Tafuta

Vatican News
Roho moja,sauti nyingi ni mada itakayoongoza Mkutano wa siku mbili tarehe  13-15 Mei 2019 huko Australia kwa mtazamio wa maandalizi ya Mwezi Maalum wa kimisionari Roho moja,sauti nyingi ni mada itakayoongoza Mkutano wa siku mbili tarehe 13-15 Mei 2019 huko Australia kwa mtazamio wa maandalizi ya Mwezi Maalum wa kimisionari 

Roho moja,sauti nyingi ni mada ya Mkutano Australia!

Roho moja,sauti nyingi ni mada itakayoongoza Mkutano wa siku mbili tarehe 13 -15 Mei 2019 huko Australia katika matazamio ya kuandaa Mwezi Maalum wa kimisionari uliotangazwa na Baba Mtakatifu Francisko kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Nia ya maombi kwa mwezi wa maalum wa kimisionari kwa utashi wa Baba Mtakatifu Francisko ni kukuza roho ya uongofu wa kimisionari kwa kila mmoja wetu hata katika maisha na shughuli za kichungaji za Kanisa. Mkutano utakaongozwa na mada ya utume wa roho moja, sauti nyingi utawakilisha fursa msingi wa kujiandaa kuishi kipindi hiki maalum. Ni uthibitisho wa Peter Gates Mkurugenzi Msaidizi kitaifa wa Utume Katoliki kutoka Ofisi za huduma ya Kipapa ya kimisionari nchini Australia, akifafanua juu ya maandalizi ya Mkutano ambao utafanyika kuanzia tarehe 13 -15 Mei 2019.

Mantiki ya ushirikishwaji, makutano na mazungumzo

Akifafanua juu ya hatia muhimu za Astralia kuhusu manada inayohusiana na changamoto za kimisionari katika Kanisa anasema kati ya matukio yaliyopendekezwa kwa matazamio ya Mwezi Maalum ambao Kanisa Katoliki litaweza kuishi uzoefu mwezi Oktoba 2019, utaona washiriki zaidi ya 450 kutoka majimbo yote ya Taifa ambao wanahusishwa katika mpango wenye tabia ya kisanii, ubunifu na semina mbalibali, katika kutazama kwa kina mantiki ya ushirikishwaji, makutano na mazungumzo.

Mitandao ya kijamii katika dunia ya leo ni muhimu

Kati ya watoa mada ni Askofu Paul Tighe Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Utamaduni ambaye atajikita kuelezea nafasi msingi ya teknolojia katika kueneza Injili na ujumbe wa Utume. Kwa mujibu wa AskofuTighe, anasema mitandao ya kijamii  leo hii ni muhimu kwani inawakilisha chombo katika kutafuta namna ya kuleta uongofu katika ulimwengu ambao daima upo katika mabadilishano ya habari. Kanisa lazima litambue kwamba mitando ya  kijamii ni jambo msingi na linawakilisha dunia ya leo, kwa ajili ya kuwaunganisha kizazi kipya ili kiweze kuwa na dhamiri mpya na tosha ya maisha yao. Na zaidi Askofu wa Ireland, wengine watakaotoa mada katika mkutano huo ni Carol Zinn, SSJ.; mkurugenzi mtendaji wa  Baraza la Kitaifa  ambaye atatoa mada  kuhusu uongozi wa watawa wanawake; Ravina Waldren kiongozi Katoliki wa Asilia katika Jimbo Kuu la Brisbane na Robert Fitzgerald, mjumbe wa Tume ya Uzalishaji katika Serikali ya Australia (Fides 19/2/2019).

20 February 2019, 14:00