Cerca

Vatican News
Yanaendelea maandalizi ya Mkutano wa Rais wa Marekani na Korea Kaskazini tarehe 27 na 28 Februari 2019  huko Hanoi Vietnam Yanaendelea maandalizi ya Mkutano wa Rais wa Marekani na Korea Kaskazini tarehe 27 na 28 Februari 2019 huko Hanoi Vietnam   (ANSA)

COREA:Kuna shauku kubwa ya amani na umoja katika Peninsula

Ni tukio la kwanza la ziara katika mwaka 2019 iliyoandaliwa tarehe 12 Februari na Tume ya pamoja ya chama cha Walei na Jumuiya za Kitawa nchini Korea ya Kusini,kuelezea haja ya kuungana kuanzia chini.Ni sawa na ukaribu kwa mara nyingine tena wa mkutano kati ya viongozi wakuu wa Korea Kaskazini na Marekani tarehe 27 na 28 Februari,huko Vietnam

Na Sr.Angela Rwezaula - Vatican

Nimeona na kutambua kwamba amani ni shauku kubwa ya watu wa Korea ya Kaskazini. Mantiki hiyo ni muhimu ambayo inajikita kwa undani hasa kuwa na matumaini makubwa ya wakati endelevu ulo bora. Ni kutazama kwa hamu kubwa wakati endelevu wa safari ya kufikia muungano kamili kati ya Korea mbili. Haya ni maelezo ya  Askofu Mkuu Hyginus Kim Hee-joong wa jimbo la Gwangju na rais wa Baraza la Maaskofu Korea akisimulia juu ya ziara yao waliyofanya huko Korea Kaskazini wakiwa na wawakilishi wa zaidi ya watu 200  wa Korea Kusini. Ni tukio la kwanza la ziara katika mwaka 2019 iliyoandaliwa tarehe 12 Februari na Tume ya pamoja ya chama cha Walei na  Jumuiya za Kitawa nchini Korea ya Kusini, kwa lengo la  thamani  kuu ya pamoja na ili kuelezea haja ya wajibu wao wa kuungana kuanzia chini.

Ukaribu katika mkutano wa Rais wa Marekani na Korea ya Kaskazini, 27 na 28 Februari nchini Vietnam

Askofu Mkuu anafafanua kupitia Gazeti la Ossservatore Romano anathibitisha kwamba, mashule, mameya, vyuo vikuu, vyama vya utamaduni na michezo vyama vya vijana, jumuiya za watawa kwa ushiriki wa wabunge, waandishi wa habari wote wamejumuishwa na wamekuwa na shauku ya kutaka kuwa na mawasiliano, mahusiano na mipango mipya ya ushirikiano na jamii ya Korea Kaskazini.  Tendo la uwezekano huo limewezekana kukutana kwa upya kwa ajili ya kuunda mahusiano kati ya nchi mbili mara baada ya mkutano wa kihistoria wa viongozi wakuu Rais wa Moon Jae-in e Kim Jong-un mwezi Aprili 2018 na taratibu kuanzishwa kwa upya mchakato wa kukaribiana na ambao unatazamia hatua msingi ya mkutano ujao kati ya Rais wa Marekani Bwana Donald Trump na Rais wa Korea Kaskazini, tarehe 27 na 28 Februari nchini Vietnam.

Imani ya pamoja

Fursa ya mkutano wa siku mbili iliyofanyika katika kituo cha utalii juu ya mlima wa Kumgang, katika fukwe za mashariki ya Korea Kaskazini, imeadhimishwa kwa pamoja katika mwaka wao mpya, ulioanza tarehe 5 Februari. Katika kusheherekea na kushirikishana tamaduni za tteokkuk, supu ya wali, chakula asili cha utamaduni kwa upande wa Kaskazini ya Peninsula. Askofu Mkuu Kim Hee-joong,ambaye alikuwa ndiyo mkuu wa uwakilishi huo anathibitisha kwamba hii ni ishara kubwa na tunda muhimu ya kuanzishwa kwani inawakilisha kuendendela kushona mahusiano ya pamoja na kuaminiana ikiwa ndiyo msingi wa kila uhusiano wa amani, heshima, uhuru na kiraia. Ni sehemu hiyo ambayo inawezekana kuanza safari ya kuweze kuanzisha mipango tofauti tofauti  ya ushirikiano katika mantiki nyingi kama vile, utalii, utamaduni, dini, mafunzo, michezo na sanaa.  

