Cerca

Vatican News
Maaskofu wa Congo wametoa onyo kali kwa wananchi wasifiche wagonjwa wa Ebola Maaskofu wa Congo wametoa onyo kali kwa wananchi wasifiche wagonjwa wa Ebola   (AFP or licensors)

Congo DRC: Hacheni kuficha wagonjwa maana ni mbaya sana!

Askofu Melkisedeki Sikuli Paluku wa Jimbo wa Butembo – Beni, wakati alipotembelea eneo la Mangina ambako janga la Ebola limeibuka na kuathiri eneo hilo la mashariki ya Congo. Wakati wa kuzungumza nao ametoa onyo kali kwa wananachi wanaoficha wagonjwa kwa maana ni mbaya sana

Frt Titus Kimario  Vatican

Inafaa kuacha mara moja kuwaficha wagonjwa maana ni mbaya sana. Hakuna sababu yeyote ya kuwaficha wagonjwa hususani katika eneo hili ambapo wanaweza kusaidiwa kwa muda. Watu hawapaswi kuwa waoga na hawatakiwi kutishwa na maneno kutoka kwa dini fulani yenye kujitengeneza ambayo husababisha baadhi ya wagonjwa kutokupokea matibabu muhimu. Hayo yamesemwa na Askofu Melkisedeki Sikuli Paluku wa Jimbo  wa Butembo – Beni, wakati  alipotembelea eneo la Mangina ambako janga la Ebola limeibuka na kuathiri eneo hilo la mashariki ya Congo.

Baadhi ya wachungaji wa madhehebu mengine  wamewapumbaza watu na kuwajengea wazo kwamba janga hilo ni "bahati mbaya". "Hawa ni wachungaji wa uongo", alisema askofu Sikuli Paluku. Na kuendelea kufafanua kwamba “Hatupaswi kuchanganya dini na matatizo ya kitabibu”. Tarehe 1 Agosti katika mkoa wa Kivu kaskazini, mamlaka ya afya ilitangaza rasmi kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola, ambapo wiki moja baada ya mwisho wa janga la awali katika mwisho mwingine wa nchi, katika jimbo la Equateur ambalo lilikuwa na jumla ya vifo 33.

Programu ya lishe duniani (PAM) ilituma vyakula kwa ajili ya wagonjwa na wafanyakazi wa afya katika miji ya Beni na Mangina. chakula pia hutolewa kwa vijiji katika maeneo yaliyoathiriwa na janga hilo, "aliongeza PAM, ambaye anafanya kazi kwa kushirikiana na caritas internationalis, Kivu kaskazini ni moja ya majimbo ya Kongo yenye idadi kubwa zaidi ya watu waliokimbia makazi yao, kwa sababu ya unyanyasaji na uwepo wa askari kadhaa ambao wamekuwa wakishambulia raia kwa miongo miwili.

 

06 September 2018, 09:04