Wakati wa kuzindua kiwanda cha kwanza cha kutengeneza chanjo ya UVIKO huko Afrika Kusini Jumatano tarehe 19 Januari 2022 Wakati wa kuzindua kiwanda cha kwanza cha kutengeneza chanjo ya UVIKO huko Afrika Kusini Jumatano tarehe 19 Januari 2022  

Afrika ya Kusini kuwa Nchi ya kwanza barani Afrika kutengeneza chanjo ya Uviko

Kiwanda cha kwanza cha chanjo ya UVIKO-19 barani Afrika kitatengenezwa nchini Afrika Kusini.Ni katika harakati za mapambano dhidi ya gonjwa hili ambalo limeona nchi hiyo kuongoza maambukizi kwa kipindi chote. Kiwanda hicho kinafadhiliwa na mmilionea mmoja wa bayoteknolojia Patrick Soon-Shiong.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika harakati za mapambamo ya upatikanaji sawa wa chanjo za UVIKO -19, ambazo zimeiina nchi ya Afrika Kusini katika mkakati huo, hatimaye imezindua kiwanda cha kwanza katika bara Afrika siku ya Jumatano tarehe 19 Januari 2022 huko Cape Town ambacho kitatengeneza dozi kuanzia mwanzo hadi mwisho na ambacho kinafadhiliwa na mmilionea  mmoja wa bayoteknolojia Patrick Soon-Shiong.

Mwanzilishi wa NantWork Dk Patrick Soon -Shion na Rais Ramaphosa wakati wa kuzinduzi wa Kiwanda cha Madawa, huko Cape, Afrika Kusini
Mwanzilishi wa NantWork Dk Patrick Soon -Shion na Rais Ramaphosa wakati wa kuzinduzi wa Kiwanda cha Madawa, huko Cape, Afrika Kusini

Dozi bilioni moja kwa mwaka ifikapo mwaka 2025

Kwa mujibu wa mfanyabiashara huyo kutoka Marekani lakini mwenye asili ya China, na ambaye alizaliwa Afrika Kusini amesema kuwa “Lengo ni kuzalisha chanjo ya kizazi cha pili, na tunataka kuitengeneza barani Afrika, kwa ajili ya Afrika, na kuisafirisha ulimwenguni kote”, Chanjo za kwanza zitatolewa mwaka huu na lengo ni kufikia dozi bilioni moja kwa mwaka ifikapo mwaka 2025.

Mwanzilishi wa NantWork Dk Patrick Soon -Shion akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kiwanda cha Madawa, huko Cape, Afrika Kusini
Mwanzilishi wa NantWork Dk Patrick Soon -Shion akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kiwanda cha Madawa, huko Cape, Afrika Kusini

Ramaphosa: Leo tunathibitisha kwamba tunajitosheleza kama bara

Kufuatia na tukio hilo, naye Rais wa Afrika Kusini Bwana Cyril Ramaphosa alisema: “Leo tunathibitisha kwamba tunajitosheleza kama bara, na tunapaswa kujivunia kile tunachofikia,". Nchi ya Afrika iliyoathiriwa zaidi na virusi hivyo, ina zaidi ya kesi milioni 3.5 ikiwa ni pamoja na vifo 93,400, wakati bara la Afrika lilirekodi kesi zaidi ya milioni 10 mwezi Januari, kulingana na taarifa za Umoja wa Afrika. Hata hivyo maambukizi yameongezeka tangu kirusi kipya cha aina ya Omicron kilipogunduliwa nchini Afrika Kusini mwishoni mwa mwezi Novemba 2021.

Mwanzilishi wa NantWork Dk Patrick Soon -Shion na Rais Ramaphosa wakati wa kuzinduzi wa Kiwanda cha Madawa, huko mji wa Cape Afrika Kusini
Mwanzilishi wa NantWork Dk Patrick Soon -Shion na Rais Ramaphosa wakati wa kuzinduzi wa Kiwanda cha Madawa, huko mji wa Cape Afrika Kusini
20 January 2022, 14:20