazima kujumuisha mantiki pia ya watu wanaoishi katika mtaa wa mabanda,kwani hao pia hawana makazi  (AFP or licensors)

Afrika Kusini:Kwaresima ni kipindi cha kujenga jumuiya ya ukarimu

Askofu Mkuu Buti Joseph Tlhagale wa Jimbo Kuu Katoliki la Johannesburg,katika ujumbe wake wa kwaresima umejikita katika mada ya wahamiaji kwa kuangazia hali halisi ya mji mkuu wa kiuchumi chini Afrika Kusini.Amezindua kampeni ya kujenga makazi kwa ajili ya watu wasio na makazi katika jiji kuu hilo

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mji wa Johannesburg ni mama gani? Je hupaswi kuwa kama mama ambaye hukusanya watoto wake wote? kama vile kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake! (Mathayo 23:37). Ni maneno magumu kweli ya Askofu Mkuu Buti Joseph Tlhagale, wa Jimbo Kuu Katoliki la Johannesburg, katika ujumbe wake  wa Kwaresima 2019 ambao umejikita katika mada ya wahamiaji akimlikia mji mkuu wa kiuchumi chini Afrika Kusini.

Kwa kutumia wito wa Injili Matayo ni pale ambapo ilikuwa muda mufupi mbele ya kifo chake, Yesu alichukua muda fulani ili kuangalia jiji kubwa la Wayahudi. Kwa huzuni alisema hivi amaneno haya ‘Yerusalemu, Yerusalemu, muuaji wa manabii na ambaye huwapiga kwa majiwe wale waliotumwa kwake, ni mara ngapi nilitaka kuwakusanya watoto wako, kama vile kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake! Lakini hamukutaka (Mathayo 23:37).

Kwa maana hiyo, askofu Mkuu anataka kusisitiza juu ya kutazama kwa kina msaada wa binadamu katika jiji na hivyo anasema kuwa, ushirikishwaji wa wahamiaji wanaotoka katika nchi za karibu kama vike Msumbiji na Zimbabwe na wa mbali kama vile  (RDC, Nigeria) , vilevile na baadhi ya nchi kutoka barani Asi  ndiyo mada moto moto katika nchi yenye rangi nyingi. Askofu Mkuu  Tlhagale anatoa umakini zaidi katika  hali halisi ya maisha yalivyo mabaya kwa upande wa wahamiaji na wakimbizi ambao hawana nyumba, na kwamba ni watu wasiotamaniwa katika sura ya ardhi hyo.

Kufuatia na hali halisi hiyo, Askofu mkuu anathibitisha kuwa pia lazima kujumuisha hata mantiki ya watu ambao wanaoishi katika mtaa wa mabanda, yani makazi duni kabisa ya kimasikini. Hata  hao kwa ujumla hawana makazi. Hali zao za maisha ni uharibifu na zenye ukatili. Watu wamekuwa na uchungu na kukosa heshima na hadhi waliyopewa na Mwenyezi Mungu. Anasema: “Nchi hii katika bara la Afrika na ambayo ilikuwa inafahamika kwa mataifa mengi wakati uliopita kuwa ni nzuri sana, sasa ni  yenye uharibifu na magofu kamili. Wewe hujali mateso ya wageni. Wewe hujali maumivu ya watoto wako wasio na makazi, njaa na wagonjwa”

Akikumbuka maneno ya Maandiko matakatifu  ambayo yanaelezea hali halisi ya wahamiaji wengi na wakimbizi, Askofu Mkuu Tlhagale anawahimiza waamini kuwajibika na kuwa na umakini wa hali yao ya shida,na ambapo watu hao wanalazimika  kuomba omba kwa sababu hawana hati na sifa zinazohitajika ili kupata kazi, wengi wao wanalala chini ya madaraja, wanazungunguka huku na huku jijini na wakati mwingine wakisumbuana na kugombana waendesha magari barabarani.

Askofu Mkuu Tlhagale mwisho ametoa  wito ili wakati wa Kwaresima uweze kugeuka kuwa kipindi mwafaka cha kujenga jumuiya ya kukaribisha(…). Ni wakati wa kurudisha ubinadamu na  uwakumbatia wageni katikati  yao, anasemana kuongeza, hiyo ni  kuwahusisha jitihada hizo kwa mashirika yote ya Kanisa. Na kwa kufanya hivyo wanaanzisha kampeni ya Kwaresima katika jiji la Johannesburg ili kujenga makao kwa wahamiaji na wakimbizi walio masikini waweze kulala chini ya paa na siyo nje ya nyumba. Wataweza kubadili Johannesburg katika mji wa kukaribisha anahitimisha.

19 March 2019, 13:54