Mauritius #coronavirus Ujumbe wa Baraza la kidini kwa waislamu!
Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican
Waislamu katika pembe zote za dunia waliokuwa wakisubiri kuanza mwezi mtukufu wa Ramadhani sasa umewadia japokuwa katika kipindi ambacho kuna maagizo tofauti katika juhudi za kupambana na virusi vya corona au covid 19 ikiwemo marufuku ya kutoka nje na mikusanyiko ya umma. Kutokana na marufuku ya mikusanyiko, idadi ya jamaa katika misikiti pia ni marufuku katika mataifa tofauti kwa lengo la kuepuka maambukizi zaidi ya Covid-19. Kuanzia Nchini Saudia,kuingia na kutoka katika jiji la Makka na Madina imepigwa marufuku. Hija ndogo ndogo zimesitishwa pia kutokana na janga a virusi vya corona. Kwa ujumla ni Mataifa tofauti ikiwemo ya Mashariki ya Kati hata chini Uturuki mikusanyiko ya umma kwa ajili ya ibada na iftar vimepigwa marufuku!
Kufutia na janga hili basi hata Baraza la Kidini katika Kisiwa cha Mauritius kinaelezea mshikamano wake kwa Waislamu wote ambao wameanza mwezi Mtukufu wa Ramadhani licha ya vizuizi vilivyopo ili waweze kuishi vema mwezi huu mtukufu wa kiislamu. Haya yanasomeka kutoka katika ujumbe wa Rais wa Baraza la Dini,Philippe Goupille,amnaye anawaalika, kama ilivyopendekezwa na maimamu wao, kuimarisha uhusiano wa kifamilia na kuishi Ramadhani hasa katika mwelekeo wa kifamilia.
Katika ujumbe wake ameandika kuwa usomaji wa Korani na sala za kila siku ambazo haziwezi kufanyika katika misikiti na pia itakuwa muhimu kutoa sadaka kwa upendo wa wote, ndivyo viwe kpaumbele. Kiukweli ni nafasi nzuri ya kuweza kupyaisha uhusiano wa kifamilia na kujikita kwa kina katika mazungumzo na vijana na watoto, ameandika, huku akikumbuka kwamba hata Wakatoliki mwishoni mwa kipindi cha toba cha Kwaresima hawakuweza kusherehekea kama kawaida ya tukio hili kubwa na zaidi hawakuweza kukusanyika kwa pamoja katika makanisa kwa ajili ya sikukuu kubwa ya Pasaka.
Kadhalika Philippe Goupille katika ujumbe huo ameandika kwamba wanaungana na dini nyingine kubwa kwa njia mpya ya kufanya kwaresma. Pia ni fursa ya kujisikia karibu na dini nyingine, ili kuishi hatima hiyo kama jamuiya na kushiriki uzoefu huu mpya ambao umewekwa kwa ajili ya wema wa raia katika kuzuia maambukizi zaidi ya virusi vya corona. Katika umoja pamoja nao watasali kwa namna ya pekee ili Mungu aokoa kisiwa cha Mauritius na kuwasindikiza katika kuzindua kwa upya maisha yao ya kijamii na kiuchumi, anaihitimisha ujumbe huo.