Cerca

Vatican News
Kardinale Philippe Nakellentuba Ouédraogo, Askofu Mkuu wa Ouagadougou, Burkina Faso Kardinale Philippe Nakellentuba Ouédraogo, Askofu Mkuu wa Ouagadougou, Burkina Faso  

Burkina Faso:Kardinali Ouédraogo anatoa wito wa dharura

Ni katika kuishi kipindi cha wasi wasi mkubwa na mauajia ya padre Antonio César Fernández Fernández,yamehuzunisha jumuiya nzima kwa mujibu wa Kardinali Philippe Nakellentuba Ouédraogo wa Jimbo Kuu Katoliki la Ouagadougou akihojiana na Vatican News baada ya tukio hili la kigaidi

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Matumaini na utashi wa kujenga hauwaachi watu wa Burkina Faso, japokuwa na kuendela kwa mashambulizi ya nguvu kwa upande wa makundi ya kijihadi. Ijumaa iliyopita aliuwawa mmisonari wa Dob Bosco (salesiani) padre Antonio César Fernández Fernández kwa mikono ya kikosi cha kigaidi. Alishambuliwa na risasi tatu wakati akirudi katika jumuiya yake mji mkuu Ouagadougou. Kwa maana hiyo mauaji na wizi kwa  bahati mbaya katika siku za mwisho umezidi kuongezeka, kwa mujibu wa uthibitisho wa Kardinali Philippe Nakellentuba Ouédraogo, askofu Mkuu wa jimbo Kuu katoliki la Ouagadougou.

Amethibitisha hayo katika mahojiano na Vatican news, kuhusiana na matukio hayo, hata kuhusu mauaji ya Padre Antonio César Fernández Fernández  ambapo Askofu Mkuu alipata taarifa hizo akiwa anaudhuria Mkutano wa wa Mwaka wa Baraza la Kipapa la nidhamu na Sakrameti mjini Vatican. Askofu Mkuu hakuficha masikitiko yake, kwa maana alikuwa anamfahamu vizuri anathibitisha kwamba wiki ya kwanza ya mwezi Februari waliandaa pamoja hija ya jimbo kuu la  Ouagadougou, katika Madhabahu ya Mama Maria , ambapo waliudhuria karibu wakazi 500 na ilikuwa ni ushuhuda wa nguvu, kwani  waamini walifika idadi kubwa sana japokuwa na ukosefu wa ulinzi na usalama.

Kila wiki ni fujo kubwa mpakani mwa Mali na Niger

PadreAntonio alikuwapo katika Misa hiyo na aliweza kukomunisha watu… kama wamisionari hawana parokia anasema, lakini wanatoa huduma kwa ajili ya vijana masikini katika mitaa ya mji mkuu. Kifo chake kimegusa jumuiya nzima. Aidha amasema kwa dhati wanaishi katika hali mbaya kwa maana tayari wamekwisha shambuliwa mara tatu na magaidi katika mji mkuu Ouagadougou na kila wiki anasema, zipo fujo na ghasia nyingi hasa mpakani mwa Mali na Niger, hata na ndani kusini na mashariki ya nchi ya Burkina Faso. Ni changamoto ya kweli katika Afrika ya Magharibi anathibitisha Kardinali Nakellentuba Ouédraogo,

Tarehe 31 Desemba 2018 Serikali ilitangaza dharura katika baadhi ya sehemu za nchi na mwezi Januari waziri Mkuu akajiuzuru. Nchi tano za ukanda wa sahel (Burkina Faso, Mauritania, Chad, Niger, Mali) wana ukosefu wakifedha ili kukubaliana na matatizo, je ni kitu gani kinahitajika? Askofu Mkuu anasema kuwa, wao wanaomba kuwa na mshikamano kwa ngazi ya kimataifa na ndiyo jambo linalokosekana. Mateso ya watu na mtu ni mateso ya ubinadamu mzima. Kwa maana hiyo unakosekana mshikamano. Nchi zote hizi katika dunia zina uwezo wa kuweza kuwasaidia, hivyo wanaweza kufanya lolote la sivyo ni kuzungumza tu lakini  je ni kitu gani kinafanyika kuwakomboa watu hawa walio chini ya vurugu na umasikini? Ni swali la Askofu Mkuu.

Kwa maana hiyo Kanisa linafanya nini?

Akijibu Askofu Mkuu anasema kwamba  wao wameunda kikundi cha kawaida kinacho waunganisha  waislam, wakristo wa kipentekoste na Kanisa Katoliki ili kuweza kufanya kazi kwa pamoja katika mazungumzo ya kidini na kiutamaduni. Wanafikiri kwamba, si kwa njia ya mtutu wa bunduki unaweza kuleta amani, bali ni katika kukuza mazungumzo. Kuna mahitaji ya kutambuana, kuheshimiana kwa pamoja na kufanya kazi kwa pamoja.

Matashi mema na wito kwa nchi na dunia nzima ni upi?

Wito wake Askofu Mkuu ni kwa ajili ya walio ndani na nje. Wa ndani ya nchi  anathibitisha kuwa ni lazima kukuza ndani ya  watu ushirikiano na majeshi, polisi na walinzi wa kila ngazi ambao wanalo jukumu la kujenga na kulinda amani katika nchi. Hili ni jambo muhimu! Lazima kujiuliza maswali, kwa nini kuna watu wengi mahalia wanashirikiana na majihadi? Lazima kujua sababu zake na kutafuta suluhisho. Je ni kwa ajili ya umasikini au ujinga? Ni lazima kujua na kutoa suluhisho la sababu zake. Na wito wake kwa walio nje ya nchi Askofu Mkuu anathibitisha ni kwa upande wa dunia kubwa yaani kwa mataifa yenye uwezo. Kuna ulazima wa mshikamano wa uhakika. Katika nchi tano za ukanda wa Sahel unahitaji matumani,lakini nchi zenye uwezo mkubwa duniani na  zenye utashi, zinamiliki kwa hakika uwezo kifedha, basi ni lazima zioneshe kidogo mshikamano na kusaidia ukanda wa nchi hizi za Sahel ili nao waweze kuishi vema katika maeneo yao. Amani ni zawadi kutoka kwa Mungu na ni tunda la kazi ya watu.

21 February 2019, 09:44