Ukraine:makombora katika soko,G7 na NATO wapyaisha ahadi dhidi Moscow
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Viongozi wa G7 waliokusanyika nchini Ujerumani wamelaani uhalifu wa kivita na wanahakikisha uungwaji mkono kamili wa Kiev. Jumatano tarehe 29 Juni 2022 mkutano wa NATO unatarajia kuanza huko Madrid na tangazo la athari kubwa linatarajiwa kutangazwa. Hata hivyo kutokana na tukio lililotokea tarehe 27 Juni, waokoaji bado wanashughulika kuondoa vifusi na kuzima moto katika kituo cha ununuzi cha Amstor huko Kremenchuk, katikati mwa Ukraine. Makombora mawili ya masafa marefu yangeweza kusababisha mauaji ya idadi kubwa ikizingatiwa kwamba ilikuwa saa 10.00 kamili za jioni ambapo, zaidi ya watu elfu moja walikuwepo kwenye jengo hilo. Walakini, viongozi wanaamini kuwa idadi ya vifo 18 bado inaweza kuongezeka! Shambulio hilo lilihusisha eneo lote la Magharibi na serikali ya Kiev nchini Ukraine na Rais wa Ukraine Zelensky alizungumza kuhusu kitendo cha kigaidi.
Tukio hilo mara moja lililaaniwa na Viongozi wa Mataifa makubwa tajiri ( G7,) ambayo yanamalizika mkutano wao Jumanne 28 Juni 2022 huko Elmau nchini Ujerumani. Viongozi wa mataifa saba yenye nguvu walisisitiza juu ya msaada wao kamili wa kifedha, kibinadamu, kijeshi na kidiplomasia kwa nchi ya Ukraine kadiri inavyohitajika. Rais Biden hata hivyo asema kuongeza vikwazo vipya dhidi ya Moscow, ambayo lazima iguswe mahali panapoumiza zaidi.
Ujumbe mwingine mzito vile vile utatoka katika mkutano mkuu wa NATO mjini Madrid nchini Hispania. Hata hivyo Urussi wanabainisha kuwa itatambuliwa kama tishio kubwa zaidi. Na katibu Mkuu Jens Stoltenberg anatarajia kuongeza vikosi vya kukabiliana haraka Ulaya Mashariki hadi 300,000. Jibu la Moscow limekuja, kati ya mengine, kutoka kwa balozi wa Urussi huko Marekani, Bwana Anatoly Antonov ambaye ameonya kuwa: “Utoaji unaoendelea wa silaha kutoka Washington hadi Kiev unaongezea zaidi mzunguko wa migogoro na kuongeza tishio zaidi na matokeo yasiyotabirika”.