Cerca

Vatican News
Sanamu nyeusi ya Mnazareth wakati wa Maandamano makubwa mjini Manila, Ufilippini Sanamu nyeusi ya Mnazareth wakati wa Maandamano makubwa mjini Manila, Ufilippini 

Manila:Milioni ya waamini katika maandamano ya Mnazareti!

Ni utamaduni kwa waumini nchini Ufilippini mbao hufanya maandamano wakiwa wamebeba sanamu nyeusi ya Yesu Mnazareti. Watu wengi utembea miguu peku,wakitaka kugusa sanamu hiyo. Sanamu ya Yesu inaaminika kuwa na nguvu za uponyaji, ambapo ni milioni ya watu hufika katika maandamano kila mwaka mwezi Januari. Ni utamaduni ulioanza karne ya XVII

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Zaidi ya watu milioni moja wameudhuria katika maandamano ya kidini yanayojulikana kama Yesu mweusi Mnazareti kwa kuzungukia mji Mkuu Manila nchini Ufilippini. Watu hao walikuwa wakiimba wimbo, “Uishi Milele”! wakati huo huo kuwa na msongamano mkubwa na wengine waking’ang’ania kugusa sanamu hiyo ambayo inasadikika kuwa na nguvu ya uponyaji. Nchini Ufilipini ni miongoni mwa mataifa yaliyo na idadi kubwa ya waamini wakatoliki, kwa maana takwimu zinathibitisha kuwa nchini Ufilippini,asilimia 82% ya watu milioni 105 ni wakatoliki.

Wengi wa watu wanaamini kuwa sanamu ya Mnazareti ina nguvu ya miujiza ya uponyaji, hivyo wagonjwa hung’ang’ana ili kuhakikisha kuwa wanaigusa japokuwa kwa shida kubwa kutokana na msongamano mkubwa. Taarifa kutoka Kanisa la Ufilipini linathibitisha kuwa sherehe hizo ni moja ya maandamano ya kidini yaliyo makuu katika dunii, kwa maana hata mwaka huu zaidi ya watu milioni moja, wameweza kuwepo katika maandamano barabarani, hata kama si kugusa, lakini hata kuona sanamu hiyo ambayo ilianza utamaduni huo tangu  mwaka 1606.

Ibada ya Mnazareti siyo harara za watu bali ni upendo kwa ajili ya Yesu

Naye Kardinali Luis Antonio Tagle Askofu Mkuu wa Jimbo la Manila nchini Ufilippini, kufuatia na maadhimisho ya  Sanamu ya Yesu Mnazareth, anathibitisha kuwa ibada ya Mnazareth siyo suala la harara za watu tu, bali ni upendo kwa ajili ya Yesu. Amethibitisha hayo wakati wa kuadhimisha Misa Takatifu tarehe 9 Januari 2019 katika Kanisa la Matakatifu Yohane Mbatizaji katika mahubiri yake. Akiendelea na mahbiri yake amasema, ni ibada ya kweli ya kupenda na uwepo wa ibada kama hizo ni upendo. Harara za watu kwa kawaida ni kuparangana na kitu ambacho kinapenda kutoa thamani binafsi na kumbe mapokeo ya ibada yanapenda Yesu na siyo kujipenda binafsi. Mtu mwenye harara hana upendo wa kweli amethibitisha  Kardinali Tagle. Aidha amesema kuwa waamini wa wa Ufilippini wanajitambulisha na kujifananisha na Yesu mteswa katika misha yao yanayojikita katika umasikini na mateso ya kila siku.

Wafilippini wanajifananisha na Yesu Mnazareti katika umasikini na mateso ya kila siku

Hata hivyo msimamizi wa Kanisa la Mtakatifu Yohane Mbatizaji  katika eneo la Quaipo mjini Manila akieleza katika vyombo vya habari za Kimisionari Fides anasema Sikukuu ya Sanamu nyeusi ya Yesu Mnazareti inajikita katika  mapokeo ya Kristo wa mateso na kwamba ni kweli kama alivyosema Kardinali Tangle kuwa waamini wa huko wanajifana nisha na Yesu katika maisha yao ya umasikini na kuteseka kila siku. Katika kuhamishwa kwake mahali sanamu ilipo, maandamano hayo hudumu kwa masaa 24 huku waamini wakisindikiza sanamu hiyo kuzungukia mji mzima wa Manila wakisali na kuimba na baadaye kurudi katika mtaa wa Quiapo. Katika tukio hilo, kwa kawaida wapo mapadre wengi Kanisani wakiungamisha na kubariki visakramenti mbalimbali.

Maandamano tangu karne ya XVII

Maandamano hayo ya Sanamu nyeusi ya Yesu Mnazareti yanafanyika kila mwaka tangu karne ya XVII na ambayo yanajulikana kama uhamisho kwa maana wakati wa sherehe hizo, sanamu hiyo ushushwa chini kwa kamba na kuwekwa kwenye kifaa fulani kisichokuwa na magudumu, bali kubebwa mabegani mwa watu. Waamini ukaa karibu sana na sanamu  hiyo wakati huo huo wengine wakipanda juu ya mabega ya watu ili kuweza kugusa sanamu hiyo. Kutokana na ajali ambazo hutokea mara kwa mara wakati wa maandamano, kwa mujibu wa kikundi cha Msalaba Mwekundu nchini Ufilippini hata kwa mwaka huu 2019, kimeweza kufanya kazi kubwa sana ya kuwasaidia mamia ya watu waliokuwa wanaanguka au  kwa sababu ya kukosa hewa au kuumia miguu, lakini kwa bahati nzuri hapakutokea hajali iliyo kubwa.

Historia ya utamaduni wa Sanamu nyeusi ya Mnazareti tangu 1606

Sanamu nyeusi ya Mnazareti  ilifika nchini Ufilippini kunako  tarehe 31 Mei 1606 kwa njia ya wamisionari  wa Shirika la Wagostini, walipokanyaga mguu wao mjini Manila. Sanamu hii ilitengenezwa huko mjini Mexico na ambayo inawakilisha Mwokozi akiwa amepiga magoti chini ya uzito wa msalaba. Umaarufu wa mihujiza, metokana na historia yake kuwa moto uliounguza na kuteketeza Meli ya wamisionari na  wakati sanamu hiyo ikabaki bila kuungua. Sanamu hiyo iliwekwa katika Kanisa la Bagumbayan ambapo  leo hii Kanisa hilo linajulikana  Luneta mjini Manila kunako tarehe 10 Septemba 1606 na baadaye ikahamishiwa katika Parokia ya Mtakatifu Nicola wa Tolentina na kubaki hapo hadi mwishoni mwa mwaka 1700.

Askofu Mkuu Basilio Sancho de Santas Justa, wa Manila wa wakati ule aliomba Sanamu hiyo ihamishiwe katika Kanisa la Mtakatifu Yohane Mbatizaji huko Quiapo ambapo ilikuwa ni kituo chake cha mwisho hadi leo hii. Mapokeo ya kufanya ibada kwa ajili ya picha hiyo ilikubaliwa  na Vatican kunako mwaka 1650 wakati wa uongozi wa Papa Innocenzo X na kutambuliwa kisheria kwa jina la Sanamu nyeusi ya Yesu Manazareti. Hata Papa Pio VII, katika karne ya IX aliweza kutoa heshima ya Sanamu ya Mnazareti kwa kuruhusu rehema kamili  kwa yule anayesali kwa kina.

SANAMU YA YESU HUKO MANILA
10 January 2019, 13:15