Muungano wa Mapadre Tanzania wamehimizwa kulinda watoto wakati wa semina yao kuanzia tarehe 12-16 Agosti 2019 jijini Dar es Salaam Muungano wa Mapadre Tanzania wamehimizwa kulinda watoto wakati wa semina yao kuanzia tarehe 12-16 Agosti 2019 jijini Dar es Salaam  

TANZANIA:Jitihada za maaskofu kwa ajili ya kulinda watoto!

Kuongeza juhudi za kulinda watoto na kuhamasisha jamii dhidi ya kila aina ya dhuluma ndiyo wito uliotolewa hivi karibuni na Padre Charles Kitima Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania,TEC katika semina ya Umoja wa Mapadre katoliki nchini humo.Wajibu wa mapadre kulinda watoto iwe kiroho na hata kimwili na kujiepusha na ushiriki wowote wa tabia mbaya isiyo ya kimaadili amesisitizia!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kuanzia tarehe 12-16 Agosti 2019, imefanyika semina ya Muungano wa mapadre nchini Tanzania, semina iliyofanyika jijini Dar es salam Tanzania kwa kuandaliwa na Kanisa mahalia kwa ushirikiana na Shirikisho la Mabaraza la maaskofu Katoliki Afrika Mashariki (AMECEA). Katika Semina hiyo Padre Charles Kitima,Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, TEC wakati wa  hotuba yake ametoa wito juu kuongeza juhudi za kulinda watoto na kuhamasisha jamii dhidi ya kila aina ya dhuluma.

Kulinda watoto dhidi ya kila ubaya na hakuna kunyamaza

Padre Kitima katika hotuba yake amesisitiza kuwa ni wajibu wa mapadre kulinda watoto iwe kiroho na hata kimwili na kujiepusha na ushiriki wowote wa tabia mbaya isiyo ya kimaadili. “Ni jukumu letu kuwalinda watoto kutokana na madhara yote” amesema Padre Kitima. Akiendelea kusisitiza amesema,“kwa namna ya pekee hasa hatupaswi kuwaruhusu wanyanyaswe kwa njia yoyote ile. Suala la ulinzi wa watoto ni la ulimwengu mzima na uhalifu unaofanywa na wahusika wengine wa wakichungaji umeacha makovu kwa watoto wadogo. Padre Kitima kwa namna hiyo amewashauri mapadre wasifunike katu shida kama tabia hiyo mbaya ambayo inaweza kufanya mambo kuwa mbaya zaidi” amesisitiza.

Kutumia vipimo vya ulinzi kwa mujibu wa Kanisa

Kuwa walinzi wa watoto ndiyo agizo la Katibu Mkuu wa TEC ambalo amehimiza mapadre washiriki wa semina hiyo. Na wakati huo huo amewakumbusha juu ya njia ya kuthibiti ambayo tayari imewekwa na Kanisa kuhusu tendo la kulinda watoto wadogo dhidi ya unyanyasaji pamoja na maendeleo, kila jimbo nchini kuwa na mpango maalum wa ulinzi wa watoto.  Japokuwa, bado utekelezaji wake katika mkamkati huo na ndiyo maana Katibu Mkuu wa TEC amesisitizia juu ya hilo!

Kuhusu Motu Proprio ya Papa

“Maaskofu tayari wamekwisha chapisha Mwongozo wa Ulinzi wa watoto” amethibitisha Padre Kitima, na kinachohitajika katika majimbo  sasa, ni kuzitumia na  kuziainisha katika kila eneo lake binafsi”. Hata hivyo kama miongozo hii inajibu  yale maelekezo yaliyopo katika  Motu Proprio ya “Vos estis lux mundi " ya Baba Mtakatifu  Francisko. Sheria hii inaweka taratibu mpya wa mchakato wa kuripoti juu ya unyanyasaji na utumiaji nguvu na kuhakikisha kwamba maaskofu na wakuu wa mashirika ya kidini, wanaripoti juu ya kazi zao; aidha inaanzisha suala la lazima la wajibu wa makuhani  na watawa  kuripoti unyanyasaji na inaonyesha kwamba, kila jimbo katoliki, lazima liwe na mfumo ambao unapatikana kwa urahisi kwa umma katika kupokea ripoti hizo.

Mkutano wa Marais wa mabaraza ya Maaskofu kuhusu ulinzi wa watoto

Baba Mtakatifu Francisko analitaka Kanisa, kwa kuanzia na wachungaji wake wakuu, ili  kutambua madhara ya nyanyaso za kijinsia katika maisha na utume wa Kanisa na katika maisha ya mtu binafsi na kuanza kuwajibika; kwa kuzuia, ili kweli Kanisa liweze kuwa ni mahali safi na salama kwa ajili ya malezi na makuzi ya watoto wa Mungu. Hili limeoneshwa wazi hasa Baba Mtakifu Francisko alipoitisha Mkutano wa Kanisa Kuhusu Ulinzi wa Watoto Wadogo Ndani ya Kanisa kuanzia tarehe 21-24 Februari 2019 mwaka huu kwa marais wa Mabaraza ya Maaskofu Katoliki duniani na mkutano huo uliofanyika mjini Vatican.

Kwa hakika kimekuwakielelezo makini cha wajibu wa kichungaji ili kuweza kukabiliana na changamoto hii nyeti katika ulimwengu mamboleo. Lengo lilikuwa ni kutoa katekesi kwa Mabaraza ya Maaskofu Katoliki katika sehemu mbali mbali za dunia, ili Maaskofu waweze kutambua madhara ya nyanyaso za kijinsia dhidi ya watoto wadogo. Hadi sasa Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kuhimiza na kuomba kwamba Kanisa liweze kuwa ni nyumba safi na salama kwa malezi na makuzi ya watoto wa Mungu wote.

Kuna hata data nyingine nchini Tanzania

Mwishoni mwa mwezi desemba 2018 kulizinduliwa kampeni ya Siku kumi na sita (16) za Kupinga Ukatili wa Kijinsia nchini Tanzania  na serikali ikasema kwamba imeandaa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kwa lengo la kupunguza kiwango cha ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika jamii ya kitanzania kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022. Mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Wanawake na Jinsia (2000); Mkakati wa Taifa wa Maendeleo ya Jinsia (2005); Sera ya Maendeleo ya Mtoto (2008); Sheria ya Makosa ya Kujamiiana – SOSPA (1998). Rejea: https://www.vaticannews.va/sw/world/news/2018-12/kassim-majaliwa-mpango-kupunguza-ukatili-kijinsia-tanzania.html

Na kwa mujibu wa Kituo cha Sheria za Haki za Binadamu (LHRC) tangu Januari hadi Juni 2018,karibu watoto 394 wa Tanzania wamekuwa waathirika wa unyanyaswaji kijinsia.

PADRE KITIMA
25 August 2019, 14:46