Kampeni ya chanjo dhidi ya virusi  nchini Myanmar inaendelea japokuwa inasemekana katika wiki mbili zijazo,nusu ya watu wake,milioni 54 wanaweza kuambukizwa kwa mujibu wa Ripoti ya Uingereza. Kampeni ya chanjo dhidi ya virusi nchini Myanmar inaendelea japokuwa inasemekana katika wiki mbili zijazo,nusu ya watu wake,milioni 54 wanaweza kuambukizwa kwa mujibu wa Ripoti ya Uingereza. 

Covid:London imetuma dozi milioni 9 za chanjo ya AstraZeneca Asia,Kenya na Jamaika

Ripoti ya REPAM inaonesha kwamba katika eneo la Pan Amazonia,watu 100,000 wamekufa na watu milioni 3.5 wameambukizwa zaidi,wakati huo huo Uingereza imetuma dozi milioni 9 za chanjo ya AstraZeneca katika nchi za Bara la Asia,Kenya na Jamaika.Nchini Myanmar,katika wiki mbili zijazo,nusu ya watu wake,milioni 54 wanaweza kuambukizwa kwa mujibu wa ripoti ya Uingereza.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Chanjo ya AstraZeneca imetolewa katika nchi za Bara la Asia, Kenya na Jamaika. Hii ni sehemu ya kuanza kwa habari zaidi,  juu ya upatikanaji wa chanjo katika nchi zilizo maskini na kwenye mpango wa COVAX. Hali halisi ni ya kukatisha tamaa nchini Myanmar, kwani katika wiki mbili zijazo, nusu ya Watu wake, milioni 54 wanaweza kuambukizwa, kulingana na ripoti ya Uingereza. Na katika eneo la Pan-Amazonia, ripoti ya REPAM, Barani Amerika Kusini inaonesha kwamba watu 100,000 wamekufa na watu milioni 3.5 wamezidi, walioambukizwa na Covid-19.

Nchini Siria, watu 23 wameuawa katika mapigano kati ya vikosi vya wanajeshi na waasi katika mkoa wa Deraa, makao ya uasi dhidi ya Rais Bashar Al Assad.  Nchini LEBANON, kumeongezaka moto katika msitu mkubwa na kuzidisha mgogoro mkubwa ambao  tayari ulikuwapo wa kiuchumi. Tarehe 4 Agosti ijayo ni kumbukumbu ya kwanza ya mlipuko wa moto katika bandari ya Beirut nchini humo. Na nchini NIGER, watu 19 wameuawa siku ya Jumatano na watu wenye silaha katika mkoa wa Banibangou, mpakani mwa Mali, na katika eneo hilo hilo watu 14 walikuwa tayari wameuawa siku ya Jumapili iliyopita. Kwa upande wa HALI YA HEWA, mito inayofurika nchini Afghanistan imesababisha vifo 40 na watu 150 kupotea; wakati nchini China, idadi ya waliokufa kutokana na mafuriko ya wiki iliyopita imeongezeka hadi kufikia vifo vya watu 99.

30 July 2021, 14:57