Tafuta

Vatican News
Uwanja wa  Armerina - Sicilia Uwanja wa Armerina - Sicilia 

Watu wa Armerina wamsumbiri Papa Francisko kwa hamu kubwa!

Tarehe 15 Septemba, Baba Mtakatifu anafanya Ziara yake ya kitume huko Armerina kisiwani Sicilia. Watu wa Armerina wanamsibiri kwa hamu, wakati wakifanya tafakari juu ya Wosia wake wa Furahini na Shangilieni na pia sala na mikesha kwa mujibu wa maelezo kutoka kwa Askofu Rosario Gisana

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Ni hamu kubwa ambayo watu wa maeneo ya Armerina mjini Palermo wanamsubiri kwa mara ya kwanza katikati ya Kisiwa cha Sicilia, mahali ambapo jimbo hilo ni  kubwa hadi kufikia katika Wilaya za Enna na Caltanisetta. Ni eneo ambalo wanaishi wakazi zaidi ya laki mbili, na mahali ambapo Mji wa Gela ndiyo unakaa wakazi wengi zaidi.

Ni moyo katika kiwanda kilichokuwapo cha Petroli ya Eni, kilicho anzishwa kunako mwaka 1963 kwa utashi wa Enrico Mateti na kufungwa mnamo mwaka 2014 , ambapo kwa sasa wanaendesha mradi wa  (biorefinery) yaani ni kituo ambacho kinaunganisha mchakato wa kubadilisha kwa majani na vifaa vya kuzalisha mafuta, nguvu, joto, na kemikali za thamani kutoka katika mabaki hayo ya asili, lakini  wakati huo huo matatizo ya ukosefu wa ajira ni mkubwa katika eneo lote hilo.

Kusubiri: Ni miezi sasa wamini wanajiandaa kumopkea Baba Mtakatifu Francisko, kwa sala, mikesha, hata mkesha wa mwisho utafanyika usiku wa Ijumaa 14 septemba kuamkia Jumamosi 15 Septemba. Ni Mkutano mkubwa ambao utakuwa na fursa ya sikukuu katika kipindi cha tafakari ya Wosia wa Kitume wa Gaudetr et Exsultate, yaani Furahini na Shangilieni.

Kukutana na waamini: Baba Mtakatifu anatafika kisiwani huko majira ya asubuhi na Helkopta katika Uwanja wa Mchezo wa Armerina,  mahali ambapo atapokelewa na Askofu  Rosario Gisana wa jimbo hilo, MKuu wa Wilaya ya Enna, Bi Rita Leonardi, Meya wa Mji Bwana Filippo Miroddi na baadaye saa tatu hivi  masaa ya Ulaya, Baba Mtakatifu Francisko atakutana na Waamini katika Uwanja wa Ulaya. Mkutano unaotarajiwa kudumu karibu saa moja na baadaye Baba Mtakatifu atakwenda Palermo, ikiwa ndiyo hatua yake ya pili ya Ziara yake Kisiwani Sicilia.

Ziara ambayo ni tukio kubwa: Naye Askofu Gisana akielezea juu ya tukio la Ziara ya Papa Francisko anasema, ilikuwa haitarajiwi. Ina maana kubwa na kwa ngazi ya  juu kwani, kwa mara nyingine tena, Papa anataka kuthibitisha kile ambacho alikionesha tangu kuazan utume wake kama kharifa wa mtume Petro, hasa umakini kwa ajili ya watu  maskini  na pembezoni mwa jamii. 

Katikati ya Sicilia: Pamoja na kwamba pale ni katikati ya kisiwa cha Sicilia, lakini ni pembezoni kwa sababu wanaishi kipindi cha msongo kwa namna ya pekee. Eneo hili ni tajiri lenye rasilimali, lakini watu wanaogopa kujikimu wenyewe  , wanaogopa kuunda viwanda vya ujasiliamali, ili kuweza kushinda mitindo hiyo ya umasikini ambayo ni zaidi ya uchumi wa kawaida.  Kwa maana hiyo Askofu anaongeza kuwa, anaamini kwamba hiyo ndiyo sababu ya Baba Mtakatifu Francisko kuhisi utashi huo wa kufanya ziara yake kwa hakika ambayo ni kilelezo cha ubaba wake kwa watu.

Baba Mtakatifu anakwenda kukutana na watu ili nao  wahisi ukaribu wake. Jumuiya yao imejiandaa kikamilifu kwa sala na mikesha katika kusubiri siku hiyo. Kwa maana hiyo Askofu anathibitisha kwamba siku hiyo itakuwa ya kumwonesha kwa dhati juu ya udhati wa kufuata mafundisho yake ambayo yanaelekeza na kutoa mpango wake wa maisha kwa watu wote!

 

 

 

13 September 2018, 15:59