Cerca

Vatican News
Maandamano ya watu kupinga Eutanasia Maandamano ya watu kupinga Eutanasia   (ANSA)

Askofu Mkuu wa Sydney awaalika watu kupinga sheria ya Eutanasia

Kanisa Katoliki huko Australia kwa haraka wanajikita katika harakati za kutetea maisha na watu waathrika walioshambuliwa na mazoezi ya Eutanasia na kifo cha kusindikizwa. Kwa kufanya hivyo Askofu Mkuu Anthony Fisher wa Jimbo Kuu la Sydney anatoa wito wa kutia sahini kwa wingi ya hapana kukubali Eutanasia,.

Sr Angela Rwezaula - Vatican 

Askofu Mkuu wa Sydney na kiongozi mkuu wa wakatoliki Australia anawaalika watu kuunga mkono katika kutia sahini ya kura ya maoni ya kupinga muswada katika bunge wa sheria ya eutanasia na kifo cha kusindikizwa

Kuanzia tarehe 14 -16 Agosti Bunge nchini Australia litajikita katika shughuli za mjadala wa  kupiga kura za maoni kwa lengo la kutazama  muswada wa sheria ya mwaka 1997 inayozuia maeneo ya Shirikisho  kuruhusu eutanasia na kifo cha kusindikizwa. Sheria hiyo ilikuwa imekubaliwa baada ya mwaka 1995, katika maeneo ya Kaskazini  mwa mchi na ambao walitoa njia huria kwa  kile walicho kiita kifo kitamu.

Kanisa linawaalika watu  watie saini ya maoni ya hapana Eutanasia.

Kanisa mahalia kwa haraka wameendelea kujikita katika harakati za kutetea maisha na watu waathrika walioshambuliwa na mazoezi haya ya vifo. Kutia sahini ya hapana kukubali eutanasia, ndiyo wito wa nguvu uliotolewa na Askofu mkuu wa Sydney, Anthony Fisher, ambapo anaomba kukusanya kwa wingi sahihi ikiwa pia kwa mpango na  kikundi cha Pro life kiitwacho matumaini  ( preventing AEuthanasia ad assisted Suicied) chama kinachounganisha mashirika mbalimbali ya kimataifa na binafsi.

Kivuli cha makubaliano ya kisiasa juu ya kifo cha kusindikizwa.

Kwa namna ya pekee sheria hii inakumba  maeneo ya mji Mkuu wa Australia, Camberra, hadi kufikia kanda  ya Kaskazini na Kisiwa cha Norfolk ambayo ni sehemu ya Jimbo Kuu Katoliki  la Sydney, kuweka sheria ya Eutanasia na kifo cha kusindikizwa.

Mpango wa sheria hiyo utawasilishwa katika bunge la wademokratiki na Bwana David Leyonhjelm ambaye amewambia vyombo vya habari kwamba, wamefikia makubaliano na waziri Mkuu Malcolm Turnbull ili kuwezesha kura za hisia ya maoni juu ya mada katika ofisi mbili za Bunge, kwa mabadilishano ya kura kwa ajili ya kurudisha jengo wa Australia na uundaji wa Tume ya Australia kwa ajili ya ujenzi na majengo. Lakini iwapo makubaliano hayatapata mwafaka , mbunge huyo  Leyonhjelm ametishia kutoa adhabu kwa serikali  hasa ya kukataa kushirikiana nayo katika miundo  ya msingi inayohusu kijamii.

Walemavu na wazee zaidi wako hatari ya Eutanasia.

Jimbo Kuu Katoliki la Sydney linakumbusha kuwa Eutananasia na kifo cha kusindikizwa ni matukio ya kushambulia bila ubaguzi hasa watu walio athirika na ambao wako tayari kama vile wazee, walemavu na makundi mbalimbali yaliyoko katika hatari, hivyo Kanisa linaomba Bunge litambue kwamba, uzoefu wa nchi za nje unaonesha kuwa hakuna mtindo wowote wa uhakika ambao unatoa sheria kufanya matendo hayo.

