Tafuta

Vatican News
Askofu Mkuu Jean-Claude Hollerich S.J. anawatakia ufanisi wa Makubalinao ya Mkakati wa kimataifa kuhusu uhamiaji salama utakaidhinisha rasmi tarehe 11 Desemba nchini Morocco Askofu Mkuu Jean-Claude Hollerich S.J. anawatakia ufanisi wa Makubalinao ya Mkakati wa kimataifa kuhusu uhamiaji salama utakaidhinisha rasmi tarehe 11 Desemba nchini Morocco  

Comece:Global Compact kuhusu uhamiaji,uwe na ufanisi wa ubinadamu fungamani!

Ujumbe wa Rais wa Tume ya Mabaraza ya maaskofu wa Umoja wa nchi za Ulaya (comece), Askofu Mkuu Jean-Claude Hollerich, kuhusu tafakari ya Kanisa katika Mkataba wa Global Compact unaohusu uhamiaji salama na wa mpangilio katika kilele cha kupitishwa rasmi tarehe 11 Desemba huko Marrakesh Morocco

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Makubaliano ya Mkakati wa kimataifa kuhusu uhamiaji salama na wa mpangilio (Global Compact) utapitishwa rasmi na nchi wanachama, kwenye mkutano wa kuidhinisha mfumo wa uhamiaji wa kimataifa, utakaofanyika huko Marrakesh, Morocco, tarehe 10-11 Desemba 2018.  Mkakati huo wa kimataifa ni mjumuisho  wa majadiliano na mashauriano kati ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na watendaji kama vile viongozi wa ngazi za kijamii, wawakilishi wa asasi za kiraia na wahamiaji wenyewe. Kwa jumla, mchakato huu wa wazi na jumuishi ni ambao umefanya michakato mingi na kuwepo kwa majadiliano mengi na kujifunza kutola kwa washiriki wote kuhusu hali halisi ya uhamiaji wa kimataifa. Mwafaka huo sasa unaunda msingi wa kuboresha utawala na uelewa wa uhamiaji wa kimataifa, kukabiliana na changamoto za sasa zinazohusiana na uhamiaji, na kuimarisha mchango wa wahamiaji na uhamiaji kwenye maendeleo endelev.

Usalama wa wahamiaji na jamii

Kutokana matarajio ya kupitishwa rasmi, taarifa kutoka kwa upande wa Kanisa Katoliki katika Makubaliano ya Umoja wa Mataifa, Askofu Mkuu Jean-Claude Hollerich, Lussemburgo  Rais wa Tume ya Baraza la Maaskofu Ulaya (Comece,) anathibitisha kuwa, Hati hiyo ni tunda la michakato mipana ambayo inatazama kwa hakika kutoa usalama na ulinzi wa watu wahamiaji na jumuiya zote zinazowakaribisha kwa kuhamasisha michakato ya uhamiaji halali  ili kuzuia hali halisi ya biashara ya binadamu, safari hatarishi, kutengenishwa kwa familia na vurugu.

Watu wenye uso na hadhi

Kwa kutumia maneno ya Baba Mtakatifu Francisko, Askofu Mkuu anasema Kanisa Katoliki barani Ulaya inathibitisha kuwa uwajibikaji wa pamoja wa kupokea, kulinda, kuhamasisha na kushirikisha,wahamiaji na wakimbizi katika jiamii  ndani ya Bara zima. Na hiyo ndiyo kila kitu kwani hao ni watu ambao wana sura, na historia zao binafai, na wanastahili kuwa kuheshimiwa, hadi tao na haki zao msingi.

Katika pendekezo hili, misingi ya binadamu na mahitaji yake halisi,na wema wa pamoja vinapaswa kuzingatiwa katika siasa za ndani na nje ya Umoja wa Ulaya na mataifa wanachama   hata masuala ya uhamiaji. Baraza la maaskofu wa Ulaya wanawatia moyo hata viongozi  wa kisiasa kitaifa kwa mujibu wa maneno ya Papa Francisko ili kueneza uwajibikaji na utekelezaji wa pamoja katika kushirikisha wahamiaji kitaifa kwa dhamana ya  haki, mshikamano na uwelewa. Na hatimaye wanatia moyo mataifa wanachama wote wa Umoja wa Mataifa katika Global Compact  na ili iweze kweli kuwa na ufanisi kwa ajili ya ustawi wa binadamu wote na katika kushirikishana.

Uhamiaji unaibua masuala mengi muhimu, kuhusu uhuru wa nchi na haki za binadamu

Ikumbukwe ilikuwa tarehe 13 Julai 2018 ambapo Mkakati wa kimataifa kuhusu uhamiaji salama  na wa mpangilio ulikamilishwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani. Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kushikamana kwa pamoja ili kujadili makubaliano yatakayozingatia nyanja zote za uhamiaji wa kimataifa kikamilifu na kwa kina. Akitoa sauti yake kuhusu mkakati huo, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed, wakati wa mkutano huo alisema: “Uhamiaji unaibua masuala mengi muhimu, kuhusu uhuru wa nchi na haki za binadamu, uhusiano baina ya maendeleo na uhamiaji ma jinsi gani yakuunga mkono ushirikiano wa kijamii. Mkakati huu unaonesha uwezekano wa utawala wa kimataifa, uwezo wetu wa kuja pamoja katika masuala yanayohitaji mshikamano wa kimataifa licha ya utata na changamoto zake".

Tume ya Mabaraza ya maaskofu wa Jumuiya ya nchi za Ulaya (Comece)

Tume ya Mabaraza ya maaskofu wa Jumuiya ya nchi za Ulaya inaundwa na maaskofu wawakilishi wa mabaraza ishirini na sita ya Mbaraza ya Maaskofu Katoliki katika Umoja wa Ulaya. Ofisi ya sekretarieti ya kudumu iko huko mjini Bruxelles.  Iliundwa kunako tarehe 3 Machi 1980 na ambayo ilianza kutoa huduma katika masuala ya habari za kichungaji katika Ulaya tangia (SIPECA,1976-1980). Majadiliano yaliyofanywa kunako 1970 juu ya kuundwa chombo cha uwakilishi kati ya mabaraza la Maaskofu na Jumuiya ya Ulaya ilipelekea maamuzi, hadi kufikia mkesha wa uchaguz wa Bunge la Ulaya kunako mwaka 1979 na ndipo ikazaliwa Tume ya Mabaraza ya maaskofu wa Jumuiya ya nchi za Ulaya (COMECE).

04 December 2018, 15:22