Mkutano Mkuu wa 20 wa AMECEA Tanzania Mkutano Mkuu wa 20 wa AMECEA Tanzania 

AMECEA:Signis Roma yahamasisha ujumbe wa Laudato Si kwa viongozi wa Kanisa

Katika miaka michache iliyopita,Signis imekuwa ikisisitiza kukuza Vyombo vya Habari kwa ajili maendeleo na amani.Katika mipango yao wanahimiza wale wanaoshughulikia masuala ya mazingira,kama vile mafunzo kuhusu Laudato Si' au kuchagua suluhisho la kijani kwa ajili ya vifaa kama vile paneli za jua kwa ajili ya usambazaji wa nishati ya kuendesha radio.Alisema hayo Katibu Mkuu Msaidizi wa Signis Bi Maria Chiara wakati wa ujumbe mshikamano kwa AMECEA.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

SIGNIS iliwahakikishia AMECEA kuunga mkono katika utekelezaji wa Laudato si kwa kushirikisha vyombo vyote vya mawasiliano katika eneo hilo. Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu Msaidizi wa SIGNIS Bi Maria Chiara De Lorenzo tarehe 12 Julai, 2022 alipokuwa akitoa ujumbe wake wa mshikamano katika Mkutano Mkuu wa 20 wa AMECEA jijini Dar es Salaam Tanzania. Kwa kutazama mada ya Mjadala wa AMECEA kuhusu Athari ya Mazingira katika Maendeleo ya Kibinadamu, Bi Maria Chiara alieleza kuwa, hivi karibuni SIGNIS imesaidia mipango mingi ya mawasiliano chini ya mafunzo, vifaa, au programu za uzalishaji, zinazotolewa na PSPF na kuchunguzwa na SIGNIS.

Mkutano Mkuu wa 20 wa AMECEA Tanzania 10 -18 Julai 2022
Mkutano Mkuu wa 20 wa AMECEA Tanzania 10 -18 Julai 2022

Katika miaka michache iliyopita, alisema kwamba wamekuwa wakisisitiza kukuza Vyombo vya Habari kwa ajili maendeleo na amani. Katika mipango yao wanahimiza wale wanaoshughulikia masuala ya mazingira, kama vile mafunzo kuhusu Laudato Si' au kuchagua suluhisho la kijani kwa ajili ya vifaa kama vile paneli za jua kwa ajili ya usambazaji wa nishati ya kuendesha radio. Vivile Bi Chiara alieleza jinsi ambavyo wanayo mipango kadhaa kadhaa nchini Liberia kama vile walivyoisaidia Radio ‘Paraclete’ na nchini Tanzania wameisaidia Radio Hekima kwa paneli za solar ili kuboresha Stesheni za radio zinazotangaza masuala ya mazingira, amani, utamaduni na haki. Hata hivyo kwa kueleza zaidi alisema Radio Paraclete nchini Liberia inatangaza kipindi maalum kuhusu kilimo cha kisasa na kitaalamu kwa kulinda udongo.

Mkutano Mkuu wa 20 wa AMECEA Tanzania 10 -18 Julai 2022
Mkutano Mkuu wa 20 wa AMECEA Tanzania 10 -18 Julai 2022

Maria Chiara pia alionesha kufurahishwa na mada ambayo Mjadala wa Mkutano wa 20 wa AMECEA ulichagua. “Nina furaha kwamba maaskofu wa AMECEA wamekusanyika hapa Tanzania ili kutoa maazimio ya jinsi gani kwa pamoja tunaweza kulinda sayari yetu”, alisema. Na akuzugumzia kuhusu Amani, Maria Chiara pia alieleza kwamba, kusikiliza kwa sikio la moyo, ndivyo Papa Francisko anahimiza kufanya kurejea katika ujumbe wake wa mwisho wa Siku ya Mawasiliano ya kijamii mwaka huu 2022. Kwa kusisitiza zaidi alisema kama wawasilianaji, ndicho walikuwa wanafanya hapo AMECEA. Hasa “kusikiliza kwa sikio la moyo, na kujifunza kutoka katika uchangamfu wa Kanisa katika kila Nchi yenu”, alisema. Ikumbukwe kwamba SIGNIS ni chama cha Mawasiliano Katoliki Ulimwengu chenye vyama wanachama na Wawakilishi katika zaidi ya nchi 100, kati ya hizi pia  nchi 6 kati ya 9 za AMECEA (na Sudan Kusini iko mbioni kwenye mchakato huo).

Mkutano Mkuu wa 20 wa AMECEA Tanzania 10 -18 Julai 2022
Mkutano Mkuu wa 20 wa AMECEA Tanzania 10 -18 Julai 2022

Ikumbukwe: Mkutano Mkuu wa AMECEA kwa kawaida hufanyika kila baada ya miaka minne. Kwa maana hiyo viongozi hao walihitimisha kwa kuchagua mada na nchi mwenyeji kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa 21 ujao  utakaofanyika mnamo 2026 jijini Kampala Uganda.

11 August 2022, 16:17