Tafuta

Vatican News
Askofu wa kwanza mzaliwa  Gjergj Meta wa jimbo la Rreshen nchini Albania Askofu wa kwanza mzaliwa Gjergj Meta wa jimbo la Rreshen nchini Albania  (Stefano Guidoni)

Albania:Usiogope zizi dogo hata katika uchache na umaskini!

Katika miezi hii kumi na mbili, anaandika Askofu Meta wa Albania kuwa amepata fursa ya kutembelea vijiji mbalimba na kukutana na watu wengi, na hata kwenda katika sehemu za maeneo ya Kanisa mahalia. Anawatia moyo ili kubadilika kwa sababu ya kupyaisha kazi ya utume wa kiinjili katika nchi yao

Sr. Angela Rwezaula - Vatican 

Inahitimishwa kwa  namna hiyo mwaliko wa matumaini katika barua ya pili ya kichungaji wa Askofu Gjergj Meta, wa Jimbo la Rrëshen nchini Albania aliyo ikabidhi tarehe 2 Septemba  katika maeneo yote ya majimbo  akiwa amehitimisha mwaka mmoja tangu kuanza  shughuli ya kichungaji kama Askofu wa kwanza kijana mzaliwa katika nchi hiyo.

Katika miezi hii kumi na mbili, anaongeza Askofu Meta, kwamba amepata fursa ya kutembelea vijiji mbalimba na kukutana na watu wengi, na hata kwenda katika sehemu za maeneo ya Kanisa mahalia. Kila sehemu amekutana na Mungu na baraka yake ambayo haikuondolewa kwa watu hao. Mimi sikuwapelekea kitu kipya, badala yake nimepokea kitu ambacho kinaendela kunibadili maisha yangu kila siku, anathibitisha katika barua yake.

Huo ni uongovu wa kweli na wa dhati: Na hiyo ndiyo roho ambayo leo hii ninapenda kukabidhi mchakato kwa wote, maaskofu, mapadre, watawa kike na kiume na walei wote kuhusika.  Akitaka kuanza kuangazia juu ya shughuli nyeti ya kichungaji anasema kuwa kuna tendo la nguvu ambalo linaonekajana kutaka kubobea katika malimwengu. Kwa maana hiyo ni lazima kuwa na mapinduzi ili Kanisa lipate kujibu hali halisi ya kuunda  kwa upya kipindi cha sasa.

Na hiyo ni operesheni ngumu, nyeti, lakini ni ya lazima na iwe hai, katika kutangaza leo hii Injili ya furaha. Anaandika pia kwamba wataanza na baadhi ya mambo ambayo yanonekana kuwa rahisi, lakini ambayuo yanajenga mwanzo wa mchakato. Hawali ya yote ni sala, kwa sababu ni jumuiya ambayo inasali, na kuishi liturujia, kwa ibada na kujikita kwa kina, kuzungumza zaidi ya kila aina ya mchakato. Baadaye yatafuta Mafundisho, ya kweli katika jimbo lao. Na ndipo hiyo inahitaji kujikita kila jumamosi ya mwezi kwa ajili ya leongo hilo.

Uwepo wa mapadre na watawa ni wa lazima, anasisitiza Askofu na kuelezea kwamba sehemu ya kwanza ya mwaka wa kichungaji utajikita katika mafundisho ya Waraka wa Mtaguso wa Pili wa Vatican, na wakati sehemu ya pili ya mwaka, kuanzia Januari hadi Juni, watajikita katika Mafundisho ya shughuli za uongozi wa jumuiya kwa mtazamao  Evangelii Nuntiandi, Yaani waraka wa Papa Paulo VI kuhusu  juhudi ya kutangza Injili kwa watu wa nyakati zetu, wakiongozwa na matumaini. Lakini ambayo daima yanakatishwa na hofu , na uchungu, wakati huo huo  bila kuwa na wasi wasi, ni huduma ambayo si tu kwa ajili ya jumuiya ndogo bali hata kwa binadamu wote, kadhalika watajikita pia katika Waraka wa hivi karibuni wa  Evangelii Gaudium  yaani Injili ya Furaha wa Papa Francisko. Kwa njia hiyo anasema “inawezekana kujenga Kanisa la kimisionari, mahali ambapo wote wanaalikwa  kutanza Injili. Na zaidi: ni muhimu wa wahusika wa kchgungaji kuwa na msiamamo na kusaidia Askofu kwa ngazi ya kichungaji, lakini pia kufanya kazi kwa uwazi na kukomaa kwa sekta mbalimbali.

Na hatimaye Askofu hakukosa kusema juu ya matatizo ya miitomya mapadre ambayo kwa upande wa Kanisa la Albania ni kubwa kiasi:Askofu anaandika kuwa hili siyo wasiwasi mkubwa, kwa maana kama ingekuwa ndo hilo, ingeleta hali ngumu ya kukabiliana kwa maana ya kutaka kufanya  maamuzi ya uchaguzi wa haraka lakini usio leta tija na kwa maana hiyo  yeye binafsi anao uhakika ya kwamba, lazima kusali kwa ajili ya miito na kwa pamoja kuweka umakini zaidi katika shughuli ya uchungaji wa vijana!

03 September 2018, 10:45