Tafuta

Kanisa nchini Congo DRC limeanza kujikusanya kwa pamoja kwa mara nyingine tena  kwa ajili ya nchi yake katika uchaguzi Kanisa nchini Congo DRC limeanza kujikusanya kwa pamoja kwa mara nyingine tena kwa ajili ya nchi yake katika uchaguzi  

Dr.Tveit aiomba Congo DRC kuungana kwa ajili ya amani!

Siku za hivi karibuni, katibu mkuu wa Baraza la Makanisa duniani, mchungaji Olav Fykse Tveit, alifunga safari kwenda Congo akiongozana na wawakilishi wengine. Katika ibada ya kiekumene kwenye Kanisa Kuu la Kiluteri huko Kinshasa na kuhamasisha waendeleze juhudi zao za kiupatanishi na kufanya hivyo kwa ajili ya amani

Frt. Tito Kimario - Vatican

Hivi karibuni Kanisa nchini Congo limeanza kujikusanya kwa pamoja kwa mara nyingine tena  kwa ajili ya nchi yake. Kwa mujibu wa Baraza la maaskofu Katoliki nchini Congo, licha ya taarifa nzuri ya mgombea mwingine wa uchaguzi wa Rais mbali na rais aliyeko madarakani ambaye anamaliza muda wake  Joseph  Kabila , bado kuna matatizo mengi ambayo yanapaswa kutiliwa maanani kama vile  uelewa na utumiaji wa mashine za kupigia kura, suala la orodha ya wapiga kura ambayo ina wapiga kura wengi ambao hawajafanya usajili wa kidigitali na baadhi ya mazingira ya kisiasa ambayo hayajafanyiwa kazi ili kuhakikisha utengamano wa hali ya kisiasa inayoridhisha. Kama hayo yote hayatazingatiwa kuna hatari ya kujiaminisha kwamba mambo yote ni shwari na kufikia katika uchaguzi na matokeo tata na ambayo yataweza yakazua kwa mara nyingine kwa upya mkwamo wa kisiasa.

Siku za hivi karibuni, katibu mkuu wa Baraza la Makanisa duniani, mchungaji Olav Fykse Tveit, alifunga safari kwenda Congo akiongozana na wawakilishi wengine. Katika ibada ya kiekumene kwenye Kanisa Kuu la Kiluteri huko Kinshasa, Mchungaji Tveit aliwahamasisha wanajumuia katika ibada hiyo kuendelea na juhudi zao za kiupatanishi. “Fanyeni yote kwa ajili ya amani” alisema na kuongeza kwamba ni jukumu muhimu sana katika maisha! Kulinda amani na kutenda mema kwa mshikamano, hata katika tofauti zetu. Ni swali la msingi kwa Kanisa na hasa katika zama hizi kuliko wakati mwingine wowote ambao tunahitaji amani na mifano bora katika maisha yetu ili kuibadilisha dunia na kuifanya mahali bora zaidi pa kuishi.

Akiendela na mahubiri yake alisema, mapinduzi ya michakato ya amani nchini Ethiopia na Eritrea yamekuwa ya kutia moyo kwa mabalozi wengi wa amani. Kumbe kama imewezekana kwao hata kwetu sote inawezekana! Aliendelea  Mchungaji Tveit kwamba “wote tunahitaji amani” kama ilivyo muhimu kwa maneno yanayounganisha na “yanayoweza kutafsiri sheria, makubaliano ili kwenda mbali zaidi ya matatizo. Kwa maana hiyo  “Tunapaswa kuungana sote kama makanisa katika suala  hili” kama alivyokumbushia hata Papa Fransisko hivi karibuni alipoutembelea Baraza la Umoja wa Kakanisa duniani mwezi wa sita mwaka huu. Kutembea, kusali na kufanya kazi pamoja ilikua kauli mbiu yetu, na hiki ndicho tunachokifanya amesisitiza Mchuchangji Tiveit

Hatimaye, Mchangaji Tveit alionesha huzuni yake kwa kifo cha Bwana  Koffi Annan, mtu wa amani, katibu mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa, aliyefariki dunia tarehe 18 Agosto. “Hata kama juhudi zake hazikufikia malengo yaliyotarajiwa, Annan akuwahi hata siku moja kukata tamaa na alipendekeza daima majadiliano na amani hususani alitoa hamasa kwa kazi za umoja wa makanisa duniani. Apate rehema, kwa Mungu apumzike kwa amani”.

Hata hivyo kuhusiana na habari hiyo zaidi, Bwana Cofi Annani aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) ambaye aliaga dunia tarehe 18 Agosti 2018  atazikwa na serikali ya taifa lake Ghana, katika Jiji la Accra Septemba 13. Hii ni kulingana na habari alizotoa mapema wiki iliyopita rais wa Ghana Nana Akufo-Addo baada ya kukutana na familia ya hayati Annan, akitaja hafla ya mazishi ya kiongozi huyo kuwa ya umuhimu kwa taifa hilo na dunia.

Akikumbukwa na Rais wake Bwana Akufo-Addo alisema kuwa  Bwana Annan aliaga dunia tarehe 18 Agosti 2018 akiwa na miaka 80 baada ya kuugua kwa muda mfupi, akiwa nchini Uswizi. “Alikuwa mmoja wa viongozi wenye umaarufu zaidi katika kizazi hiki, alikuwa kama ndugu yetu mkubwa. Itakua hafla kubwa kwa taifa letu na tunatarajia viongozi wengi kuhudhuria,”

Ni wazi sasa kuwa Bw Annan atazikwa Jijini Accra kwenye kaburi la kijeshi, lililojengwa majuzi. Kiongozi huyo alizaliwa eneo la Kumasi na kukulia huko kabla ya kufanya kazi na Umoja wa Mataifa UN kwa takriban miongo minne, akifikia kileleni kama katibu mkuu wa muungano huo!

 

 

29 August 2018, 16:28