Tafuta

Malaika aliwatangazia wachungaji habari njema na kuwaambia wasiogope! Malaika aliwatangazia wachungaji habari njema na kuwaambia wasiogope! 

Ujumbe wa Noeli kutoka Shirikisho la Kiluteri duniani:msiogope!

Ujumbe wa Sikukuu ya kuzaliwa kwa Bwana 2019 uliotiwa saini na Rais wa Shirikisho la Kiluteri, Askofu Mkuu Panti Filibus Musa, mzaliwa wa nchi ya Nigeria, unaanza na tamko la Malaika alipowatangazia wachungaji kuwa wasiogope kwa maana anawaletea habari njema ya furaha. Hiyo ni kutaka kuhamasisha juu ya kupokea wageni wahamiaji bila hofu

Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote; maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana. Ni katika mwanzo wa Ujumbe wa Sikukuu ya Kuzaliwa kwa Bwana kutoka Shirikisho la Kiangilikani Duniani. Ni ujumbe uliotiwa saini na Rais wake, Askofu Mkuu Panti Filibus Musa mzaliwa wa nchi ya Nigeria. Katika ujumbe huo, Askofu Mkuu wa kianglikani ametazama kwa karibu juu ya sentensi iliyotamkwa na Malaika akiwaambia wachungaji kuwa: “Msiogope”, kwa kutaka kusisitizia jinsi gani hofu inaweza kusababisha madhara makubwa, ukosefu wa kuwa na maana, kuwa na hukumu na zaidi ubaguzi kwa wengine.

Jumuiya nyingi nchini Nigeria zimekuwa na hofu kubwa hasa katika makabila na dini

Akiendelea katika kufafanua ujumbe wake juu ya hofu, Askofu Mkuu wa Kianglikani anasema kuwa: Hofu ni kizingiti cha kukaribisha, kupokea na kutovumilia. Hofu husababisha wasiwasi na inaweza kumfanya mtu binafsi au jumuiya kupoteza maana ya habari njema. Hofu kwa dhati umetengenisha watu na jumuiya nzima. Akitoa mfano wa nchi yake binafsi anasema: “Kwa bahati mbaya, katika baadhi ya Kanda za nchi yangu, Nigeria, Jumuiya nyingi zimekuwa na hofu kubwa hasa katika makabila na dini, ambapo kila mmoja sasa anaogopa mwingine au kumkaribisha mwingine”. Kadhalika anasisitiza: “Nchini Nigeria, kwa dhati wanaishi kipeo cha hali mbaya ya ukosefu wa msimamo kutokana na vurugu na udhaifu wa kiuchumi. Kipeo cha wakimbizi sasa kimefikia mwaka wa tano na kuzidi kuongezeka idadi kubwa ya janga la kweli kibinadamu”.

Kwa mujibu wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya wakimbizi

Kwa mujibu wa Tume ya ngazi ya  Juu ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya wakimbizi, inathibitisha kuwa ni watu 1.700.000 wa Nigeria ambao wamerundikana na kwa maana hiyo anaongeza kusema: “ Tunapaswa kushinda woga tulio nao mbele ya wengine na kufanya uzoefu wa kweli wa utulivu ambao unaweza kuoneshwa na jamii nzima kwa ujumla. Aidha anaongeza kusisitiza kuwa: “hatuweza kuruhusu kukumbwa na hofu ya namna hii  ya kukatisha uwepo wa amani ambao ni wa kibinadamu, hasa katika dunia ambapo katika historia ya kijiografia kamwe hakuna ubaguzi wala utengeno. Askofu Mkuu Panti Filibus Musa wa Kianglikani, katika ujumbe anaandika: “Makaribisho yetu kwa wale ambao ni wageni kutoka sehemu nyingine za kanda na utamaduni tofauti, yanaweza kuaminiwa tu iwapo sisi tutaondoa hofu zetu.   Habari njema ya Yesu Kristo inaweza kupokelewa kiukweli, iwapo tunaweza kushinda hofu na kuwapokea wengine”.

Habari njema itusaidie kuwajibika katika huduma ya kibinadamu

Habari njema inapaswa itusaidie kuwajibika zaidi katika huduma ya kibinadamu. Na zaidi iwapo tunataka kuwa wapashanaji habari hii njema ni lazima kujinasua dhidi ya hofu na kukabiliana na hatari. Hakuna haja ya kuogopa kukabiliana na changamoto kwa kutumia majengo na mifumo ambayo inawezesha kwa dhati kukamilisha maisha ya kuwa binadamu kwa wote. Kutokana na hilo, ndipo Askofu Mkuu anatoa wito ili kila mmoja anayejikita katika matendo ya kila siku kwa upande wa sekta hiyo awajibike na atumie haki ya kweli, amani njema na uvumilivu wa kwa ujumla.

20 December 2018, 16:19