Pembe ya Afrikauhitaji wa msaada kutokana na mabadiliko ya tabianchi
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kwa sababu ya kushindwa kwa vipindi vitatu vya musimu wa mvua mfululizo, Nchi nne za Pembe ya Afrika ziko zinaishi kipindi kigumu sana cha ukame kwa makumi ya miaka sasa. Hizi ni pamoja na nchi ya Gibuti, Ethiopia, Kenya na Somalia, ambapo milioni 10 ya watoto wanahitaji msaada wa kuweza kuishi maisha yao. Ukame huo unaongezea utapiamlo wa kutisha kwa watoto na familia zao. Kwa ujumla ni milioni 1.7 za watoto wenye utapiamlo katika sehemu hizo. Nchini Ethiopia tatizo kubwa la utapiamlo wa kutisha kwa watoto chini ya miaka 5 na katika sehemu ambazo zimekumbwa na ukame, mwezi Februari walikuwa ni zaidi ya asilimia 15% kulinganisha na mwezi Februari 2021.
Baada ya hitimisho la utume wa siku nne nchini Ethiopia, mkurugenzi mkuu wa UNICEF, Bi. Catherine Russell alishauri jumuiya ya Kimataifa kuongeza juhudi za msaada kwa haraka ili kuepuka janga kubwa la kibinadamu kufuatia na ukame nchini Ethiopia na eneno linalobaki la Pembe ya Afrika. Muktadha wa ukame nchini Ethiopia ni mgumu sana kwa mujibu wa Bi Russel. Katika Kanda ya Somalia na katika sehemu ambazo zimepata pigo la ukame, yeye binafsi alikutana na watoto na familia ambao kwa hakika wamepoteza kila kitu. Mifugo yao imekufa na matokeo hayo, hawana chanzo cha kipato chochote. Hawawezi kuwalisha watoto wao na wanasafri kutafuta chakula na maji. Kwa maana hiyo ni lazima kuwafikia familia hizo sasa, kabla hawajachelewa.
Ndoa za utotoni nchini Ethiopia
Bi Russell amethibitisha jinis ambavyo wao kama shirika linaendelea kukabiliana na mgogoro wa utapiamlo, kukosa kwa maji safi na salama ya kunywa hata kwa kuongeza hali halisi kuwa mbaya ya watoto na wanawake. Watoto wanalimika kunya maji machafu na ambayo yanawaweka hatari ya kipindu pindu na magonjwa mengine zaidi. Katika kanda ya Somali walioweza kuthibitisha zaidi ya kesi 1,000 za ugonjwa wa surua na vifo vya watoto 16. Lakini hata hivyo si tu suala la utapia ml ona magongwa yanyohatarisha maisha ya watoto. Suala jingine ni kwamba zaidi ya watoto 600,000 wa kanda zilizokumbwa na ukame wanaacha chule kwa sababu ya ukame huo. Shule zimefungwa kwa sababu ya ukosfu wa machi na watoto wengi wanaacha shule kwa sababu wanapaswa kutembea umbali mrefu katika kutafuta hakula na maji au, kuwale wadogo za ona wawtoto wengine wakati wazazo wao au walezi wao wanaondoka kwenda kutafuta maji kwa ajili ya familia na mifugo yao kwa ujumla.
UNICEF kuwkeza katika mifumo ya maji kwa kutumia mfumo wa nguvu ya Solar
Bi Russell ameeleza kwamba kusafikai kwa umbali mrefu sana, unawaweka watoto katika hatari, zikiwemi zile ya ndoa za utotoni. Hii ni kwa sababu mara nyingi vinaongezeka zaidi vipindi vya ukame, na kwa sababu familia zao wanawaoza watoto wao wa kike wakiwa na matumaini kwamba wanaweza kumwilishwa na kulindwa na wao kupata fedha za mahari. Katika maeneo mengine ya liyokumbwa na ukame huko Ethiopia kuna ongezeko la ndoa za utotoni kwa wasilimia 51%. Katika kutoa jibu, mhimili huu wa UNICEF nchini Ethiopia una lengo la kuwafikia idadi karibia milioni 3,4 za watu, miongini wamo milioni 1,4 za watoto kama sehemu yake ya jibu la haraka. UNICEF iko inajitahidi kurudisha na kuweka visima kwa kupeleka maji ya dharura, kuwatibu watoto wenye utapiamlo wa kukithiri na kutoa msaada wa mafunzo na ulinzi wa watoto. UNICEF vile vile iko inawekeza mifumo ya maji kwa njia ya nguvu za Solar ngumu ili kutoa suluhisho la uendelevu wa muda mrefu.
Pongezi kwa afadhili na kuomba juhudi za kutenda zaidi
Kufuatia na juhudi hizo, ndipo Mkurugenzi mkuu amepongeza ukarimu wa msaada kwa wafadhili lakini pia kwamba wanapaswa kufanya zaidi ili kusalidia maisha ya mamilioni ya watoto. Lazima wakumbuke kuwa nyuma ya kila takwimu kuna mtoto mmoja mwenye tumaini sawa na ndoto sawa za watoto wa ulimwengu mzima na wanayo haki sawa ya kufikia nguvu yao kamili. Katika ziara ya Mkurugenzo Mkuu wa UNICEF alikutana na wahusika wa Serikali akiwemo hata Rais wa Ethiopia Bi. Sahle-Work Zwede, Naibu Waziri Mkuu, na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, Demeke Mekonnen Hassen na katika Mikutanoa yao hiyo Bi Russell alijadili juu ya ushirika wa muda mrefu na UNICEF na serikali na jinsi gani ya kuongeza nguvu za kutoa jibu la pamoja katika suala la ukame na kuwekeza katika ujenzi wa maisha ya watu.