Tafuta

Vatican News
Askofu Mkuu José Domingo Ulloa Mendieta wa Jimbo Kuu Katoliki la Panama na vijana wote wa Amerika ya Kati wako tayari kuwapokea vijana toka pande zote za dunia Askofu Mkuu José Domingo Ulloa Mendieta wa Jimbo Kuu Katoliki la Panama na vijana wote wa Amerika ya Kati wako tayari kuwapokea vijana toka pande zote za dunia  (CLP)

Siku ya Vijana Panama:Papa atapyaisha Kanisa hai katika huduma

Katika mahojiano na Askofu Mkuu José Domingo Ulloa Mendieta wa Jimbo Kuu Katoliki la Panama kuhusiana na Siku ya vijana duniani inayokaribia anasema,Kanisa na jamii wanahitaji vijana.Wako tayari wanamsubiri Baba Mtakatifu wakiwa katika sala zao za kila siku na vijana wataimarishwa imani yao kwa kusikiliza kwa makini katekesi na ushauri wa Baba Mtakatifu

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Siku ya vijana huko Panama itakuwa ni fursa kwa ajili ya kufanya kile kinachonekana na ambacho ni hali halisi ya vijana, kati yao wahamiaji, watu wa asili na jumuiya za asili kutoka Afrika.  Ndiyo maneno yaliyothibitishwa siku chache kabla ya  Mkutano wa kimataifa kwa vijana,  Askofu Mkuu wa Amerika ya Kisini Jose José Domingo Ulloa Mendieta, Jimbo Kuu Katoliki la Panama anasema kwamba, Kanisa la Panama ni hali halisi inayozungumza  na yule aliye tofauti, lakini bila bila kuwa mbali, naye na linatambua kusaidia mazungumzo ya kiekuemen na kidini; kadhalika ni katika Kanisa ambalo ni huduma kwa wote bila kubagua hata mmoja.

Askofu Mkuu akifafanua kwa jinsi gani wamekujiandaa katika mkutano huo mkubwa na Baba Mtakatifu na vijana kutoka duniani kote anasema, katika maandalizi yameongozwa  hatua ya mwao na sala na na kuukabidhi mpango mzima katika mikono ya Bwana, ambapo walikuwa wakifanya sala ya pamoja kwa ajili ya Siku ya vijana kila tarehe 22 ya kila mwezi kwa karibia miaka miwili sasa. Walichagua siku hiyo kutokana na kwamba ni  Sikukuu ya Mtakatifu Yohane Paulo II aliyeanzisha Siku ya vijana duniani. Hata hivyo pia wamepata msaada wa hali ya juu kutoka katika kampuni ambayo iliendeleza mchakato kwa namna ya mtindo mwema na kuwaruhusu waweza kufuatilia hatua kwa hatua ambayo imewafikisha katika maandalizi na miongozi tofauti ya Kamati ya maandalizi mahalia ya Siku ya Vijana duniani.

Baba Mtakatifu Francisko atakuta kitu gani?

Askofu Mkuu Ulloa Mendata pia akielezea ni kitu gani Baba Mtakatifu Francisko atakuta huko, anasema kwamba atakutana na Kanisa kijana na lenye furaha, lililo wazi na kuwa na  utamaduni na makabila mengi wakati huo wakiwa na imani hai na wanaojibidisha kutangaza Injili. Kanisa ambalo halikatishi tamaa na ambalo Baba Mtakatifu Francusko alitoa jibu kwa kuandaa tukio hilo maalum, la kihistoria kama Siku ya vijana Duniani.  Ni Kanisa ambalo linathibitisha shughuli za Baba Mtakatifu Francisko kutangaza Kanisa linalotaka kutoka nchi na kutafuta wale ambao wanaishi katika pembezoni mwa jamii. Atakutana na Kanisa ambalo linazungumza na kila aliye tofauti, lakini ambalo siyo mbali na watu, bali linatambua kusaidia katika mazungumzo ya kiekumene na kidini. Kanisa ambalo linatoa huduma kwa wote bila kubagua hata mmoja.

 Siku ya vijana ni kitovu cha vijana ili kutafuta kwanza Kristo bila kusahau masuala ya uasilia na wahamiaji, lakini mantiki zake muhimu ni zipi?

Askofu Mkuu akigusia juu ya Siku ya vijana kuweka kitovu cha vijana ili kutafuta kwanza Kristo bila kusahau masuala ya ualisilia na wahamiaji, anasema Siku ya vijana ni fursa ta kuweka bayana hali halisi ya vijana kati yao na  wahamiaji, watu wa asili na jumuiya mbalimbali yenye asili ya waafrika. Haiwezekani kudharau hali halisi hizi, anabainisha na kuongeza kusema,  hata kuacha hivi hivi bila kufanya lolote. Kwa maana hiyo Askofu mkuu  anaamini kwamba mantiki ya Siku ya vijana itasaidia kuweka bayana  hali halisi, kama Kanisa la Amerika ya Kati lilivyo kwisha au kuendelea kuwasindikiza.

Matazamio ya Siku ya vijana huko Panama

Katika kufananua juu ya matazamio ya siku ya vijana  ni matumaini ya Askofu Mkuu Ulloa kuwa, siku hiyo inaweza kuleta matunda kwa idadi kubwa ya vijana wa dini ya Kanda ya Amerika ya Kati na Baraza zima la Marekani. Na kwa wale ambao hawawezi kufika wameza kufanya kila njia ya  kuhakikisha kuwa vijana wote wanaweza kufuatilia kwa njia ya mitandao ya mawasiliano. Lakini jambo la muhimu ni kwamba vijana wote waweze kumalizia mkutano wao wakiwa na utulivu na kujikita kwa kina katika kutafuta majibu na maswali yanayohusu maisha yao na kupata kujieleza katika mpango wao mzima wa maisha.

Matashi mema ya Askofu Mkuu mwa vijana na wote wa Siku ya vijana duniani

Kwa kuhitimisha mahojiano yake kuhusiana na siku hii maalum ya vijana duniani, Askofu Mkuu Ulloa anawataka vijana wapate kujiachia ili wabembelezwe na upendo na   huruma ya Baba Mungu na kuchukua fursa hii mwafaka wakati wa kusikiliza katekesi na maneno ya Baba Mtakatifu ambayo yanataka kuimarisha imani, lakini pia anawaleza kuwa Kanisa na jamii linawahitaji wao… wawe na ujasiri wa kujibu wito wa Mungu na kwa njia ya sala zao ambazo  wanawasindikiza kama mababa wachungaji.

15 January 2019, 12:55