Vatican News
Padre Anthony Makunda Katibu  mkuu wa Amecea amesema wanathibitisha jitihada zao za kukausha machozi kwenye nyuso nyingi za watoto ndani ya jumuiya zao. Padre Anthony Makunda Katibu mkuu wa Amecea amesema wanathibitisha jitihada zao za kukausha machozi kwenye nyuso nyingi za watoto ndani ya jumuiya zao. 

AMECEA:Jukumu la ulinzi wa watoto ni la kijamii!

Katika makao makuu ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Kanda ya Afrika Mashariki( Amecea)Nairobi,Kenya kumefanyika Semina iliyokuwa inatazama mada ya ulinzi wa watoto na watu wazima wenye kuathirika.Katibu Mkuu wa Amecea amethibitisha kuwa jukumu la wahusika wa ulinzi katika majimbo siyo tu kuwaelekeza waamini Wakatoliki,bali ni kulinda watoto wote bila kujali dini,changamoto hiyo ni suala la kijamii.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika semina ya kanda ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika  Mashariki (AMECEA) iliyo fanyika hivi karibuni huko Nakuru nchini Kenya ilifunguliwa kwa  mwaliko wa nguvu hasa katika jitihada za Kanisa kwa ajili ya kuhakiki na ulinzi wa watoto na watu waathirika. Semina hiyo ilikuwa inawalenga maafisa wahusika wa wasimamizi wa Utoto katika Majimbo katoliki ya  Kanda za Amecea.

Kwa mujibu wa tovuti ya Amecea, Padre Anthony Makunda Katibu  mkuu wa Amecea amesema “tuko hapa kuthibitisha jitihada zetu za kukausha machozi kwenye nyuso nyingi za watoto ndani ya jumuiya zetu. Hatuwezi kustarehe kama vile hatuna matatizo ya kukabiliana nayo. Hatuwezi kubaki tumefunga ofisi zetu, bali lazima twende kutazama kile ambacho kinatukia katika mantiki mahalia ambayo inahitaji umakini wetu”.

Uwajibikaji huo unapaswa ufanyiwe kazi kwa wote katika jamii na kwa maana hiyo Padre Makunde amewakumbusha maafisa hao wa kuwalinda watoto ya kuwa jukumu lao, “siyo tu kuwaelekeza waamini Wakatoliki, bali ni kulinda watoto wote bila kujali dini kwani changamoto hiyo ni suala la kijamii. Iwe kaama ni kiongozi wa Kikristo kutoka kwa dhehebu lingine la Kikristo au jamii ya kidini, iwe ni mzazi au mlezi ambaye amemnyanyasa mtoto, hiyo inatugusa pia kwa sababu wanapozungumza juu ya viongozi wa dini, sote tuko kwenye mashua moja”.

Kulingana na Katibu Mkuu, semina hiyo imewapa fursa ya kutathmini kile ambacho kimefanyika hadi sasa kikanda katika jukumu lao la kulinda watoto. “Tumetumia muda wa kufanya tathmini kama kanda ili kujionea wenyewe tumewezaje kumudu safari hii ambayo mama Kanisa alitualika kutembea katika nyayo hizo”. Aidha Padre Makunda ameongeza kusema: “Mchakato wa uratibu huu hautakiwi kuwa tu wa maagizo kutoka Roma; badala yake, unapaswa kumilikiwa na sisi wenyewe kama maafisa katika mikutano yetu na Kanisa mahalia la hapa. Na hii tayari imeoneshwa na ahadi za Marais wa Mabaraza  yetu ya Maaskofu katika kanda yote ya  AMECEA”.

Mkutano huo wa siku tatu unafuatiwa na ule kwa kwanza uliofanyika mwaka jana (2019) nchini Ethiopia, kwa kawakutanisha washiriki kutoka nchi saba za AMECEA, ambazo ni Kenya, Uganda, Tanzania, Malawi, Zambia, Sudan Kusini na Ethiopia- Eritrea na Shirikisho hili (Amecea) liliundwa kunako mwaka 1951 likiwa na makao yake makuu jijini Nairobi, Kenya.  Hata hivyo katika Mkutano huo Katibu Mkuu ameweza kuelezea masikitiko yake kwa baadhi ya Makanisa kama vile Eritrea kutoweza kushiriki Semina hiyo kutokana hali halisi ya kisiasa inayowakumba nchini humo hasa mara baada ya kutaifishwa kwa majengo ya Afya na Elimu  miliki ya Kanisa Katoliki kwa mujibu wa Serikali ya nchi. Kwa upande wa Kanisa la Asmara. Kufuatia na hiyo Shirikisho la Amecea limeonesha ukaribu wa kwa njia ya Sala na maombi na kwamba “Mungu Mwenyezi aweze kubadili akili na tabia za viongozi wa kisiasa katika nchi hiyo na kuruhusu watu waweze kufaidika na uhuru wa kidini ambao ni haki kwa wote”.

Katika suala la kanisa nchini Eritrea, hivi karibuni Kanisa Katoliki nchini Eritrea limeonesha kusononeka kwake dhidi ya Serikali ya Asmara kufuatia na kutoruhusu kuingia kwa uwakilishi wa Kanisa kutoka nchini Ethiopia tarehe 22 Februari 2020. Viongozi ambao hawakurusiwa ni Kardinali Berhaneyesus Demerew Souraphiel, Askofu Mkuu wa Addis Abeba, Askofu  Abune Mussiè Ghebreghiorghis Uqbu, wa Emdeber na Padre  Teshome Fiqre Weldetensae, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu nchini Ethiopia walikuwa washiriki katika maadhimisho ya Jubilei ya dhahabu  na sikukuu ya Kanisa la Kidane Mehert, ambayo ni Makao makuu ya Askofu  Mkuu wa Asmara,  Menghesteab Tesfamariam, lakini walizuiwa katika uwanja wa Mji mkuu wa Eritrea na kulazimishwa kurudi nchini kwao Ethiopia siku iliyofuata baada ya mjadala mkubwa ambao haukuleta muafaka. https://www.vaticannews.va/sw/church/news/2020-03/maaskofu-waomba-maelezo-serikali-ya-eritrea.html

 

 

07 March 2020, 13:42