Zaidi wanaonesha kuwa vyama vya madaktari wa Australia wamekuwa wakipinga sheria hiyo ya kifo cha  kusinidikizwa na  na eutanasia. Kwa njia hiyo Askofu Mkuu Fisher anathibitisha kuwa wapo tayari kusaidia wagonjwa vema na waathrika wa jumuiya yao. Katika Mtandao wa Chama cha Madaktari Australia wanabaki kwa sasa na upinzani mkubwa wa kuruhusu sheria ya Euthanaisa na kifo kusindikizwa na hivyo madaktari wako kinyume na matukio hayo mabayo yanataka mwisho wa maisha ya binadamu.

Mwaka jana wataalam 105 wa Australia walitia sahini wazi wakiomba serikali ya Victoria isiruhusu sheria hiyo ya Euthanasia na kifo vha  kusijndikiza, vilevile waliomba badala yake  serikali itoe zana za kutosha ili kuwasaidia wagonjwa ambao wako hala ya hatari ya kifo, lakini bila kuwaua kwa makusudi.

Shirika la Hope katika maandishi yao kwenye mtandao wanasema duniani vyama 107 kati ya 109 vya  madaktari kitaifa ambao wanaunda mashirika ya madaktari ulimwenguni, wanazidi kupinga euthanasia na kifo cha kusindikizwa. Na wana thibitisha kwamba, wazungumze na kuliambia Bunge  kuwa, ipo haja ya kuwasikiliza madaktari! Waombe wasikilize taaluma ya madaktari, ambao wanalinda wazalendo wa Australia katika hatatr hii ya euthanasia na kifo cha kusindikizwa.

Serikali ya Victoria kuwa ya kwanza kuruhusu sheria ya eutanasia.

Mjadala mkubwa wa mwisho wa maisha ulifunguliwa kwa upya mara baada ya Novemba mwaka jana, Serikali ya Victoria kuwa ya kwanza katika nchi kuruhusu Euthanasia na  kuthibitisha ya kuwa wagonjwa walio hatari ya kifo watapewa haku ya kuomba dawa ya kumaliza maisha yao ili watulize mateso. Na yote hayo yanatarajiwa kuanza mwezi Juni 2019.  Hata hivyo aliye endelea kutia chachu na kutikisa dhamiri la uamuzi huo, anajulikana kwa jina la  David Goodall, mtafiti, mwenye umri wa maika 104, japokuwa hakua mgonjwa wa kuteseka lakini alichagua kupanda ndege kwenda nchini Uswiss ili kufa kicho cha kusindikizwa!

Ulaya inazidi matukio ya euthanasia.

Jambo la kuongeza wasiwasi ni takwimu zinazoonesha  kuongezeka kwa vifokwa njia ya euthanasia katika nchi ambazo zimekublai sheria hii. Namba inazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka, mfano nchi ya Holand na Ubelgiji, kama inavyojieleza ripoti ya mashirika  ya kuthihiti  nchi mblii ambazo zinajieleza hata makumi ya kesi za watu ambao wamkimbilia katika nchi hizo kwa ajili ya vifo vya kusindikizwa.

Padre Skruzny: wote wako hatarini : Katika vyombo vya habari, Vatican News, vimemkariri Padre Erick Skruzny Gombera  wa Seminari ya Redemptoris Mater huko Synedy akizungumza juu ya wasiwasi mkubwa kwa kile kilichotokea huko Ulaya baada ya kuruhusu sheria ya eutanansia. Na hivyo anasemAskofu Mkuu Ficher wa Sydney anatafuta kila njia  kusaida kila sehemu, ili watu kweli watambua hatari uluyopi ambayo inazidi kushiria hata nchi za Ulaya, kama vile Holand, Ubelgiji , Ireland , kwa maana wakati wa kufanya utafiti imeonekana wazi kuwa watu wengu wanafanya hivyo bila kuwa na hatia na mwishow wate wansihia katika mtego wa hatari na siyo wazee tu bali hata vijana , watoto na wale ambao hawana mtetezi na mlinzi. Kwa maana hiyo Askofu Fisher anawasiwasi mkubwa juu ya hilo!

 

14 August 2018, 15:36