RAI WA ZAMANI WA AFRIKA KUSINI DE KLERK AMEFARIKI DUNIA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 85 KWA SABABU NA SARATANI RAI WA ZAMANI WA AFRIKA KUSINI DE KLERK AMEFARIKI DUNIA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 85 KWA SABABU NA SARATANI 

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Bwana De Klerki amefariki akiwa na umri wa miaka 85

Bwana Frederik W. De Klerk Rais wa zamani wa Afrika kusini amefariki akiwa na umri wa miaka 85,kwa mujibu wa, taasisi yake ilitangaza alhamisi 11 Novemba 2021kuwa alifariki baada ya kupambana na ugonjwa wa saratani.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

rRais wa zamani wa Afrika Kusini Bwana Frederiki de Klerk, ambaye pia alikuwa mhusika mkuu katika kipindi cha mpito cha taifa kuelekea demokrasia, alikuwa amegubduliwa na saratani mwaka huu, kulingana na msemaji wa Taasisi yake. Bwana de Klerk alikuwa mkuu wa nchi kati ya Septemba 1989 na Mei 1994. Mwaka 1990 alitangaza kumwachilia huru kiongozi aliyepinga ubaguzi wa rangi, Hayati Nelson Mandela, na kusababisha kura za vyama vingi mwaka 1994.

RAIS WA ZAMANI FREDERIK W. DE KLERK AMEAGA DUNIA
RAIS WA ZAMANI FREDERIK W. DE KLERK AMEAGA DUNIA

Taarifa kutoka mhusika wa rais huyo wa zamani Frederik de Klerk siku ya Alhamisi asubuhi  tarehe 11 Novemba 2021 ilisomwa: “Rais wa zamani Frederick de Klerk alifariki kwa amani nyumbani kwake huko Fresnaye (Cape Town) mapema leo asubuhi kufuatia mapambano yake dhidi ya saratani ya mesothelioma.” De Klerk alitangaza kukutwa na maradhi ya saratani wakati wa kusherekea miaka 85 ya kuzaliwa kwake, mnamo tarehe 18 Machi mwaka huu.

RAIS WA ZAMANI FREDERIK W. DE KLERK NA NELSONO MANDELA WAKIPOKEA TUZO YA AMANI YA NOBEL 1993
RAIS WA ZAMANI FREDERIK W. DE KLERK NA NELSONO MANDELA WAKIPOKEA TUZO YA AMANI YA NOBEL 1993

Raii wa Zamani huyo anakumbukwa zaidi kwa hotuba yake maarufu aliyoitoa tarehe 2 Februari mwaka 1990, akitangaza kuondolewa marufuku dhidi ya chama cha African National Congress (ANC) na vyama vingine vilivyokuwa vinatetea ukombozi. Katika hotuba hiyo hiyo, aliamuru kuachiliwa kutoka jela kwa Mandela aliyekuwa akipinga ubaguzi wa rangi baada ya kifungo cha takriban miaka 27.

RAIS WA ZAMANI FREDERIK W. DE KLERK NA NELSONO MANDELA WA AFRIKA KUSINI
RAIS WA ZAMANI FREDERIK W. DE KLERK NA NELSONO MANDELA WA AFRIKA KUSINI

De Klerk na rais wa kwanza mweusi wa Afrika kusini Bwana Nelson Mandela walipata wote Tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1993 kwa kuongoza mabadiliko makubwa kutoka kwa utawala wa wazungu walio wachache nchini humo.

12 November 2021, 10:18