Tafuta

Vatican News
Uchaguzi Mkuu wa Rais nchini Senegal unakaribia tarehe 24 Februari 2019, lakini kuna wasiwasi mkubwa wa ghasia na vurugu Uchaguzi Mkuu wa Rais nchini Senegal unakaribia tarehe 24 Februari 2019, lakini kuna wasiwasi mkubwa wa ghasia na vurugu  (AFP or licensors)

Senegal:Wasiwasi wa Maaskofu kuhusu ghasia za kampeni

Ikiwa inakaribia uchaguzi wa rais nchini Senegal, mivutano ya kisiasa inazidi kuongezeka kati ya Serikali na nguvu za upinzani wa kisiasa. Hali ya wasiwasi mkubwa inaoneshwa na maaskofu katika waraka wao huku wakitoa wito wa taadhali dhidi ya machafuko na ghasia hizo kwa kuzingatia mada ya Papa Francisko ya siku ya amani isemayo siasa safi ni huduma ya amani

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Maaskofu Katoliki nchini Senegali wanao wasiwasi mkubwa kuhusu hali halisi ya mivutano na ghasia zinazoendelea kwa sasa katika kampeni ya uchaguzi kwa rais unaotarajiwa kufanyika tare 24 Februari 2019. Katika waraka wao uliotolewa na vyombo vya habari tarehe 23 Januari 2019, maaskofu wanatoa wito wa kuwa na dhamiri ya maadili ya nchi ya Senegal kwa namna ya pekee kwa wadau wa kisiasa ili waweze kuwajibika katika mwendendo ambao unahakikisha kura ya uhakika, uwazo na amani.

Hakuna kufanya ghasia na kutumia nguvu

Katika wito waraka wao unaoongozwa na mada hakuna kutumia nguvu, maaskofu wa Senegal wanatoa taadhali ya kuwa makini ili kuilinda amani kijamii katika nchi na kuwatia moyo wawe na mazungumzo yanayo heshimu kwa kuepuka kile ambacho kinaweza kutoka kabla na baada ya upigwaji wa kura. Mwaliko wa maaskofu hasa unawalenga wagombea wa uchaguzi huo na kuwakumbusha maneno ya Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko wa Siku ya 52 ya Amani duniani kwamba, siasa safi ni huduma ya amani. Tabia mbovu za siasa mbaya kama vile ufisadi, kushikilia madaraka, kutafuta haki kwa njia ya vurugu, kuchochea ghasia, kukataa kulinda mazingira nyumba yetu ni vitu vinavyo dhoofisha wazo la kweli la kidemokrasia na kuweka amani ya kijamii katika hatari.

Siasa safi katika huduma ya amani na wema wa pamoja

Utajiri mkubwa wa shughuli za kisiasa, maaskofu wanasisitiza unatulia juu ya kuheshimu maisha, uhuru na hadhi ya mtu, juu ya uwajibika kwa ajili ya ustawi wa pamoja, kuhamasisha mazungumzo ya amani na ushirikiano kijamii, kuwajibika kwa ajili ya haki na kukataa kila haki ya ubaguzi kijamii. Kwa kuhitimisha waraka wao, maaskofu wa Senegal wanaeleze matashi yao mema ni kwamba viongozi wanaweza kuendesha utaratibu wao wa kazi ya upigaji kura kwa uaminifu na kuheshimu sheria ya nchi.

Maelfu ya wakaguzi wa Kanisa kusimamia uchaguzi

Katika mtazamio wa upigaji wa kura, tarehe 24 Februari, Kanisa la Senegali limeweka katika kambi maelfu ya wakagusi ili kulinda mchakato wa uchaguzi kwa namna ya kwamba matokeo yasiweze kupingwa na kukubaliwa kwa sehemu zote. Zaidi kama ilivyotekea mwaka 2012, hata kwa mara nyingine tena, Kanisa linajikita kuanzisha mambo mengi na wazalendo wake. Kwanza kampendi ya mawasiliano katika majimbo kwa njia ya kutoa habari kwa njia ya radio na kuwasaidia kuweka taarifa mbalimbali katika mabango kwenye maeneo mengi na mitaa ya watu na wagombea uchaguzi kwa mantiki zilizopendekezwa na wazalendo wenyewe na  kampeni ya mawasiliano na elimu jamii.

26 January 2019, 15:01