Papa Francisko atoa wito wa kuhamasisha haki na msimamo nchini Myanmar!

Ukaribu wa Papa Francisko kwa nchi ya Myanmar ameuonesha wakati wa fursa ya sala ya Malaika wa Bwana hasa kwa wahusika wa nchi hiyo ili kuondokana na mgogoro huo wa kisiasa ambao umesababishwa na mapinduzi nchini humo.Amewaalika wote kusali kwa kimya.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana, Jumapili tarehe 7 Februari 2021, Papa Fracisko ameelezea wasi wasi wake katika kipindi kigumu walicho nacho  nchini Myanmar, mara baada ya mapindizu ya kijeshi yaliyotokea mnamo tarehe Mosi Februari na kusababisha kukamatwa kwa kiongozi na mwenye nobel ya amani Aung San Suu Kyi. Nchi ambayo ilibaki moyoni mwa Papa wakati wa ziara yake ya kitume mnamo mwaka 2017,  kwa maana hiyo amewaalika waamini wote kwa pamoja kusali kwa ukimya:

Katika wakati huu nyeti napenda kuwahakikishia kwa mara nyingine tena  ukaribu wangu wa kiroho, sala yangu na mshikamano wangu kwa watu wa Myanmar na ninaomba kwamba wale ambao wana jukumu nchini wajikite kwa  na dhati kwa ajili uwajibikaji wa huduma ya wema wa wote, kuhamasisha haki kijamii na msimamo wa kitaifa katika umoja wa kidemokrasia. Tuombee Myanmar.

Jamapili ya sala na kufunga

Maneno ya Papa yamewadia katika  siku ambayo Baraza la Maaskofu  wa Birmania  (Cbcm) wamewaalika waamini kushiriki katika siku maalum ya kufunga na sala kwa ajili ya amani. Maaskofu wameomba nia na mahubri ambayo yazindue tena wito wa mazungumzo na siyo vurugu, na kurudisha demokrasia, ambayo Kardinali Charles Bo, Rais wa Baraza la maaskofu alikuwa amekwisha toa katika wuto wito wake kwa watu na taasisi zote manmo tarehe 4  Februari 2021. Kwa maneno yake, ambayo yalikumbusha ni kiasi gani amani na demokrasia ndiyo njia pekee, yameongezewa tena kwa siku za hivi karibuni na na Kardinali Vincent Nichols, rais wa Baraza la Maaskofu wa Ungereza na  Wales (CBCEW)  ambaye kwa tamko fupi aliunga mkono  maombi ya upatanisho kwa ajili ya nchi ya Myanmar na kwa kuachiliwa kwa wafungwa wote wa kisiasa.

Maandamano ya amani

Wakati huo huo, tarehe 7 Februari 2021, kama ilivyokuwa  katika siku za hivi karibuni, watu wengi nchini Myanmar wameandamana kwa amani ili kupinga mapinduzi yaliyofanyika siku ya Jumatatu  Mosi Februari iliyopita, na kukamatwa  kwa viongozi hao kadhaa. Licha ya maombi ya kimataifa ya kuwaachilia huru watu wote gerezani au chini ya kifungo cha nyumbani, hakuna habari yoyote ya Aung San Suu Kyi, kiongozi wa Ligi ya Kitaifa ya Demokrasia (NLD), chama kilichoshinda katika kura mnamo tarehe 8 Novemba 2020. Kwa sasa, baada ya kukamatwa mnamo 1 Februari na kutangazwa kwa hali ya hatari, kiongozi huyo anaonekana alishtumiwa kwa kukiuka sheria kuhusu uagizaji nje wa nchi kwa umiliki wa mazungumzo na anaonekana kukamatwa katika eneo lisilojulikana. Pia akiwa gerezani Win Htein, kiongozi wa kihistoria wa chama cha Aung San Suu Kyi, na Sean Turnell, profesa wa Australia, mshauri wa uchumi wa kiongozi aliyefukuzwa wa Birmania na wa kwanza kukamatwa kati ya wageni baada ya mapinduzi.

Miito kimataifa hadi sasa hazina maana

Jumatano iliyopita Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa,  bila kulaani waziwazi mapinduzi ya serikali ya Uchina na Urusi, imeomba serikali mpya iliyokabidhiwa kwa Jenerali Min Aung Hlaing, kuachiliwa kwa wote waliokamatwa, kuheshimu haki za binadamu kwa kuzuia matumizi ya vurugu na kurejeshwa mchakato wa kidemokrasia. Kwa kuongezea, nchini Indonesia na Malaysia wameomba kuitishwa kwa mkutano maalum wa Asean, Chama cha Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia, ambayo Myanmar ni mwanachama. Lakini hadi sasa kila kitu kinaonekana kuwa bure. Hadi sasa, ukimya wa mitandao ya kijamii uliowekwa pia umeongeza kutengwa kwa nchi. Sauti pekee inayowezekana ya kuonesha kutoridhika kwa hivyo ni uwanja ambao unaendelea kuhuisha kama hospitali, ambapo madaktari katika miji 30 wamepata njia ya maandamano ya amani kwa kuoneesha utepe mwekundu, rangi na ishara ya chama cha San Suu Kyi.

07 February 2021, 15:06