Tafuta

Vatican News
Kama Yesu alivyozaliwa masikini hata Noeli inatualika kuwa na umakini zaidi kwa ajili ya masikini Kama Yesu alivyozaliwa masikini hata Noeli inatualika kuwa na umakini zaidi kwa ajili ya masikini  (@Vatican Media)

Sri Lanka:Maaskofu wanatoa wito wa kuadhimisha upendo na masikini!

Maendeleo ya kibinadamu yanawezekana tu iwapo jamii inajikita katika kuheshimu,kuwa na haki pia amani.Ndiyo maneno muhimu yanayosikika katika ujumbe wa Sikukuu ya Noeli 2018 kutoka Baraza la Maaskofu katoliki nchini Sri Lanka

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katika maadhimisho ya Noeli 2018, maaskofu katoliki nchini Sri Lanka, wameaalika waamini wote na wenye mapenzi mema kuadhimisha Noeli ya upendo kwa ajili ya maskini. Katika ujumbe wao uliotolewa katika fursaya sikukuu, wanatoa ushauri kwa waamini wote kwa kusema: “Tujibidishe kuwa wadau wa amani, umoja na mapatano, kuachilia mbali mambo yasiyo ya msingi yenye utofauti wa kuzuia wema wa pamoja”. Kadhalika wanaongeza kuandikika: Sote tunao uwajibu wa kuguswa zaidi mbele ya mahitaji ya binadamu na mateso yaliyo ndani ya nchi yetu”.

Maendeleo yanawezekana tu kwa kuheshumu, haki na amani

Maaskofu wa Sri Lanka wanaendelea na kuashauru kuwa: “ Kama Yesu alivyozaliwa maskini hata Noeli inatualika kuwa na umakini zaidi kwa ajili ya maskini duniani. Matatizo ya umaskini yanaweza kupata suluhisho iwapo tutajikita katika kuunda mifumo ya kiuchumi iliyo na usawa”. Kwa mujibu wa maaskofu wanasema, “maendeleo ya mwanadamu, yanawezekana tu, katika jumuiya inayojikita katika heshima ya pamoja, haki na amani. Ni lazima kuwa na uwajibu wa dhati kwa upande wa wote ili kuunda mazingira ya nchi yetu”.

Kulinda kazi ya uumbaji

Maaskofu kadhalika wanatoa wito wa kuunda jamii inayoheshimu mazingira na kugundua unyenyekevu kuwa ni  asili ya Noeli ambayo inashirikisha hata wakristo wa Sanjeewa Indrajith, ambao ni wajumbe wa upyaisho wa utume. Na kwa maana hiyo maaskofu anawakumbusha kwa namna  gani ambayo Kristo alikuja ulimwenguni. Ni katika holi la wanyama, akiwa amezungukwa na ng’ombe na kondoo, wakati huo huo  akapokea zawadi zilizoletwa na Mamajusi. Kwa njia hiyo ni lazima wahamasishe Noeli ya urafiki wa kiekolojia,  na ndipo wataweza watagundua kuwa Kristo  amezaliwa katikati ya asili.  Kiongozi wa Dini ya Sanjeewa Indrajith, analinganisha picha ya nyumba ya wageni mahali ambapo Maria na Yosefu walikuwa wanatafuta mahali pa kujifungulia mtoto na holi la wanyama alipozaliwa Yesu.  Yeye anafafanua na ksema kuwa: Nyumba ya wageni ni ishara ya kutumia hovyo, ya utamaduni wa ubaguzi, hushindani, uhuru wa masoko. Wakati  holi la wanyama  kinyume chake ni ishara ya urahisi, utulivu, upole, utunzaji, upendo na roho ya umoja.

Hakuna kutumia hovyo

Katika ujumbe wao, Maskofu wa Sri Lanka pia wanasimulia kazi ya uumbaji kwa mujibu wa Bibilia, kitabu cha Mwanzo, mahali ambapo Mungu anapumzika na kutafakari kile alichokiumba na “kuona kila kitu kilikuwa chema”( Mw 1,16-19). Na hatimaye, wanasisitiza kwamba: “tuachilie mbali nyumba ya wageni iliyojaa mambo mengi ya kutumia na ili kuweza kutawaliwa na holi, ambalo ni ishara ya urahisi, mtinfo wa maisha mema, utunzaji na upendo.

 

26 December 2018, 14:55