Tafuta

Vatican News
Rais mpya wa Mexico Manuel López Obradorn ameliomba Kanisa Katoliki kushirkiana katika ushauri wa hali halisi ya nchi Rais mpya wa Mexico Manuel López Obradorn ameliomba Kanisa Katoliki kushirkiana katika ushauri wa hali halisi ya nchi  (ANSA)

Kanisa nchini Mexico inatoa mchango wake mkuu katika serikali

Kanisa halitoi mchango wake kwa ajili ya wema wa wote kwa njia ya mafundisho na shughuli zake tu, bali hata kuwa na kuwa na fursa za nafasi ya makutano, mazungumzo na ujenzi wa amani. Kwa maana hiyo Rais Noya nchini humo ameliomba Kanisa ushiriki hai katika Jukwaa la taifa , ambapo Rais wa Baraza la Maaskofu nchini humo amekubali.

Sr. Angela Rwezaula - Vatican News

Baraza la Maaskofu nchini Mexico kama sehemu muhimu ya utume wake, wamekubali mwaliko wa kawaida wa Rais aliyechaguliwa Bwana, Lic. Andrés Manuel López Obradorn kuudhulia  Jukwaa la ushauri kwa ajili ya kutafuta mchakato wa mkataba wa mapatano ya kitaifa.

Jukwaa hili la kusikiliza na kushauriana ni moja ya nafasi ya mazungumzo yaliyokubaliwa  ili kutafuta mapendekezo yaliyo tokana na sekta mbalimbali za watu katika kanda nyingi za nchi , pia  kuwa kiini cha maendeleo ya kisiasa ya umma na hatimaye kufikia ushindi dhidi ya vurugu, ujenzi wa amani na mapatano kitaifa.

Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Mexico Kardinali José Francisco Robles  Ortega amekabidhi shughuli hiyo Askofu Mkuu Carlos Garfias Merlos wa jimbo la Morelia ambaye ni mkuu wa kitengo cha haki, mapatano, Imani  wa Baraza hilo ili kuweza kutoa mchango wao kitaifa kwenye  shughuli za kichungaji ambapo katika shughuli hiyo, Kanisa Katoliki limejikita kwa dhati katika nyanja mbalimbali kwa kipindi cha muda mrefu katika nchi hiyo.

Wakati huo huo, ameaaalika pia maaskofu wote, kupokea maombi yaliyotolewa na serikali kwa namna ya kwamba wanaweza kushiriki angalau moja ya jukwaa katika majimbo , kwa njia hiyo kwa kuwashirikisha padre, watawa au walei, wawakilishi katika moja ya mkutano huo kwani ni moja ya shughuli yenye thamani kubwa katika mchakato wa kichungaji kwa upande wa mapatano na ujenzi wa amani.

Jukwaa hili linaweza kuwa kweli moja ya fursa kubwa, kuweza kushirikishana kwa ujasiri, uvumilivu na busara, utajiri wa Injili kwa namna ya utulivu na wingi wa maono na mtazamo wa juu kwa ajili ya uwelewa na wa nchi yao, na  kufanya kazi kazi kwa pamoja kwa namna chanya ya kutafuta suluhisho la migogoro.

19 August 2018, 10:05