Tafuta

Vatican News
Wiki ya kuadhimisha Hija ya wafiadini nchini  Korea Kusini Wiki ya kuadhimisha Hija ya wafiadini nchini Korea Kusini 

Wiki ya kuadhimisha usimamizi wa wafiadini Korea ya Kusini!

Safari ya hija katika jimbo kuu la Seoul katika nyayo za wafiadini wa Korea inatambuliwa rasmi na Vatican kama Hija ya Kimataifa. Hija hiyo imeanza Septemba 10 na itahitimishwa tarehe 15 Septemba 2018.

Frt Titus Kimario - Vatican

Kuanzia tarehe 10 hadi 15 Septemba ni wiki ya matukio yanayoendelea kusherehekea safari za hija huko Seoul inayounganisha makanisa yaliyo chini ya usimamizi wa wafiadini wa Kikorea na maeneo ya mauaji katika mji mkuu wa Korea Kusini.

Safari ya hija katika jimbo kuu la Seoul katika nyayo za wafiadini  wa Korea itatambuliwa rasmi na Vatican kama “Hija ya Kimataifa”. Sherehe hiyo ya utambulisho, linaeleza shirika la habari  za kimisionari Fides kwamba zitafanyika tarehe 14 Septemba kwa uwepo wa Kardinali Andrew Yeom Soo-Jung, askofu mkuu wa Seoul, Askofu Rino Fisichela ambaye ni Rais wa Baraza la Kipapa la uinjilishaji mpya; kadhalika Atakuwepo pia Balozi wa Vatican nchini  Korea ya Kusini, Askofu Mkuu Afreld Xuereb, pamoja na viongozi wengine katoliki  wa Asia wapatao 30 kutoka mataifa 13 na vijana 30 wakatoliki kutoka mataifa 9.

Huo ni  mpango uliobuniwa na Jimbo Kuu kunako mwaka 2013 katika mazingira ya “Mwezi wa Mashahidi” ambao uadhimishwa kila mwaka mwezi septemba na Kanisa la Korea ikiwa na lengo la kuwafanya waumini wajue zaidi historia ya wale waliojitoa sadaka maisha yao kwa ajili ya imani nchini Korea. Kati  wafia dinia hao  yumo Andrea Kim Taegon, Paolo Chong Hasang pamoja na wenzao  101 ambao walitangzwa kuwa watakatifu kunako mwaka 1984 huko Seoul na Baba Mtakatifu wakati huo Mtakatifu Yohane Paolo II. Paolo Yun Jinchung pamoja na wenzake 123 walitangazwa wenye heri na Baba Mtakatifu Francisko tarehe 16 Agosti 2014 katika ziara yake ya kitume nchini Korea na katika siku ya vijana barani  Asia.

Ni njia tatu zinapendekezwa kwa mahujaji, kwanza “Njia ya Habari njema”, pili “Njia ya Uzima wa milele” na ya tatu  “Njia ya Umoja”. Katika tukio hilo muhimu pia yatafunguliwa rasmi Madhabahu ya kihistoria ya Mashahidi huko Seosomun”ambayo ni  moja ya maeneo muhimu zaidi ya wafiadini. Kadhalika wameandaa Kongamano la kimataifa tarehe 13 Septemba 2018 linaoongozwa na  mada ya  “Utamaduni wa Asia na Ukristo” na  ili kuimarisha uwepo wa imani ya kikristo Korea, China na Malaysia

13 September 2018, 09:29