Cerca

Vatican News
Dharura ya wahamiaji duniani ni sababu ya mateso ya wote kwa maana kila mmoja anastahili hadhi yake Dharura ya wahamiaji duniani ni sababu ya mateso ya wote kwa maana kila mmoja anastahili hadhi yake 

Maaskofu Afrika Kaskazini:dharura ya wahamiaji sababu ya mateso!

“Dharura ya wahamiaji inazidi kuongezeka duniani kote na inabaki kuwa sababu msingi za mateso ambayo tunashirikishana katika nchi zetu”. Ndiyo kitovu kilichoguswa katika Mkutano Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanda ya Kaskazini mwa Afrika (Cerna) ambao waliungana pamoja kuanzia tarehe 23-26 Septemba 2018 mjini Tangeri, Morocco

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Mkutano Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanda ya Kaskazini mwa Afrika (Cerna) walioungana pamoja kuanzia tarehe 23-26 Septemba 2018 mjini Tangeri nchini Morocco. Pamoja na mengi waliyoweka mezani, ni matukio ya uhamiaji ambao unazidi kuongezeka duniani, ambapo maaskofu wanakiri kuwa, ndiyo suala msingi na sababu ya kuendelea na mateso ambayo wanashirikishana katika nchi zao. Kwa mujibu wa taarifa yao kutoka katika ujumbe wao wa mwisho wa kazi ya mkutano huo wanasema “ uhamiaji unawekwa katika kiini cha mjadala wa mshikamano wetu na wale ambao wanateseka kwa maana pana, ikiwa ni  heshima ambayo kila mmoja aliye binadamu  na kila hali yake anastahili”.

Ziara ya wawakilishi wa Baraza la Maaskofu Italia Cei

Katika Mkutano wao mkuu wa Baraza la Maskofu wa Kanda ya Kaskazini mwa Afrika, kama ishara ya ukaribu na mshikamano, uliudhuriwa pia na wawakilishi ambao waliongozwa na Tume ya Baraza la Maaskofu ya Italia kwa upande wa wahamiaji na Chama cha Migrantes, Askofu Guerino Di Tora na Padre Giovanni De Robertis, lakini pia alikuwapo hata Kardinali Franceso Montenegro, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Agrigento kisiwani Sicilia na Rais wa Caritas nchini Italia.

Uhuru wa dini Afrika Kaskazini

Mada kuhusu uhuru wa dini pia ilikuwa fundo msingi lililokabiliwa kwa kina katika mchakato wa mkutano huo. Katika waraka wao wanaandika: “ maendeleo ya jamii Afrika ya Kaskazini daima imekuwa ni mapambania zaidi juu ya kutambuliwa kwa wingi wa dini na uhuru wa dhamiri”. Kutokna na hilo, ndipo Baraza la Maaskofu wa Afrika ya kaskazini (Cerna) wanatoa mwaliko wa dhati kwa jumuiya nzima kupokea changamoto ya kitasaufi ya makutano ya kidini,  Maaskofu wanaandika,“ katika ukuu wake na kwa namna ya pekee katika kukutana na Mungu”.

Kutangazwa kwa wafia dini wa Argeria mwezi Desemba

Hatimaye katika waraka wao wa mwisho, wa Baraza la Maaskofu wa Afrika ya Kaskazini (Cerna, wanaonesha pia, “ furaha kubwa ya Makanisa kutokana na kwamba tarehe 8 Desemba kutangazwa kwa wafiadini huko Orano, kwa Askofu Pierre Claverie na wenzake 18 waliouwawa nchini Algeria kati ya mwaka 1994 na 1996. Hawa ni waathirika wa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vimekatisha nchi ya Afrika ya Kaskazini wakati wa migogoro kati ya waislam mbele  ya wokovu wa kiislam na majeshi ya nchi ya Algeria. Ni vurugu iliyowakumba wanazalendo wa Algeria na matukio hayo kujionesha zaidi katika mashaidi 7 watawa kutoka shirika la Trapisti kwenye Monasteri ya Tibhirne, pamoja na Mkuu wao wa shirika Padre Christian De Chergé waliotekwa nyara na kuwawa, lakini hadi sasa bila kujua ni kwa jinsi gani.

 

 

01 October 2018, 10:33