Kuongeza kwa kasi ya maarifa huzidisha matumaini ya kuponya saratani
Na Angella Rwezaula: - Vatican.
Katika kauli mbiu iliyoongoza Siku ya XXIII ya Kimataifa na kupambana na Saratani Ulimwenguni kwa mwaka 2023 inasema “Kesi huongezeka kidogo lakini muhimu zaidi kuishi na kurefushwa. Kattika taarifa kuhusu siku hii wanabainisha kwamba kuna ongezeko kidogo la kesi ambalo bado katika miaka 15 iliyopita, kutokana na matibabu mapya, kuna sababu nzuri ya kuishi watu 2.5 hadi milioni 3.6 na saratani miaka mitano baada ya kugunduliwa.
Ufikiaji sawa wa utunzaji kwa wote
Mada ya kampeni ya 2022-2024 ambayo ni “Funga Pengo la Utunzaji: Kila mtu anastahili kupata huduma ya saratani. Kauli mbiu inayotaka kumulika jinsi ilivyo muhimu kuelewa na kutambua ukosefu wa usawa katika utunzaji wa saratani ulimwenguni kote. Ukosefu wa usawa ambao unasisitiza tofauti katika upatikanaji wa matibabu ya ugonjwa ambao kiukweli unazidi kutibika, hasa ikiwa utatambuliwa kwa wakati. Na katika hilo, kinga na elimu ni mambo msingi.
Kuna utofauti wa miaka ya nyuma na sasa
Kwa kisikiliza maoni kutoka katika mahojiano na Profesa Paolo Tortora ambaye ni mkurugenzi wa Kitengo cha (Oncology) Matibabu ya Saratani cha Hospitali ya Gemelli Jijini Roma, alielezea hali ya sasa kwamba kwa Italia inahusika, katika mwaka 2022 kulikuwa na ongezeko la matukio ya saratani karibu 4% kwa wanaume na 0.7 kwa wanawake wenye wastani wa 1%. Inawezekana kwamba hiyo pia ni kwa sababu ya ukweli kwamba utambuzi haujafanywa mapema kwa sababu ya janga la uviko. Kwa hivyo, ongezeko kidogo lilirekodiwa kwa aina zote za saratani. Walakini, ikiwa tutazingatia kunusurika, ambayo ni dhahiri inahusishwa na maendeleo katika matibabu na uchunguzi, inaweza kuonekana kuwa kumekuwa na kiwango kikubwa katika miaka 15 ambayo labda hatungetarajia,” alisema daktari huyo.
Ujumbe wa matumaini
Kugunduliwa na saratani mapema kungeshtua mtu yeyote, lakini kuna matumaini. Daktari Tortorella alisema kwamba katika miaka ya hivi karibuni amekuwa akiona mambo ambayo hakuwahi kuyaona katika miongo iliyopita. Kwa kufanya utafiti, hata wa kwanza, kuna matumaini ya kuweza kuponya ugonjwa. Kwa wale wanaougua, uwezekano wa kupona ni wa juu sana kuliko hapo awali. Kuongeza kasi hii ya maarifa kunaongoza utafiti katika mwelekeo unaotakiwa. Huu ni ujumbe ambao ninahisi kuutoa, kwa uaminifu na utulivu uliokithiri”, alihitimisha Tortorella.