Tafuta

Vatican News
Hija ya Maaskofu wawakilishi duniani katika nchi Takatifu kuanzia 12-17 Januari 2019 Hija ya Maaskofu wawakilishi duniani katika nchi Takatifu kuanzia 12-17 Januari 2019 

Hija ya mwaka 2019 ya maaskofu kutembelea nchi Takatifu!

Hata mwaka 2019 kama utamaduni, ratiba inaonesha tayari maandalizi ya hija ya maaskofu kutembelea nchi Takatifu kwa lengo la kuwasaidia jumuiya za kikristo katika nchi Takatifu. Hija hiyo itaanza tarehe 12 hadi 17 Januari 2019

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Toleo la mwaka 2019 kwa ajili ya hija ya mshikamano wa maaskofu kwa ajili ya nchi Takatifu mwaka huu ambayo inajikita kutazama kwa karibu wakristo wa Israeli kati ya changamoto na fursa, hija itakayoanza tarahe 12 hadi 17 Januari katika miji ya Yerusalemu, Haifa na katika baadhi ya vijiji vya Wakristo wa karibu na Yordani na Israeli. Hiki ni kikundi kilichoanzishwa mwisho wa karne ya XX kwa mwaliko wa Vatican, kwa lengo la kutaka kutembelea na kusaidia jumuiya za kikristo mahalia katika nchi Takatifu. Kikundi hiki cha Uratibu kwa ajili ya nchi Takatifu kimeundwa na maaskofu wawakilishi kutoka nchi za Bara la Ulaya nzima, Amerika ya Kaskazini na Afrika ya Kusini.

Msingi wa matendo yao unawakilishwa na mambo matatu makuu: sala, hija na utekelezaji

Katika hija yao msingi wa matendo makuu yanawakilishwa na mambo makuu matatu yaani, sala hija na utekelezaji. Maombi yanafanyika ndiyo msingi wa kila mkutano wa mwaka wakati wa kuadhimisha  ibada za misa ya kila siku na mara nyingi hufanyika katika mafungo tofauti na katika jumuiya katoliki mahalia. Hija hiyo ni moja ya kipindi mwafaka katika muungano wa mwaka kwa maaskofu kutoka pande za dunia kuwakilisha mataifa yao katika nchi hiyo Takatifu. Kwa kawaida, maaskofu wanapokuwa katika hija hiyo nchi Takatifu wanakwenda binafsi au wanakwenda kama kikundi kutembelea jumuiya katoliki mahalia na kukutana na waamini wao, wakati mwingine hata viongozi wa kisiasa mahalia. Kuhusu tendo la utekelezaji, hilo linajikita kuhakikisha shughuli ambayo inafanyika kila mara baada ya kumalizaza kwa mkutano huo wa mwaka nchi Takatifu.

Utekelezaji katika matendo ya dhati mara baada ya kurudi nchini mwao

Mara baada ya kurudi kutoka katika hija hiyo ya nchi Takatifu, maaskofu washiriki wote waanalikwa kuzungumza na serikali zao binafsi, bunge  na mabalozi wa Israeli na Palestina, pia katika vyombo vya habari juu ya masuala yanayohusu maisha ya wakristo wanapokuwa katika nchi zao. Taarifa zaidi zineeza kuwa ratiba ya mpango wa hija  mwaka huu imetangulia, hivyo itaanza hija hiyo tarehe 11 Januari 2019 kwa kuwakilishwa na tafakari  juu ya Waraka wa “Nostra Aetate” uliotolewa na Mababa wa Mtaguso mkuu wa Pili wa Vatican kuhusiana na majadiliano ya kidini. Tafakari hiyo  itatolewa na Mkuu wa Kiyahudi Daniel Sperber na baadaye wawakilishi wote watashiriki masifu ya jioni ya siku ya Jumamosi katika Sinagogi ya “Yedidya” na mara baada ya masifu itafuata chakula cha jioni katika familia za Jumuiya ya wayahudi.

Mipango na ratiba ya siku sijazo kwa mahujaji nchi Takatifu

Hata hivyo pia taarifa elekezi inaonesha juu ya kile kitakacho endelea katika siku zijazo wakati wa kufanyika hija hiyo kwamba, kutakuwa na mkutano kati ya Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa msimamizi wa kitume wa Upatriaki wa Kalatino huko Yerusalamu, Balozi wa Vatican nchini Israeli na Ciprus na wawakilishi wa kitume  wa Yerusalemu na Palestina, Mkuu Askofu Leopoldo Girelli, pamoja na viongozi wa makundi ya kidini kama vile wa drusi, kiyahudi na bahai. Uwakilishi wa maaskofu watakwenda pia katika vituo vya Zababdeh, Jenin, Ikrit, Miilya, watakutana na wanafunzi wa shule za wakristo wa Haifa na kuwatembelea watoto walemavu katika Kituo cha Moyo Mtakatifu, pia kuwatembelea wagonjwa katika Hopitali ya Kiitaliano, vituo vyote hivyo viwili viko huko Haifa. Hija yao rasmi inatarajiwa kufungwa tarehe 16 Januari 2019 mchana.

Kwanini Waraka wa Nostra Aetate?

Waraka wa Nostra Aetate wa Mababa wa Mgaguso Mkuu wa Pili wa Vatican uliochapishwa unahusu majadiliano ya kidini na hasa katika ibara yake ya nne inajikita hasa kufafanua juu ya majadiliano ya kidini  na kwa ujumla kati ya Wayahudi na Wakristo. Katika waraka huu pia unaangalia pamoja na mambo mengine hali ya majadiliano ya kitaalimungu kati ya Wayahudi na Wakristo. Ufunuo wa Mungu katika historia kama “Neno la Mungu linalojifunua katika Mapokeo ya Wayahudi na Wakristo. Yapo mahusino ya  pekee kati ya Agano la Kale na Agano Jipya. Katika waraka huo unakazia umuhimu wa wokovu kwa watu wote unaoletwa na Kristo Yesu na kwamba, Agano Kati ya Mungu na Waisraeli bado linaendelea tangu wakati ule. Kwa maana katika kuutafakari, ni kutaka kuendeleza kwa dhati uhusiano huo wa mababa wa Mtaguso wa Pili wa Vatican.

HIJA NCHI TAKATIFU

 

09 January 2019, 13:41