Tafuta

2020.04.24 Kardinali Charles Bo,Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Yangon nchini Myanmar. 2020.04.24 Kardinali Charles Bo,Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Yangon nchini Myanmar. 

Myanmar:Kard Bo.Mazungumzo ndiyo njia pekee ya amani

Askofu Mkuu wa Yangon anakubali ni kiasi gani kiongozi wa Birmania alijitoa maisha yake kwa ajili ya watu wake ili kupata nuru baada ya giza na ukaribu wake binafsi na sala ili arudi kutembea kati ya watu wake.Walakini,anamkumbusha jukumu la kuwasikiliza wengine,kwa sababu tukio lilitokea ni ukosefu wa mazungumzo na mawasiliano.Ni katika ujumbe wake baada ya mapinduzi ya kijeshi,ambapo jeshi na chama cha Aung San Suu Kyi lazima wazungumze.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Askofu mkuu wa Yangon nchini Myanmar, Kardinali Charles Bo anajaribu kurudisha kwa upya kile kilichotokea na anashangaa kile kilichoharibika baada ya 2015, wakati shukrani kwa jeshi la kitaifa liliweza kuleta mabadiliko ya amani ya nguvu kwa serikali iliyochaguliwa, chini ya mtazamo wa kupendeza ulimwenguni. “Kumekuwa na ukosefu wa mazungumzo kati ya viongozi wa serikali waliochaguliwa na Tatmadaw? Anauliza swali katika ujumbe huo. Kwa mujibu wa Kardinali Bo anasema, “Jeshi, lilikuwa limeahidi amani na demokrasia halisi na demokrasia ilikuwa njia ya matumaini ya kufanikisha wema wa wote”. Yote haya ni kutokana na kwamba hivi karibuni Jumatatu, tarehe Mosi Februari 2021 limefanyika tukio la mapinduzi ya kijeshi nchini Myanmar na kusababisha kushikiliwa kwenye mahabusu za kijeshi kwa Aung San Suu Kyi, Rais Win Myint na viongozi wengine wa kiraia, ambapo mataifa mengi yamelaani tendo hili na kutoa wito wa kurejeshwa utawala wa kidemokrasia na kuachiliwa huru viongozi hao wa kisiasa.

Hivi karibuni mamilioni ya watu walipigia kura kwa ajili ya  demokrasia, anasema kardinali Bo, lakini sasa jeshi kwa umoja limechukua udhibiti. Na ulimwengu umelaani uamuzi huo. Na anatoa onyo kuwa “madai ya makosa katika kura yangeweza kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo, mbele ya waangalizi wasio na upande wowote”. Mbele ya kukabiliana na ahadi za uchaguzi mpya wa kidemokrasia uliowekwa na jeshi, Kardinali Bo anarudia kusema kwamba watu wataweza kuamini ikiwa tu ahadi hizo zitaambatana na vitendo vinavyoonesha upendo mzuri kwao. Kardinali Bo anasisitiza wito wake kuwa hakuna vurugu ifanyike dhidi ya watu, wakati anabainisha kuwa manaibu wa Ligi ya Kitaifa ya Demokrasia, lakini pia waandishi, wanaharakati na vijana wamekamatwa. Ombi ni kuachiliwa haraka iwezekanavyo.

Akigeukia kwa namna ya pekee hasa Aung San Suu Kyi, Askofu Mkuu wa Yangon anakubali ni kiasi gani kiongozi wa Birmania aliweza kujitoa maisha yake kwa ajili ya watu wake huku akifanya uzoefu wa nuru baada ya giza, na kutoa ukaribu wake wa kibinafsi na na hivyo sala ili yeye aweze kwa mara nyingine tena kurudi kutembea kati ya watu wake. Walakini, anamkumbusha jukumu la kuwasikiliza wengine, kwa sababu tukio hilo lilitokea kutona na  ukosefu wa mazungumzo na mawasiliano na ukosefu wa kutambuliwa kati ya vyama vyao.

Hakuna kuwekewa vikwazo vya kimataifa ambavyo vinahukumu watu kwa umaskini. Kardinali Charles Bo kwa kuhitimisha ujumbe wake na hisia za shukrani kwa jamuiya ya kimataifa kwa kuwasindikiza na masuala ya taifa lake wakati huu, lakini anaomba kwamba hakuna hatua zichukuliwe ambazo mwishowe ziwadhuru watu na kusisitiza kwa nguvu zote kwamba: “hukumu inaweza kuleta matokeo ambayo siyo kidogo. (…) Hatua hizi ngumu zimetoa faida kubwa kwa wale wenye nguvu ambao wameweka macho yao kwenye rasilimali zetu”. “Ninakusihi: msilazimishe watu wanaohusika kuuza uhuru wetu ”. Hatari ni kuanguka kwa uchumi wa Myanmar na umaskini kwa mamilioni ya watu. Kwa njia hiyo wito wake wa  mwisho ni: “Kuhusisha pande zote katika upatanisho na ndiyo njia pekee. (…) Tutatue mizozo yetu na mazungumzo. Amani inawezekana. Amani ndiyo njia pekee. Demokrasia ndiyo nuru pekee kwenye njia hii”.

04 February 2021, 14:17