Ni lazima kushinda hofu ili kuishi kwa pamoja

Yote hayo yanwezekana kutakana na ruhusa na sheria rasmi kutoka kwa waziri wa muungano wa Seul Bwana Cho Myoung-gyon, ambaye ni mtu wa imani katoliki na kama ilivyo rais Moon Jae-in. Waziri alitangaza wazi ya kutaka kuongeza juhudi ya mazungumzo na mabadilishano ya utamaduni na kuunga mkono juu ya mahusiano yenye thamani katika jumuiya za kidini ili kujenga maelewano kati ya makundi yaliyo madogo. Kwa maana hiyo serikali ya Korea Kasikazini ilikubaliana, tangu katikati ya mwaka 2017 zaidi ya maombi ya watu 1000 aliwapatiwa ruhusu ya kuwa na mawasilino ya Korea ya Kaskazini, katika hali mpya ya mahusiano ya sehemu zote mbili. Lengo kubwa ni kuhamasisha nguvu na kuongeza mawasiliano ya kutembelea kwa mantiki pia ya michezo, utamaduni na dini; wakati huo huo kusuka mawazo  mapya katika hatua ya kambi hata ya kisiasa. Kwa sasa ni kipindi cha kupitia kutoka katika hofu ya vita ili kufikia kuishi kwa amani. Dini zinaweza kuleta mchango mkubwa sana wa kujenga amani katika peninsula ya Korea na kuwa kisima cha mapatano kwa mujibu wa Askofu Cho Myoung-gyon.

Matumaini ya Kanisani ni kuona mapatano, utulivu na amani duniani

Adha askofu Kim Hee-joong amesimulia kwa mtazamo wake zaidi ya mipaka na maneno kwamba anaona matumaini. Kwa siku mbili waliishi kiurafiki sana, kushirikishana kwa pamoja na kusikilizana wakati wa kufanya mjadala  na wataalam wa jamii ya Korea ya Kaskazini. Waliojumuika nao ni wawakilishi wa Tume ya mapatano na vyama mbalimbali ambavyo vinatambulika kwa serikali ina  maana ya jumuiya za kidini na wameweza kubadilishana mawazo kwa kina. Moja ya mada muhimu iliyotolewa katika hotuba ya Askofu Mkuu wa Korea Kusini na Kaskazini ameonesha kwamba, wote ni ndugu katika taifa moja la watu. Aidha akaeleza juu ya matendo mema yanayofanywa na diplomasia ya Vatican katika dunia kwa lengo la kutafuta amani , mapatano na utulivu wa kuishi kati ya watu kwa wema wa kila mtu duniani. Amekazia misingi ya kuheshimu na usawa wa kimataifa. Ni dhana ambayo leo hii ni muhimu anathibitisha kuwa, kwa upande wa Korea ya Kaskazini utafikiri ndiyo  lengo la dhati  katika jumuiya za kimataifa.

Kwa kuongoza kikundi cha viongozi wa dini ambao wanajumuishwa na wabudha, wakristo na madhehebu mengine kama dini za kiutamaduni, Askofu Mkuu Gwangju  hakukosa kuelezea shauku ya maaskofu wengine katoliki wa korea kutaka kutembelea moja kwa moja nchini Kore ya Kaskazini. Na amehaidiwa ombi hili kupelekwa kwa viongozi wakuu, hata hivyo anathibitisha kwamba pamoja na hayo yote, leo hii tayari wanaishi hali yenye kuonesha matunda ya ushirikiano na matumaini yanakua. Katika mlima Kumgang, wakorea ya Kaskazini na Kusini waliungana cchini ya anga moja na kusubiri mawio ya jua kwa pamoja katika matazamio ya kuona machweo ya mwaka mpya. Katika utamaduni wao ishara ya matashi mema inayowaruhusu kufikia matarajio mema na endelevu!

19 February 2019, 14:10